Nyerere unamuonea bure.
Nyerere amekuta nchi iko so disorganized, magonjwa, ujinga, umaskini wa kutupwa na ukabila
Nyerere alikua na mlima mrefu sana wa kupanda, kwanza kuhakikisha chembechembe za ukabila zinakufa na kuleta umoja, kupambana na ujinga, kuhakikisha watu wanajua hata kusoma na kuandika. Ulitaka awape elimu gani kama hata kusoma na kuandika hawajui? Ulitaka awape elimu ya uraia wakati hata kusoma hawajui?
Mwalimu kakuta pepopunda, surua, polio, kifua kikuu, kifaduro, kwashakoo na magonjwa mengine yametamalaki kwa watanzania, ulitaka awape alimu ya uraia huku akiwaacha wafe?
Mwalimu kakuta Watanzania ni mafukara wa kutupwa, hawana matumaini ya kesho, akaanzisha vijiji angalau wawe pamoja ili iwe rahisi kuwaletea maendeleo kwa sababu walikua so scattered and disorganized, akaanzisha mashamba ya ushirika ama sustainable farming, akahakikisha anapeleka watu shule wakasome waje wampokee ma kubadilisha nchi kina Chenge na wengine, matokeo yake, wamekua wezi.
Nyerere alipigana kuanzisha viwanda, mashamba ya vijiji, na mambo mengine mengi bila kuuza ardhi hata kipande kimoja kwa waarabu wala wazungu.
That man died poor, had nothing kwa kuwapigania Watanzania
Na alivyokua mwema yule bwana, alipotoka madarakani aliangalia nyuma, akaona failures zake na success zake, akakiri kwamba kweli kuna mahala alifeli, na sababu kubwa za failure za mwalimu zilikua nje ya uwezo wake, kumbuka oil crisis and financial crisis za 70s and 80's.
Yule jamaa alipoona he can continue failing, akajipumzikia yeye mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yeyote. Angeweza kufia madarakani.
Tukubaliane kwamba CCM ndio ya kulaumiwa, ila kumpa Nyerere zigo la lawama ni kumuonea. Yule bwana aliachia hii nchi miaka zaidi ya 35 iliyopita, hao wengine waliofuata walifanya nini?