Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Uthibitisho kuwa hatuwezi kutatua matatizo yetu maana hata hatujui tuna matatizo gani.
Tunajua matatizo yetu na sababu ni Nyerere

1. Ujamaa

Huu ni upumbavu, huwezi kufundisha maskini kugawana umaskini, Mwl hakuelewa Maana ya ujamaa, (sharing). Ujamaa ni ideology ya kijinga ambayo haitekelezeki na huwezi kupata ujamaa bila kupitia kwanza ubepari. Ukitaka ujamaa ufanye kazi lazima uwanyonge wezi wote wa Mali ya umma kitu ambacho bongo hakifanyiki. Nyerere alianzisha ujamaa bila nchi kuwa tajiri na ya kibepari. Nyerere alianzisha ujamaa na kujenga viwanda vya umma bila kujua human beings are selfish by nature hivyo lazima waibe kwa kuwa ni Mali ya umma ila Mali binafsi utajiibiaje mf Mo Dewji au Bakhressa. Nyerere alipaswa kufundisha raia Ubepari sio ujamaa. Na wazungu hawakumwelewa wakaacha ideology yake iitwe ujamaa japo yeye alimaanisha Socialism! Ubepari hufundisha raia entrepreneurship , uwekezaji hasa katika viwanda, technology , science, bishara, kilimo cha kisasa na makampuni. Ubepari hufundisha juhudi binafsi, kufanya kazi kwa faida na kulipa kodi ambayo serikali hutumia kujenga miundombinu ambayo huboresha biashara na viwanda. Nyerere ndie ameharibu hii nchi kwa kuanzisha ujamaa ambao hakuulewa na ukazalisha ufisadi wa Mali ya umma hadi leo. Mimi nimesoma ulaya na nimejua maana ya socialism na capitalism kuliko Nyerere!

2. Kiswahili

Hii ni sababu ya pili ya umaskini wa bongo. Hii lugha tunaongea nyumbani na inatuunganisha kama taifa hiyo ingetosha ila haikupaswa Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia maana lugha ya Dunia ni English. Elimu kubwa ya Dunia Iko kwa kiingereza, vitabu vingi vya science na technology viko in English. kazi ni nyingi nje ya nchi zinahitaji mtu kuongea English. Nyerere hakutaka wabongo kuondoka nchini bali wawe maskini wakae wamtukuze.

3. Udini

Hili ni tatizo kubwa Sana. Nyerere alikuwa mdini Sana kupitia majina katika mitihani, watu wengi hawakupenya! Ukiangalia uwiano wa watu walio katika mfumo RASMI wa kazi za mshahara asilimia 70 hadi 80 ni wakristo. Je watu wa dini zingine hawana akili? Kwanini hawapewi kazi? Serikalini fanya takwimu utaona, kila ofisi wakristo 10 mwislam au mpagani mmoja, kwaya zinapigwa ofisini wengine zinaboa sana. Hivyo akili ya maendeleo ya bongo ni ya dini moja tu na huu ufisadi ni wao wenyewe watupu. Ukibisha ni juu yako.

4. Wazee ni viongozi

Mwalimu wangu wa saikolojia alisema mtu akifikisha miaka 50 anakuwa mbinafsi na anawaza kufa tu maana jioni inaanza kuingia, Sasa bongo imejaa watunga sera wazee watupu Tena waliosoma enzi za ukoloni, wanachotaka ni kutukuzwa na kusifiwa tu, lazima waibe wawe na Mali nyingi tuwasifie na kuwatukuza, wanachowaza wazee Hawa viongozi si kujenga nchi bali matumbo yao tu na ten percent. Ukibisha ni juu yako.

Wengine ongezeeni!
 

Kweli mwalimu alifanikiwa kutuunganisha na kuwa taifa moja, tukazungumza kiswahili taifa zima.
Ila hapo kwenye umasikinishaji ndo naumia zaidi nikikumbuka nyuzi nilizosoma humu zikieleza sababu, nia na mbinu alizotumia mwalimu kuua vyama vya ushirika! SHIREKU, NYANZA, KNCU malizieni na nyingine...
 

That went over your head. Logic ni ile ile, mmepata maraisi wangapi toka JKN? Wote hao wameshindwa kurekebisha mapungufu yake? Nyerere alikaa madarakani 25yrs only, miaka mingine 35 ya kujiendesha wenyewe bado mnamlaumu JKN? Hamuoni hapo tatizo ni nyie kwa kushindwa kujiendsha? Playing blamegame au victimhood ni trait namba moja ya watu wavivu wa kufikiri wanaamini kila failure yao ni kosa la mtu mwingine. Msipojua hili huwezi kuendelea individually au collectively.
 
Ni njia gani itatumika kuiondoa CCM madarakani na kufanikiwa ?
 
Wacha uzushi. Nyerere hakujenga viwanja vya mpira bali alijenga shule za sekondari zenye vifaa na na vyuo vingi sana nchi nzima; wakati Nyerere anaondoka madarakani, hakuna mkoa ambao haukuwa na sekondari ya serikali. Vile vile alijenga utaratibu imara wa kuaweliemisa wazee ambao hawakupata nafasi ya kwenda shuule kwa kupitia elimu ya watu wazim na kuwahimiza sana kujenga tabia ya kujisomea. Aliandika vijitabu vingi sana kuwataka raia wavisome. Alivyoondoka madarakani mambo yakaanza kwenza mzobamzoba hadi Magufuli alivyaamsha tena halafu leo mnataka kurudisha Nyerere kwenye siasa?

Mama huyu nchi imeanza kumshinda hadi anahamisha sera kwenda kwenye vita ya kidni na lawama zote azirudiesha kwa Nyerere ambaye aliondoka madarakani miaka 41 iliyopita hata wewe mwenyewe unayeandika makala hii hujazaliwa. Kikwete mwenyewe ambaye ndiye godfather wenu humu ndani alisomeshwa na Nyerere. Uongozi bila akili na busara ni mzigo mkubwa sana. Mara nyingi tukiwa na rais mwislamu basi nchi huanza kuyumba kwa misimamo ya kidini mano. Kikwete alijitahidi sana kuidhibi, lakini Mwinyi alishindwa hadi bucha za nguruwe kuvunjwa kiholela. Sasa hivi yale ya Mwinyi yanaanza kuibuka tena.
 
Nyerere alikaa madarakani miaka 24, na kati ya hiyo 24, mmoja ulikuwa ni chini ya Malkia, na mwingine miwili kabla ya Muungano, kwa hiyo effective term yake ilikuwa ni miaka 21 tu.
 
Kila siku nalisema hili Nyerere ndo katufikisha hapa hakutaka watanzania wajitegemee alitaka tuitegemee serikali kwa kila kitu ona sasa
 
kwani we ni raia wa nchi gani?
 
Hayo yote hayakusaidii. Pambana na hali iliopo sasa ili kuwe na kesho bora kwa wanao. We umekalia kumlaumu marehemu tu itakusaidiaje kwa mfano?
Nyie ndio ambao mnataka wakina Mbowe waandamane on your behalf huku nyie mmekaa tu kama mazombi.
Sahihi kabisa, Nyerere hayupo tena muhimu zaidi ni sisi tuliopo tutengeneze kesho yetu iliyo bora.
 
Kuendelea kumlaumu Nyerere miaka 60 baada ya uhuru ni sawa na kumlaumu babu yako for your failures. Baba yako had an opportunity na wewe ushakua mtu mzima you can correct them as well. Cheap excuses ndo zinafanya muendelee kuwa hapo mlipo.
Good message
 
🤜🤛👍
 
Nyerere alikaa madarakani miaka 24, na kati ya hiyo 24, mmmoja ulikuwa ni chini ya Malkia, na mwingine miwili kabla ya Muungano, kwa hiyo effective term yake ilikuwa ni miaka 21 tu.
21 yrs na bado kazidiwa maendeleo na JPM 5yrs na Samia 2 yrs
 
Sahihi kabisa, Nyerere hayupo tena muhimu zaidi ni sisi tuliopo tutengeneze kesho yetu iliyo bora.
Damage aliyoifanya ni kubwa mno kuweza ku resolve hiyo damage ni kuwa na katiba mpya yenye kujali maslaho ya taifa. Siyo katiba hii ya kumlinda mtu mmoja.
 
Uko wrong. Nyerere was the best president followed by JPM
 
21 yrs na bado kazidiwa maendeleo na JPM 5yrs na Samia 2 yrs
Siyo kweli;ilikuwa ni mazingira tofauti sana kati ya nezi za Nyerere na enzi za leo. Ungewapa JPM na Samia kutawala nchi hii enzi za Nyerere huenda ingewashinda kabisa.
 
Nyerere alikuwa na utu, alithamini watu wote sawia na alichukia ufisadi na ubadhrifu toka ndani ya moyo wake je hao akina Lowasa anaowasifia wametajwa kuhusika na wizi wa mali ya uma mara ngapi na hawajakanusha, je hivyo walivyoiba si wangevifanya vya uma kiwango cha umasikini kingepungua?
 
Siyo kweli;ilikuwa ni mazingira tofauti sana kati ya nezi za Nyerere na enzi za leo. Ungewapa JPM na Samia kutawala nchi hii enzi za Nyerere huenda ingewashinda kabisa.
Kipindi cha Nyerere mpaka anang'atuka literacy rate ilikuwa chini ya 50%. Hapa unasemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…