Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Correction: Ni Megawati 2,115 na sio Megawati 2,100 kama ulivyoandika.
 
[emoji1361][emoji1361][emoji1361][emoji1361]
 
Kikwete alitudanganya na Gesi ya Mtwara Hadi Leo
Gesi iliyopo ni ya kupikia tu
Tusidanganyane kila kitu kina side effects zake
Bora Magufuli alithubutu Hawa wengine wametunyoa tu Wakaondoka zao
 
Hizo lita zinazopotea ni kwa muda mfupi tu ujao mkuu,we need something sustainable.Kwa hali ya sasa ya Climate Change terrorism by Geo-engineers,Hydropower generation sio sustainable kabisa,so sio busara ku-invest kwenye Hydropower.

Kwa kiasi kikubwa gas power na geo-thermal power generation ndio sources reliable zaidi kwa kuwa zote zinatumiwa maji kidogo kwa kuwa the water is recycled.
 
Akili yako haina maarifa
 
Misri lile bwawa lao la kufua umeme katika mto Nile walijenga juu ya miti?. Ghana na Zimbabwe yale mabwawa makubwa walijenga kwenye hewa bila kukata miti?

Ulaya miradi mikubwa ya nyuklia wanajenga hewani? Acha kushikiwa akili we dogo
Unazungumzia Aswan Dam la Misri? Hiyo miti ya kukata Aswan ingetoka wapi? Unajua kuwa mpaka hivi leo faida ya huu mradi bado watu wanajiuliza? Majengo na makazi mengi ya kihistoria yalipotezwa katika huu ujenzi? Ingawa mradi umeondoa athari za mafuriko lakini vile vile umezuia rutuba zilizokuwa zinaletwa na mto Nile ( hili nalo tutaliona katika Rufiji Delta). Unajua pia kuwa asilimia 85 ya maji yanayojaza mto Nile yanatoka Blue Nile ambao unaanzia Ethiopia ambako nao wamejenga Dam yao?

Akosombo Dam limeongeza matetemeko, limepunguza rutuba down stream na hivyo kulazimisha matumizi ya mbolea ambayo imeathiri udongo, mvua imepungua na joto limeongezeka katika eneo la bwawa na magonjwa kama bilharzia na malaria yameongezeka?

Kariba Dam nayo ina matatizo kama hayo. Na mbaya zaidi kulikuwa na dalili kuwa msingi wake unaathirika na hivyo kuwepo uwezekano wa ku collapse. Na kuhusu ule umeme wa uhakika? Zimbabwe na Zambia Sasa hivi wana shida kubwa ya umeme!

Na ndio bila shaka miti ilikatwa wakati wa ujenzi wa baadhi ya mabwawa haya lakini wakati ule athari za ukataji miti ulikuwa hazijulikani kama huu wakati. Sasa hivi hatuwezi kujitetea kuwa hatukujua kuhusu athari za mabwawa makubwa. Tuliambiwa tukaleta ubishi.

Miradi ipi ya nyuklia Ulaya unayojua yamejengwa porini? Au yaliyolazimu miti mingi ikatwe kwa ajili ya ujenzi wa barabara?

Huu mradi utatuletea matatizo makubwa huko mbeleni. Huu mradi ni albatross yetu. Na hautajaa katika misimu miwili.

Amandla...
 
Ukikumbuka yaliyokuwa yanaahidiwa wakati wa mradi wa gesi, bandari ya bagamoyo, mabasi ya mwendokasi, treni ya Mwakyembe, Sullivan Summit, ugunduzi wa gesi mtwara, na mengine mengi kuhusu miradi ya namna hii inayopigiwa chapuo kuwa ni muarobaini, hutojihangaisha na hili pia. Bahati mbaya si wanasiasa au wataalamu wote lugha zao moja.
 
Mi nashangaa kila siku watu wanalilia gesi ya mtwara, magufuli kaondoka, nchi imerudishwa kwa wenyewe, endelezeni sasa mlipoishia, zalisheni hio gesi tusambaze Africa, Bado Africa ni dark continent, karibu kila nchi ina upungufu wa umeme, muombeni mchina awauzie hio gesi Kama mlivyokubaliana, tunataka umeme wa uhakika na nafuu basi
 
Jinyonge sasa, bwawa limeshajengwa
 
Nachelea kusema unafikiria na matako, Wewe ni aina ya viongozi ambao watapenda kuona Tanzania haipigi hatua milele katika ramani ya dunia
 
Milion 4 tena [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hiyo hesabu ya 11 Trilioni umeitolea wapi? Inaonekana aliyekulipa amekulipa mpaka za ziada.
 
Sehemu ilipokatwa miti kutakuwa ziwa lenye urefu wa kilomita 100. Ziwa victoria lina ukubwa wa kilomita za mraba 68,000 na eneo lote ni maji na hakuna miti lakini maeneo yanayozunguka ziwa Victoria mvua huwa inanyesha ya kutosha.
 
Mafisadi ya gesi yanapinga sana huu mradi.

Mnatudanganya na ishu ya miti wakati hata hiyo gesi haitatunufaisha kwa namna yeyote.
Kama issue ni miti kanda ya ziwa kusingenyesha mvuq kabisa maana ziwa Victoria lenye kilomita za mraba 68,000 hakuna miti ni maji lakini mvua zinanyesha kwa wingi.
 
Maji yanatoka wapi ,na hii changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi ?
Bwawa la kuhifadhi maji lina mrefu wa kilomita 100 ni kama kutokea Dar hadi Chalinze na litakuwa ziwa kubwa kuzidi ziwa Rukwa. Maji yake yakijaa yatazalisha umeme mwaka mzima bila hata mvua kunyesha kwa mwaka mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…