Music publishing ni ishu tata sana. Sio huku kwetu tu bali hata huko kwa walioendelea. Kuna mifano kadhaa ya wanamuziki wakubwa ambao walitangaza kufilisika (bankruptcy) licha ya "kuuza" mamilioni ya kopi za rekodi. Mfano Toni Braxton, TLC n.k. Lakini huo ni mjadala wa siku nyingine.
Typical music production (unless kila kitu mpaka kuimba amefanya mtu mmoja) huwa inahusisha producers, composers, melody makers, session musicians na engineers. Hawa huwa wanakuwa na haki zinazoitwa mechanical rights za huo wimbo. Ukiangalia hapo sijamtaja mtu mmoja, MUIMBAJI/WAIMBAJI. Hawa wanakuwa na haki za uimbaji (singing right) kwenye huo wimbo.
Tafsiri ya rights zilizotajwa hapo juu ni kwamba kwa namna fulani KILA mtu aliyeshiriki kutengeneza huo wimbo (unless kwa sababu fulani amekubali kufanya bure) anatakiwa kulipwa. Analipwaje ndio mjadala ninaouona kwenye huu uzi. Suala la mshiriki kwenye production atalipwaje huwa liko kimkataba, inaweza kuwa malipo ya mara moja au percentage fulani ya publishing (wenzetu wanaitaga points). Kuna watu wamesema kwamba P Funk amepora haki ya watu aliofanya nao kazi ya production. Tutajuaje kama P alishamalizana nao kimalipo na wakaachia rights zao za publishing? Je, hizo haki zao zimesajiliwa kisheria? Hii ishu nitaijadili kidogo huko mbele.
Again, typical music production huwa inasimamiwa Producer. Kwenye music production kumekuwa na tatizo la watu kuchanganya producer na beat maker au session musician. Kwa kawaida huwa inategemewa producer awe pia musician ili awe na uwezo wa kuendesha zoezi zima la production. Lakini SIO lazima yeye apige vyombo au kufanya programming kwenye huo wimbo unaotengenezwa. Kuna mtu kasema "P Funk hajui hata kupiga kinanda", kwanza sio kweli, P Funk anaweza kupiga kinanda, pili ili awe ame-produce wimbo fulani sio lazima personally afanye beat making, yeye anahakikisha kila mhusika ana-play role yake na standard ya production inakuwa per exellent. Producers wengi wakubwa huko duniani huwa hawapigi vyombo wao wenyewe bali hutumia session musician au beat makers mfano Quincy Jones, Dr Dre, P Diddy, Irv Gotti etc.
Sasa tuje kwenye ishu tata ya hatimiliki aka publishing. Tofauti na watu wengi wanavyoamini, publishing rights sio automatic. Ni lazima ziwe zimesajiliwa kisheria (registered) ili zilindwe, kama umefanya kazi yoyote ya ubunifu bila kuisajili wakatokea wajanja wakasajili imekula kwako. Jamaa watapiga hela huku wewe ukipiga miayo. Huku kwetu nina uhakika kuanzia wasanii, wapiga vyombo na wengineo walikuwa hawalijui hilo ndio maana watu wengi wakiwemo wasanii wanaamini kwamba akienda studio akalipia kurekodi wimbo automatically unakuwa mali yake. Kitu ambacho sio kweli.
Sijajua mikataba ambayo wasanii wa hapa kwetu (wakiwemo wa WCB) huwa wanaingia na lebo huwa ina-address suala la publishing au hapana. Ambacho nina uhakika nacho ni kwamba wasanii wengi (hasa wa zamani) hawako aware kuhusu ishu ya publishing, na ndio mzozo wa Prof Jay na P Funk ulipoanzia.
Actually ishu ya Prof Jay na P Funk kuhusu beat ya nikusaidiaje haikuanzia kwenye beat hiyo kutumika kwenye movie. Baada ya Prof Jay kurekodi wimbo huo na kuhit, Chameleone akamfuata P akitaka atumie hiyo beat, P akamchaji Chameleone USD 2,000. Prof aliposikia akaja juu na kulalamika kwamba beat yake imeuzwa bila idhini yake. Lakini kiukweli Prof hakuwa ma haki yoyote kwa kuwa Chameleone alitumia beat tu, sio wimbo wote. Wimbo wa Chameleone ukaja kutumika kwenye movie ya Queen of Kitwe iliyotengenezwa na Disney na Chameleone akavuta mpunga. P akakomaa na Disney na kwa kuwa sheria ilikuwa upande wake alalipwa. Again Prof hakuwa na haki kwani wimbo uliotumika ni wa Chameleone na sio wa kwake.
Hitimisho ni kwamba music business is very shady, inatakiwa msanii ajifunze SANA sheria za hatimiliki na ahakikishe haki zake ziko documented na zimesajiliwa kisheria ili zilindwe.