Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Ujinga wa kusema msanii anamiliki kila kitu upo Africa na bongo ni moja ya hizo nchi in fact kwa mataifa makubwa Kama US huwa Kuna mgao wa hatari kuanzia waandika mashahiri,Mwanamziki mwenyewe Hadi producer.
Wasanii bongo hawajui mziki ni biashara kubwa na uendeshaji wake ni wakibepari
Msanii kumiliki kila kitu hata kanye west akisikia atashangaa
 
Watu ubepari wanauchukulia poa 😀😀😀
Kwenye ubepari hakuna huruma mbele ya maslahi
Kundi la 112 usa lilipotaka kujitoa badboys wakajikuta hadi jina kumbe sio milki yao ndio mwanzo wa kupoteana hadi leo sasa kwa jinsi wanavyoonekana kwenye kideo na boss wao diddy wanabang mtu wa kawaida unaweza kudhani anaweza kuwafanyia hivyo kweli 😀😀😀 kawachinjia baharini bila huruma mpaka kesho hajageuka nyuma
 
Ujamaa ulitulemaza mkuu na umasikini poa ni shida Sana.
 
Statement ya akili Sana hiyo. Eti "sikujua kuwa sheria hairuhusu hii". Mahakama inakupiga nyundo tu.
Yani mahakama haijui hiko kitu inakupopoa as long as kipindi unasigne haukuwa chini ya 18 na hukuwa umelewa au chizi
 
Hili tatizo hata usa lipo yani Ashanti imebidi amimbe tena album yake nzima.
Lil Wayne pia ndio karusha tena video kwenye account yake ya YouTube upya maana haki ilikua kwa cash money.
Yani ukizubaa unapopolewa tena sana unabaki mtupu kazi ya utumwa
 
Hivi hawa wasanii wa WCB huwa wanakuwa managed na nani? Kwa sababu kama wanakuwa managed na hao hao kina Tale, Fela na Salaam then kuna tatizo la conflict of interest. Haiwezekani mtu anayemiliki au kuongoza lebo awe pia meneja wa msanii. Meneja anatakiwa asiwe part ya label ili aweze kulinda maslahi ya msanii. Hii itasaidia wasanii kutosaini mikataba ya ajabu ajabu. Angalizo: Nimewatumia WCB kama mfano tu. Hii inazihusu label zote.
 
Awe na mwanasheria tuu wa kusoma mikataba
 
Kiongozi I have very deep infos kuhusu hii game ya bongo music industry hii ni kwa dababu nimefanya kazi kwa karibu na hii industry for the good 2yrs. Kila wakati huwa natamani kuandika gazeti humu nielimishe watu huwa kila nikianza naishoa kati halafu naamua kufuta maana kinachofanyika kwenye industry ni UBAKAJI na kuviziana kwamba atakaemuwahi mwenzake basi ameshinda milele. Sometimes huwa naogopa maana taarifa nilizipata nikiwa nafanya kazi kwenye taasisi ya umma na kwa namna nilivyoji-expose humu ni rahisi sana kuwa traceable ila nitaleta gazeti juu ya game ya muziki na film inavyoendeshwa hapa mjini.
Kikubwa ni kuwa ELIMU ELIMU ELIMU na mbaya zaidi hawa wahusika wenyewe hawapo tayari kupata elimu hiyo na kibaya zaidi ni kuwa wenye hiyo elimu ni wachache maana hata wale wanaojinasibu sana kumbe hawafahamu sana kuhusu COPYRIGHT inavyofanya kazi yaani hadi baadhi ya mawakili.
Sasa kwa kuwa wengi (more than 90%) ya wasanii na managers wao hawana elimu ya kutosha juu ya haya mambo ndio mwisho wa siku wanaviziana na anaemuwahi mwenzie ndio anatoboa
 
Awe na mwanasheria tuu wa kusoma mikataba
Ukweli mchungu ni kuwa mbali na kuwa na mwanasheria wa kupitia mikataba
1. JE, HUYO MWANASHERIA ANA UELEWA MPANA WA INDUSTRY YA MUZIKI WA HAPA NCHINI NA DUNIANI KWA UJUMLA?
2. JE, HUYO MSANII NA MANAGEMENT YAKE WAPO TAYARI KUMLIPA WAKILI(Hata 5M tu) ILI WAPATE HIYO HUDUMA YA USHAURI WA KISHERIA?
 
Shida ni pale kwenye mikataba unapoamua kushuka signato. Maana hawakuwa na hela ya kununua beat so yeye anakuwa anajitolea bit zote wewe unaleta mashaairi. Ofcoz masta itabaki kwa p funk ni business ambayo hata USA wasanii yamewakuta haya ndio maana hata maiko Jackson aliwaambia vijana wahalikishe wanamili masta zao ili wasife njaa Maana hapo ndio kwenye hela. So nadhani hata rayvanny pia masta anazo diamond. So hata Sasa yanatokea muhimu wasanii walate elimu ya kutosha kuhusu mastaaaaa hizo. Pfunk alitumia mwanya Enzi hizo but now still Kuna wasanii hawamiliki mziki wao
 
P Funk anakula mpaka hela za marehemu Ngwea. Yeye p Funk anajinadi kama anapaza sauti juu ya haki za wasanii vipi mbona yeye anawanyonya mpaka leo?

Haki za ubunifu kwenye midundo mbona anawatapeli wenzie?

Tukemee unyonyaji wa P Funk
Kuna mtu anakula hela ya eazy e na Tupac mpk ss kwa mambo hayo hayo. Unajua mpk Leo Dr. Dree hamiliki the cronic
 
Wasanii wetu wengi hawajui sheria ya Intellectual Property..

Kimsingi hata maproducer wengi sana wananyonywa na wasanii.. fikiria msanii nyimbo baada ya kurekodi ikatoboa producer huwa anafaidika vipi?

Kimsingi wote wanatakiwa kufaidika.. kama hawakuingia mkataba wa kinyonyaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…