sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Kwanza nna declare interest mimi ni shabiki mkubwa wa Professor Jay na kwenye list yangu ya MCs bora wa muda wote nimemuweka nafasi ya pili.
Napenda sana muziki wake hata siasa zake nilikuwa nazipenda.
Ila kuna kitu nakiona hakipo sawa baada ya yeye kurudi kwenye ugonjwa uliomuweka kitandani kwa muda mrefu mpaka kuchungulia kaburi, nilitegemea angetulia na apate shughuli za kumuingizia kipato zisizohitaji mikiki mikiki. Wazo lake la Foundation lilikuwa bora kabisa.
Soma Pia: Joseph Haule 'Prof. Jay: Nitagombea Ubunge Mikumi 2025
Nasikitika kumuona kwenye majukwaa ya muziki akifanya performance na pia kwenye majukwaa ya siasa akifanya mikutano.
Kwa yoyote anayemshauri au kumuunga mkono kurudi kwenye hizi shughuli basi hana nia njema na hampendi anataka kumtumia.
Prof pumzika tunaona unavyo struggle kuwasiliana na watu na kujichanganya bado haupo sawa.
Tunaokupenda tunaomba upumzike. Mungu amekutoa kwenye hali ambayo kuendelea kuishi ni kama muujiza. Pesa zipo huwezi kuwa nazo vile vile kila siku kubali ndio maisha na upumzike.
Natoa ushauri huu kwa kuwa nakukubali.