Hivyo ndivyo P. Funk anavyosema na kuuaminisha umma. Anasema kuw msanii hanunui beat ya produsa bali analipia muda wa studio, beat inakuwa mali ya produsa.
Sasa ili uitwe wimbo, maana yake kuna vocals na beat, kwa pamoja ndio vinafanya uitwe wimbo. Kuna msikikizaji atapenda mdundo na kununua huo wimbo, kuna mwingine atapenda maneno na kununua huo wimbo, ni ngumu kujua mtu anaponunua wimbo anakuwa amevutiwa na mdundo au vocals (maneno) au vyote. Ndio maana mgao huenda kwa wahusika wote wa wimbo, waandishi, waandaaji, waimbaji nk
Hii ishu ya Nikusaidiaje, Jay ndie aliyepambana na Chameleone, tafsiri ni kwamba, P Funk alikuwa ameuza beat yake na akaona ni sawa kwa Jay kulalamika, baadae akamzunguka Jay na kuchukua mpunga kwa wamarekani, ndipo hapo mtafaruku ulipoibuka