Ukweli usemwe: Nandy ni msanii namba moja wa kike ambaye tumebarikiwa kwa sasa

Ukweli usemwe: Nandy ni msanii namba moja wa kike ambaye tumebarikiwa kwa sasa

Mkuu hivi Rubby alivyotoa wimbo unaitwa na Yule ulikuwa umesha anza kufatilia muziki?
Mkuu underground kuwa na hit song hakumfanyi kuwa ndiyo msanii mkubwa...
Mziki sijaanza kitambo sana.
Nimeanza kipindi wakina James Dandu,John Maganga wanaimba copy viwanja vya Leaders club.Dj akiwa Rankim Ramadhan R.I.P pembeni yupo Bony Love.

Kila zama zina watu wake waku-hits.
Ata enzi za Unique Sisters na Binti Comando walitisha kwa kipindi chao.
Aihitaji nguvu kubwa kutambulisha radha ya" Sukari"mkuu,mtu akilamba tu anajua radha yake.
 
Hapa nakubishia zuchu ana sauti nzuri Sana kuliko nandy Mara ngapi nandy anaharibu kuimba live au mzee baba ufuatilii labda uniambie Ruby sawa.
fatilia show za majukwaani utakuja kusema hapa. ZUCHU kuimba live bado sana anapiga kelele... kaangalie sho zake hata ile ya mlimani
 
Kuanzia kuimba,stage , level za uimbaji, maadhi yao ni tofauti kbisa.
mmoja ni underground mwingine ni msanii mkubwa.
mmoja anaimba taarab mwingine anaimba afro pop.
mmoja kwenye stage ni mchovu kabisa mwingine ana jitahidi sana.
Mmmoja kuimba live awezi kabisa na anaimba vibaya mwingine ni fundi kabisa.
ZUCHU VS NANDY
Kwani kuimba taarabu ni kosa?

Tatizo lako Zuchu wewe umeanza kumsikia akiwa Wasafi.Zuchu ni mmoja ya mshiriki katika shindano la Tecno lilofanyika Nigeria 2015 la kusaka vipaji vya uimbaji Africa na akashika nafasi ya Tatu.

Tokea huko alikuwa anapiga show za live mpaka akafanikiwa kishika nafasi ya tatu na huko alikuwa anaimba hizo nyimbo za Afro pop hata zenye mahazi ya mbele kwani dogo ngeli inapanda.






Na ndio maana hata ktk nyimbo ya Nobody na Sukari ni Afro pop zipo vizuri.
Na sio taarab hata nyimbo zenye swaga za kizungu yupo vizuri (mf karantini).

Tatu Zuchu nyimbo anatunga mwenyewe,Nandy ndiyo ana CV kubwa ila Zuchu tokea mwaka jana na huu mwaka yupo juu mpaka hivi sasa.
 
Maua sana anajua sana Kishinda nandy, ila mzee wa kudaambuaa ni noumaa sana mda sio mrefu zuchu atawafunika wasaani wote wakike maana ni 🔥🔥🔥🔥
Zuchu kidog anaweza kimbizana na Maua Sama , maua Sama fundiii yuleeee, Nandy hamnaaaa na mda utaendelea kuongea , Ruby ndo kabisaa takataka Ile , ifkie hatua tukubaliane na nguvu ya soko na sio maoni yetu ya kijuaji et msanii mkubwa wakat mshale unazd kushuka chini......
 
Kuanzia kuimba,stage , level za uimbaji, maadhi yao ni tofauti kbisa.
mmoja ni underground mwingine ni msanii mkubwa.
mmoja anaimba taarab mwingine anaimba afro pop.
mmoja kwenye stage ni mchovu kabisa mwingine ana jitahidi sana.
Mmmoja kuimba live awezi kabisa na anaimba vibaya mwingine ni fundi kabisa.
ZUCHU VS NANDY
Zuchu anaimba taarabu mkuu , ???
 
Mi kusema kweli wasaniia wa Kike siwakubali kivile especially hawa wanaochepukia.

Ila kuna mpuuzi aliimba pini moja na Mafiq... "...[emoji445]Pesa hunaaaa, una magari mangapiii, yako mapozi tu mi nikupeleke wapii... [emoji445]".. yule demu anajua.
Ila wee kwahiyo mama harrier ni mpuuzi? Lol [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kweli kabisa. Nandy ametulia. Yuko focussed. Ni mjasiriamali with business options. Nasubiri kwa hamu ngoma yake na Koffii Olomide
 
𝐌𝐬𝐚𝐧𝐢𝐢 𝐑𝐮𝐛𝐛𝐲 𝐧𝐢 𝐚𝐥𝐦𝐚𝐬 𝐢𝐬𝐢𝐲𝐨𝐭𝐚𝐦𝐛𝐮𝐥𝐢𝐤𝐚 𝐧𝐚 𝐰𝐞𝐧𝐠𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐤𝐢𝐰𝐚𝐧𝐝𝐚 𝐜𝐡𝐚 𝐌𝐮𝐳𝐢𝐤𝐢 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐮𝐩𝐚𝐧𝐝𝐞 𝐰𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐰𝐚𝐤𝐞!

𝐍𝐢 𝐯𝐢𝐥𝐞 𝐭𝐮 𝐡𝐚𝐢𝐣𝐚𝐩𝐢𝐠𝐰𝐚 𝐩𝐨𝐥𝐢𝐬𝐡 𝐚𝐥𝐦𝐚𝐬 𝐡𝐢𝐢, 𝐚𝐠𝐡𝐚𝐥𝐚𝐛𝐮 𝐢𝐧𝐠𝐞𝐮𝐳𝐰𝐚 𝐛𝐞𝐢 𝐤𝐮𝐛𝐰𝐚 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐬𝐨𝐤𝐨 𝐥𝐚 𝐝𝐮𝐧𝐢𝐚!

𝐍𝐚𝐧𝐝𝐢 𝐧𝐢 𝐝𝐡𝐚𝐡𝐚𝐛𝐮 𝐥𝐚𝐤𝐢𝐧𝐢 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐲𝐨 𝐡𝐚𝐢𝐣𝐚𝐬𝐮𝐠𝐮𝐥𝐢𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐤𝐮𝐩𝐢𝐭𝐢𝐬𝐡𝐰𝐚 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐨𝐭𝐨 𝐢𝐥𝐢 𝐢𝐧𝐠'𝐚𝐞 𝐧𝐚 𝐤𝐮𝐮𝐳𝐰𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐭𝐡𝐚𝐦𝐚𝐧𝐢 𝐤𝐮𝐛𝐰𝐚!

𝐙𝐮𝐜𝐡𝐮?...𝐳𝐮𝐜𝐡𝐮 𝐧𝐢 𝐂𝐡𝐮𝐦𝐚 𝐜𝐡𝐚 𝐋𝐢𝐠𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐡𝐚𝐨 𝐰𝐚𝐭𝐚𝐭𝐮. 𝐀𝐦𝐞𝐟𝐮𝐤𝐮𝐥𝐢𝐰𝐚 𝐡𝐮𝐤𝐨 𝐚𝐥𝐢𝐩𝐨𝐤𝐮𝐰𝐚, 𝐚𝐦𝐞𝐩𝐢𝐭𝐢𝐬𝐡𝐰𝐚 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐨𝐭𝐨 𝐧𝐚 𝐣𝐨𝐭𝐨 𝐤𝐮𝐛𝐰𝐚 𝐚𝐦𝐞𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐜𝐡𝐮𝐦𝐚 𝐛𝐨𝐫𝐚 𝐜𝐡𝐚 𝐩𝐮𝐚 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐜𝐡𝐨 𝐥𝐞𝐨 𝐬𝐨𝐤𝐨𝐧𝐢 𝐤𝐢𝐥𝐚 𝐦𝐭𝐞𝐣𝐚 𝐚𝐧𝐚𝐤𝐢𝐮𝐥𝐢𝐳𝐢𝐚!

𝐋𝐚𝐤𝐢𝐧𝐢 𝐮𝐡𝐚𝐥𝐢𝐬𝐢𝐚 𝐧𝐢 𝐤𝐰𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐡𝐚𝐰𝐞𝐳𝐢 𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐀𝐥𝐦𝐚𝐬𝐢 𝐰𝐚𝐥𝐚 𝐃𝐡𝐚𝐡𝐚𝐛𝐮!
Hapo sasa.
 
mkuu kumlinganisha Zuchu na Nandy hapo ndipo ulipo kosea kabisa kwa sababu hawa wote wanaimba miziki tofauti na wapo level tofauti.
Zuchu ni chipukizi na Nandy yuko level ya juu... tatizo mmeanza kusikiliza muziki 2016 basi mkiona mtu ametoa hit moja basi ni bora kuliko wengine.. Zuchu bado anayo safari kumfikia Nandy kwenye kila kitu..... na hata Nandy anayo safari kumfikia Lady jaydee kwenye kila kitu.
Lady jay dee? Huko mbali mnoo mbona, nandy bado sana kumkuta vee money.
 
Rubby ana tatizo la kibri na hafugiki na wala haambiliki kwa hiyo kum manage Ruby ni liability muda wowote biashara yenu inaweza kufa lakini kwangu mimi sijaona mwenye uwezo kama wake hapa tz
Ruby ni next level, sema ana matatizo yake tyuuh binafsi na kukosa promo.
 
Maua sana anajua sana Kishinda nandy, ila mzee wa kudaambuaa ni noumaa sana mda sio mrefu zuchu atawafunika wasaani wote wakike maana ni [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Unaota wewe eti eeeeh? Poleeeeh sanaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi waimbaji wangapi ni watunzi duniani na watunzi wangapi ni waimbaji ? Hapa huwa watu wanatoa credit zisizostahili kwa baadhi ya watu na kutowapa credit wanaostahili...,

Kwa ufupi kwa sasa mashairi mengi ni mabovu..... sio kwamba hawawezi kutunga mashairi bali wame-concentrate kwenye maneno ya ngono (which is unnessary) na hii ni kwa wengi wao....
Inategemea wanamwimbia nani, Muzik wao umelenga kundi gani zaidi.Na hilo kundi linapenda kusikia nini.Kumbuka hii Ni biashara. Kundi kubwa la muziki wa bongo fleva Ni vijana siyo hao babu na bibi.Hao babu na bibi wana miziki yao.

Dunia yenyewe inaenda kasi,hicho unachoita matusi kwa sasa ni vitu vya kawaida sana kwa kizazi hiki. Huwezi kuusikiliza mezani na watoto lkn watoto wenyewe ndio wanapenda na wao ndyo soko la huo muziki.

Wanaimba kile ambacho sokoni kinauzika.Penda unachopenda usitake kujua kuhusu mwenzako anapenda nn.Kila mtu ana exposure yake ktk maisha.🤣🤣
 
Ruby ni next level, sema ana matatizo yake tyuuh binafsi na kukosa promo.
Sahihi kabisa mkuu,sijaona bongo mwanamuziki anaweza kuimba laivu km rubi na sauti ni ile ile.Namkubali sana sema ndiyo hivyo.
 
Hivi Vanessa ndio ameacha muziki kabisa? Ana kipaji level za mbali
Aache muziki wapi? Hakuna [emoji445]bila vee, mbna ana flows tyuuh verse, hujasikia kashirikishwa na vanny boy, song inaitwa "Twerk" na kaua vibayaaaah.
Vee hajawahi niangusha yaan. Sijutiii kuwa fan wake.
 
Sahihi kabisa mkuu,sijaona bongo mwanamuziki anaweza kuimba laivu km rubi na sauti ni ile ile.Namkubali sana sema ndiyo hivyo.
Ruby bhana analiza wengi ukweli usemwe tyuuh, promo hapati.
 
Wasalaam wanajamvi.

Kama mnakumbuka ujio wa Nandy alianza baada ya Ruby kukorofishana na Clouds media. Watu wengi nikiwapo mimi walikuwa wana doubt sana kipaji cha Nandy toka awali.. na kama kipindi kile watu walikuwa wakimsikia Nandy basi utawasikia wakisema hamna kitu huyo ameletwa kumfunika Ruby lakini hana kipaji kabisa.

Lakini kwa Msanii Nandy ilikuwa tofauti kwani kila wakati ukipata kusikiliza wimbo wake unagundua kabisa hapa tunaye msanii wakike hodari kabisa.
Msanii Nandy ni bora sana kwenye vitu vingi ukilinganisha na wasanii wenzie wakike kwa sasa.
Ukisikiliza wimbo wa Nandy wa sasa utaona utofauti kabisa na wimbo wa juzi na jana na hiki ndicho kinawashinda wasanii wengi wa kike kwa sasa maana wengi wao karibu nyimbo zote zinafanana kabisa kila kitu.
Pia swala la utulivu kwenye stage linamfanya Nandy awe bora sana kuliko wasanii wenzie wa kike... wasanii wakike wanatatizo la uwezo wa kusikika wakiwa kwenye jukwaaa, wengi wao wanapiga kelele sana tena sana hadi unaweza kujiuliza kama ndio huyu unayemsikia kwenye radio au lah.

Ukimsikiliza Nandy unaona kabisa kipaji kikubwa sana ambacho kinajua kutumiwa vilivyo tofauti kabisa na wasanii wetu wa kike natamani sana kama Rubby angeliamka usingizini akapambana maana ni Rubby pekee ndio ana uwezo mkubwa lakini amelala na aambiliki na ndiye msanii anayefanya Nandy aendelee kutamba kwa Level yake.
Nandy nilimkuabali sana kwenye Halleluya x Willy Paul.

 
Back
Top Bottom