Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Waliokuja baada ya Nyerere ndio walioiharibu hii Nchi !!
Nyerere alikataa madini yasichimbwe mpaka wenyewe wenye Nchi waelimike na kujua thamani zake ndio yaje yachimbwe,
Lakini badala yake kila mtu anajua nini kilitokea !! 3% !!!!!!
Hakika
 
Kama ni mtu wa kusoma historia vizuri. Mwalimu Nyerere alikuwa na shida kubwa ya uoga. Nawaomba muende mkasome historia ya Bi. Fatima Matola, namna alivyopigania uhuru wa Tanganyika.

Tena issue ya ukabila tusiliongelee kabisa hapa tuongelee namna Mwalimu alivyo fail kujenga taifa la wasomi. Na je, tufanye nini sasa kuanzia hapa tulipo?
Mada yako inahitimisha kuwa Nyerere hakuna alichotufanyia Nchi hii,ameturudisha nyuma sanaa,
Wachangiaji wanakujibu mambo aliyoyafanya kwa Nchi hii,unarudi tena eti tuongelee Elimu tu.

Kuna uwezekano mkubwa hata hapo kwenye elimu,bado elimu iliyotolewa kipindi hicho ilikuwa bora na nzuri kuliko hata sasa
 
Unaweza ukaongea kwa kutoa mifano? Elimu ipi ilitolewa kipindi hicho? Niambie shule ngapi za msingi zilijengwa wakati wa Nyerere?
 
Alikuwa na maono ila tu viongozi aliowaweka kusimamia sera zake hawakumwelewa. Wengi walimuangausha. Wakati wake shule za ufundi zilikuwa vizuri kuliko Leo, viwanda vya umma vilikuwa vizuri ila tu wahujumu nao walikuwa kazini. Alijitahidi sana ila alishindwa kuipa lugha ya malkia kipaumbele kama wenzetu majirani.
 
Soma kitabu cha tujisahihishe kasema yote alipofeli na sababu za kwanini alifeli acha kutupa lawama hovyo.
Ndugu yangu kitabu hicho ninacho Nyumbani na ninakisoma kila wakati. Kitabu hicho kiliandikwa mwaka 1962 wakati Nyerere akiwa madarakani mwaka mmoja tu.

Inakuwaje unaingia madarakani mwaka mmoja tu na unaanza kulaumu?

Je, kuna kitabu chochote cha Nyerere alichoandika kuhusu sera ya Elimu Tanzania?

Vitabu vyake vyote vilikuwa na mwelekeo wa kisiasa tu. Hakukuwa na mpango mkakati wa kujenga taifa la wasomi.

Kama mpango huo ulikuwepo naomba uuweke hapa na utekelezaji wake.
 
Yani watu hamtaki ku accept failures zenu, mnafanya blame shifting
Hii mada niliona niipite tu kwakuwa kuanzia mtoa mada na wachangiaji wengi bado wako kwenye "Kati ya pesa na elimu, kipi bora" debate mode ki-primary zaidi.

Pamoja na wao kujisahaulisha UHALISIA lakini pia ni kana kwamba wamegoma kutumia uwezo wao wa kufikiri AU wanafikiri based on what they have seen already.

Ukiwapanga kwa UPIGAJI kazi uliotukuka katika nchi hii, wenye uzalendo na uwajibikaji, dhamira safi ya kuisogeza nchi mbele, basi listi itakuwa
1. JKN
2. JKN
3. JKN
4. JKN
5. Sokoine
6. Sokoine
7. JPM
8. JPM
9. JPM
10. BWM
 
Kakab umenena vyema babangu ni mwana mathematics mzuri sanaaa ila kwakuwa ametoka ktk familia ya kiislamu ilikuwa ngumu kupata mata matokeo ya mtihani wake hakuona jina lake...na wengi walifanyiwa hivi...kifupi ni jamaaa katukosea kila sekta
 
Kwasababu huna faida na nchi hii zaidi ya kulalamikia waliokufa,Nyerere alifanya kwa sehemu yake.
Hata wabakaji maarufu,wauaji, wezi,watukutu n.k nao wanakumbukwa, tumia kichwa chako kufikiri sio kufugia nywele tu.

Usitukuze sana kukumbukwa hata ukiwa mpuuzi kupindukia napo utakumbukwa
 
Hii mada niliona niipite tu kwakuwa kuanzia mtoa mada na wachangiaji wengi bado wako kwenye "Kati ya pesa na elimu, kipi bora" debate mode ki-primary zaidi.

Pamoja na wao kujisahaulisha UHALISIA lakini pia ni kana kwamba wamegoma kutumia uwezo wao wa kufikiri AU wanafikiri based on what they have seen already.

Ukiwapanga kwa UPIGAJI kazi uliotukuka katika nchi hii, wenye uzalendo na uwajibikaji, dhamira safi ya kuisogeza nchi mbele, basi listi itakuwa
1. JKN
2. JKN
3. JKN
4. JKN
5. Sokoine
6. Sokoine
7. JPM
8. JPM
9. JPM
10. BWM
Mzee bado hujaongelea chochote hapa. Kuhusu elimu. Hapa unataka kuhamisha mada.

Mwalimu Nyerere alikaa kwenye uongozi miaka 24. Alilifanyia nini taifa hili kuhusu Elimu?

Kumbuka alikuwa na sera ya kuondoa Ujinga, Umaskini na Maradhi.

But alifanya nini kuhusu elimu kwa watanzania?
 
Alikuwa na maono ila tu viongozi aliowaweka kusimamia sera zake hawakumwelewa. Wengi walimuangausha. Wakati wake shule za ufundi zilikuwa vizuri kuliko Leo, viwanda vya umma vilikuwa vizuri ila tu wahujumu nao walikuwa kazini. Alijitahidi sana ila alishindwa kuipa lugha ya malkia kipaumbele kama wenzetu majirani.
Nyerere alikuwa mbishi kupindukia mbaya zaidi alikuwa mjinga pasipo kujua dunia inaenda vipi kwa wakati wake.

Alishauriwa na watu wengi ndani ya chama na nje ya chama, ndani ya nchi na nje ya nchi lakini alikomaa na ujinga wake mpaka ukafeli mikononi mwake aliishia kuwaona wabaya wote waliomshauri aachane na ujinga wake.

Magufuli alikuwa second version ya Nyerere kwenye ubishi wa kijinga
 
Ukweli mchungu ,pro ujamaa watakuja kukuambia eti mwalimu aliacha Mali nyingi za umma.
Mwalimu aliacha viwanda vingi, ndege,treni,mabenki na shughuri nyingi zilizokuwa zinaendelea,in between tumekuwa na viongozi wabinafsi kiasi wanaacha treni ife wasafirishe mizigo kwa malori yao na abiria Kwa mabasi Yao,shida ya mwalimu ni kufanya uchaguzi wa kura kutokuwa na maana na nguvu iliyokusidiwa.
 
Nyerere alikuwa mbishi kupindukia mbaya zaidi alikuwa mjinga pasipo kujua dunia inaenda vipi kwa wakati wake.

Alishauriwa na watu wengi ndani ya chama na nje ya chama, ndani ya nchi na nje ya nchi lakini alikomaa na ujinga wake mpaka ukafeli mikononi mwake aliishia kuwaona wabaya wote waliomshauri aachane na ujinga wake.

Magufuli alikuwa second version ya Nyerere kwenye ubishi wa kijinga
Nataka nikuongezee jambo hapa.
Kuna mtu mmoja aliitwa Oscar Kambona. Huyu aliweza kutendewa mambo ya ajabu sana na Mwalimu.

Kambona alipendekeza vyama vingi since independence. Bado Nyerere alikataa. Baada Nyerere aliweza kuwakamata ndugu zake Oscar Kambona na kuwafunga.

Kambona alikuwa Muumini wa kanisa la Anglican na alisomeshwa na viongozi wa Angican masuala ya Sheria huko Uingereza.

Inakuwaje vichwa kama hivi unaamua kuvipoteza kwa matakwa yako Binafsi. Kambona angesikilizwa hakika leo tungekuwa na katiba nzuri na nchi ya wasomi.
 
Mwalimu aliacha viwanda vingi, ndege,treni,mabenki na shughuri nyingi zilizokuwa zinaendelea,in between tumekuwa na viongozi wabinafsi kiasi wanaacha treni ife wasafirishe mizigo kwa malori yao na abiria Kwa mabasi Yao,shida ya mwalimu ni kufanya uchaguzi wa kura kutokuwa na maana na nguvu iliyokusidiwa.
Tuambie sasa aliacha shule ngapi za msingi?
 
Unaweza ukaongea kwa kutoa mifano? Elimu ipi ilitolewa kipindi hicho? Niambie shule ngapi za msingi zilijengwa wakati wa Nyerere?
Wewe mwenye mada nadhani haumlaumu Nyerere bila uthibitisho,naona unakomaa na swali la alijenga shule za msingi ngapi? Bila shaka kabla ya kuleta mada ya kumlaumu kuhusu elimu,utakuwa umeshafanya utafiti ni shule ngapi alijenga.

Kwa hiyo tulitegemea utuambie kwa miaka 24 aliyokaa madarakani alijenga shule kadhaa...na hawa wa baada yake miaka 38 baada yake wamejenga kadhaa..hapo nasi tuseme ni kweli Nyerere hakufanya kitu.

Jambo jingine bayana ni kwamba,hata ukibahatika kupata takwimu ya kutaka kuwatukuza hawa wa baada yake kwamba wamejenga shule za msingi nyingi kila kijiji,lazima utambue vijiji vimeongezeka vingi tu tangu 1985 hadi sasa
 
Mwalimu Nyerere alikaa kwenye uongozi miaka 24. Alilifanyia nini taifa hili kuhusu Elimu?
Unataka kujua idadi ya wasomi kutoka kwenye kipindi chake au ubora wa wasomi waliopatikana kwenye kipindi chake?

Si ajabu kuwa umewahi kusikia watu wakisema, "elimu ilikuwa enzi hizo, darasa la nne enzi zetu ndio kidato chenu cha nne siku hizi"

Baada ya miaka 24, kuna miaka 38 ya tawala za watu wengi tofauti, kwenye elimu, unadhani ujinga unaongezeka au unapungua?

Sahau kuhusu miaka 24(huna unachoweza kulaumu wala kufananisha ukilibganisha na ujinga mwingi ulioendelea kwenye awamu zulizofuata), miaka 38 ya kujitawala, NANI KAFANYA NINI kwenye ELIMU.

Labda ungeniambia hayo ili nijue unatuhumu au unauliza. Kama unatuhumu, weka "ilivyopaswa kuwa na ilivyokuwa", pengine nitafahamu unachojaribu kunielewesha
 
Back
Top Bottom