Moshi25
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,555
- 4,118
Tunajua matatizo yetu na sababu ni NyerereUthibitisho kuwa hatuwezi kutatua matatizo yetu maana hata hatujui tuna matatizo gani.
1. Ujamaa
Huu ni upumbavu, huwezi kufundisha maskini kugawana umaskini, Mwl hakuelewa Maana ya ujamaa, (sharing). Ujamaa ni ideology ya kijinga ambayo haitekelezeki na huwezi kupata ujamaa bila kupitia kwanza ubepari. Ukitaka ujamaa ufanye kazi lazima uwanyonge wezi wote wa Mali ya umma kitu ambacho bongo hakifanyiki. Nyerere alianzisha ujamaa bila nchi kuwa tajiri na ya kibepari. Nyerere alianzisha ujamaa na kujenga viwanda vya umma bila kujua human beings are selfish by nature hivyo lazima waibe kwa kuwa ni Mali ya umma ila Mali binafsi utajiibiaje mf Mo Dewji au Bakhressa. Nyerere alipaswa kufundisha raia Ubepari sio ujamaa. Na wazungu hawakumwelewa wakaacha ideology yake iitwe ujamaa japo yeye alimaanisha Socialism! Ubepari hufundisha raia entrepreneurship , uwekezaji hasa katika viwanda, technology , science, bishara, kilimo cha kisasa na makampuni. Ubepari hufundisha juhudi binafsi, kufanya kazi kwa faida na kulipa kodi ambayo serikali hutumia kujenga miundombinu ambayo huboresha biashara na viwanda. Nyerere ndie ameharibu hii nchi kwa kuanzisha ujamaa ambao hakuulewa na ukazalisha ufisadi wa Mali ya umma hadi leo. Mimi nimesoma ulaya na nimejua maana ya socialism na capitalism kuliko Nyerere!
2. Kiswahili
Hii ni sababu ya pili ya umaskini wa bongo. Hii lugha tunaongea nyumbani na inatuunganisha kama taifa hiyo ingetosha ila haikupaswa Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia maana lugha ya Dunia ni English. Elimu kubwa ya Dunia Iko kwa kiingereza, vitabu vingi vya science na technology viko in English. kazi ni nyingi nje ya nchi zinahitaji mtu kuongea English. Nyerere hakutaka wabongo kuondoka nchini bali wawe maskini wakae wamtukuze.
3. Udini
Hili ni tatizo kubwa Sana. Nyerere alikuwa mdini Sana kupitia majina katika mitihani, watu wengi hawakupenya! Ukiangalia uwiano wa watu walio katika mfumo RASMI wa kazi za mshahara asilimia 70 hadi 80 ni wakristo. Je watu wa dini zingine hawana akili? Kwanini hawapewi kazi? Serikalini fanya takwimu utaona, kila ofisi wakristo 10 mwislam au mpagani mmoja, kwaya zinapigwa ofisini wengine zinaboa sana. Hivyo akili ya maendeleo ya bongo ni ya dini moja tu na huu ufisadi ni wao wenyewe watupu. Ukibisha ni juu yako.
4. Wazee ni viongozi
Mwalimu wangu wa saikolojia alisema mtu akifikisha miaka 50 anakuwa mbinafsi na anawaza kufa tu maana jioni inaanza kuingia, Sasa bongo imejaa watunga sera wazee watupu Tena waliosoma enzi za ukoloni, wanachotaka ni kutukuzwa na kusifiwa tu, lazima waibe wawe na Mali nyingi tuwasifie na kuwatukuza, wanachowaza wazee Hawa viongozi si kujenga nchi bali matumbo yao tu na ten percent. Ukibisha ni juu yako.
Wengine ongezeeni!