Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Nafikiri waliingia mgogoro na Prof. Jay baada ya P. Funk kuchukua hela kwa kampuni ya movie iliyotumia beat ya bombo clat ambapo original ni beat ya nikusaidiaje. Profesa alilalamika kuwa hakupewa hata senti
Nakumbuka sio movie, ni ngoma sijui nikusaidiaje ile biti akauziwa tena chameleone akaimbuia bomboclat.. Jay kuulizia p kaishakula hela, chameleone akataka kumpa tena hela Prof akaamua wapige kolabo, ngoma nimeisahau jina.
 
Music production ina mambo mengi Sana aisee. Beats siku zote ni ubunifu wa producer. Kwa hiyo hakuna tatizo akila faidA ya ubunifu wake.
Kwenye production na ubunifu kuna hakishiliki... walioshiriki kutengeneza beats mgao wao mbona hawapewi? Nyimbo nyingi pale yeye alikuwa anafanya mastering tu na mixing ila ubunifu wanafanya kina bizimani lakini anatepeli jasho lao. Huo ni unyonyaji na uzuri yeye amejipambanua kama mtetezi wa haki za wabunifu.
 
Bizman na wengine waliokuwa wanasaidia Majani kwenye production, lini uliwahi wasikia wakilalamika!? Je, wakati kazi zinasajiliwa kwenye mamlaka husika hao waliorodheshwa katika production? Ila usisahau hizo ni kazi za Bongo Records. Kama Kuna makubaliano baina ya P Funk na Producers washiriki hayo yanakuwa ni makubaliano yao binafsi.
 
Kwenye creative industry hakuna kitu kinaitwa kuorodheshwa au kutoorodheshwa au ulipwe baada ya kulalamika. Kama mtu ni mwandishi wa nyimbo basi analipwa kama mwandishi kama ni producer atalipwa kama producer kuna co producers wengi pale bongo records yeye anawaficha anaenda kupiga kelele kuhusu producers wa studio zingine huyu mtu ni mbaya sana.

Wengine wakifanya makubaliano binafsi mbona tunapiga kelele why not kwa p funk pale na unyonyaji wake?
 
Hii 40% gharama yake ni nn ili uipate? Mavazi, chakula, malazi, usafiri n.k vinaingia humu?
 
Nakumbuka sio movie, ni ngoma sijui nikusaidiaje ile biti akauziwa tena chameleone akaimbuia bomboclat.. Jay kuulizia p kaishakula hela, chameleone akataka kumpa tena hela Prof akaamua wapige kolabo, ngoma nimeisahau jina.
Ni movie.

Profesa J alitoa wimbo wa nikusaidiaje, Chameleone akatamani beat akalichukua na kufanya wimbo wake wa bombo clat. Profesa akawa na mgogoro na Chameleone, wakayasolve kwa kufanya wimbo wa Ndivyo Sivyo, wakamalizana kisanii.

Kina Lupita Nyongo wakatengeneza filamu yao na katika soundtracks zilizotumika wakatumia wimbo wa Bombo Clat wa Chameleone Jose, wakamlipa bwana Chameleone. P Funk kujua akamfuata Chameleone amtoe mpunga, Chameleone akampa jamaa USD 4,000 kumbe yeye (Chameleone) amelipwa USD 50,000. P Funk akawafuata Kampuni husika ya movie na kutaka kuwashtaki na hapo wenye kampuni wakampa USD 100,000 kama sikosei na hapo ndio Profesa J akajua kuwa jamaa amekula hela na yeye J hajapata kitu, ingawa alilipia beat husika, hivyo kustahili mapato yatokanayo na beat. Na ndiyo sababu kwa Chameleone mlalamikaji alikuwa ni Jay na sio P Funk
 
Hivi mkuu naomba unieleweshe, ina maana ukitoka WCB hata ukiwalipa bado nyimbo zinabaki kuwa za kwao?
Kila kona kuna unyonyaji ila mimi kinachonichekesha ni mashabiki wa WCB kutetea yale wanayofanya wcb wakati hao hao walikuwa wanaponda clouds kwa mambo hayo hayo.

Huwezi kupatana vizuri ukiwa na njaa na hawa wasanii uwa wakiwa hawajatoka wana sign mikataba wakiwa wanawaza kuwa na majina na kumiliki magari, wakishapata hivyo na kugundua pesa wanayotengeneza na wanachoambulia ni mbingu na mafuta, basi hapo ndipo wanachanganyikiwa.

Kuhusu kupata pesa ni kweli walipata sana sema walikuwa wanaishi lifestyle flani la movie na usela mavi
 
Nitakuja na uzi siku moja niwaeleweshe kuhusu mikataba ya muziki. Biashara ya muziki ni kama biashara ya miti record lebo sio charity group.
Toa hiyo elimu isije ikawa mwenye lebo anapata ndogo ila haionekani sababu watu wanatazama turnover badala ya profit.

Mm nina biashara, mishahara kwa mwaka inaweza kuwa m100 kwa wafanyakazi approx 6, ila faida iliyobaki kabla ya kodi ikawa 20m. Ukipiga hapo wafanyakazi walipata kubwa kuliko mmiliki ila hilo haliwezi kuonekana.
 
Nimekusoma vyema mzee
 
Aina shida nitaleta uzi.

Watu hawaangalii kilichowekwa wanatazama kinachopatikana.
 
Yeye profesa J why hakwenda kudai haki yake mapema?? Au hajui kama beat ni haki yake maana alilipia kufanya ngoma??
 
Hii biashara imekaa kihuni sana... Hivi LAIZER akitengeneza beat la wimbo inakua mali yake au ya diamond?? je beat ikitumika kufanya kazi nyingine huko nje mpunga ukatolewa analipwa nani hizo hela??? MSANII AU DIAMOND AU LAIZER??
 
Mwenye haki kwenye beat hiyo ni P Funk na ndio maana ni yeye alieshikia bango mpaka mkwanja ukatoka. Na mamlaka zote za hakimiliki za Uganda na Tanzania (COSOTA) zilimsaidia mpaka akapata haki yake na Wala sio Prof. Jay. CoSoTa isingeweza kumnyima Prof. Jay Kama angekuwa na haki kwenye hili.
 
Hii biashara imekaa kihuni sana... Hivi LAIZER akitengeneza beat la wimbo inakua mali yake au ya diamond?? je beat ikitumika kufanya kazi nyingine huko nje mpunga ukatolewa analipwa nani hizo hela??? MSANII AU DIAMOND AU LAIZER??
Haya ni maswali mazuri mno ila majibu yake ni ngumu unless kama mikataba tungekuwa nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…