Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Korea Kaskazini ya Kiduku ni masikini kuliko Tanzania, imezidiwa kwa kila kitu na Tanzania kasoro kutengeneza mabomu tu kama mwendawazimu.

Tumeizidi Korea ya Kiduku kwa GDP.
Vitu pekee tulivyo izidi NK ni idadi ya watu, ujinga na upumbavu
 
Hizi pumba tupu,its all about maslahi.
 
Unafahamu kwamba wazee wetu walisomeshwa na serikali kuanzi elimu ya msingi hadi chuo kikuu bure,unafahamu kwamba Nyerere alitaifisha shule zilizokuwa zinamilikiwa na taasisi za kidini ziwe shule za umma?
 
Acha lawama wewe umelifanyia nini hili taifa hadi sasa kulekebisha hayo makosa,kumbuka Nyerere hakuwa malaika pia kulikua na mambo mengi sana ya kuwrka sawa katika taifa hili,asingeweza kufanya yote kwa usawa.

Acha unafiki
 
Hapa ndipo matatizo yanapoanzia.
Niambie sasa Nyerere alijenga shule ngapi za msingi ili watanzania waondoe UJINGA?

Kwanini aliweza kujenga ofsi za chama kila kijiji lakini akashindwa kujenga shule kila kijiji?

Wakati wa Nyerere mwananchi kupata elimu ilikuwa ni bahati na siyo haki.

Kuna mikoa kadha wa ladha Nyerere aliitenga. Hakukuwa na shule huko kigoma, Sumbawanga, Lindi nk. Hivi unategemea watu wa maeneo hayo wangepata wapi elimu?

Shule nyingi zililuwa mikoa ya Kilimanjaro na Kagera tu. Na hizo zilijengwa na wakoloni kwa strategy zao.

Nyerere ali fail pakubwa mno kwenye Elimu.
 
Sema yote ila Baba wa taifa hili atabaki kuwa Nyerere,
 
Acha lawama wewe umelifanyia nini hili taifa hadi sasa kulekebisha hayo makosa,kumbuka Nyerere hakuwa malaika pia kulikua na mambo mengi sana ya kuwrka sawa katika taifa hili,asingeweza kufanya yote kwa usawa.

Acha unafiki
Mimi sijawahi kuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania. Ningepata nafasi hiyo hakika ningetengeneza Taifa la wasomi.
 
Tatizo lako mwenzangu huwa unaweka tu maandishi. Hapa tunajibishana kwa hoja. Niambie Nyerere alilifanyia nini taifa hili katika sera yake ya kuondoa
1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI?

Yerere alikuwa muongeaji mzuri tu lakini siyo mtekelezaji.

Kwakuwa umeamua kujivika unafiki na kuyatazama mapungufu ya Nyerere kamwe huwezi ona mazuri yake pia. Hatupo hapa kukufundisha historia ya nchi ila vitabu viko vingi sana vimeelezea historia ya nchi tangu uhuru.
 
Hapa ndugu yangu naongelea Elimu. Mambo mengine wewe yalete tujadili. But ukweli lazima usemwe.

Wewe leta evidence kuonesha namna gani Mwalimu Nyerere alijenga elimu katika nchi hii.

Kama alishindwa kufanya hivyo unataka tukae kimya? Lazima tuseme ilituweze kujifunza na kutafuta namna ya kuondokana na zimwi hili.
 
Kwahiyo mtu akija kwako kutaka kuchukua ardhi yako utamchekea??utakua mpuuzi wa namna gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…