Ukweli usiopingika: Katika marais waliotumikia taifa letu ni hayati JPM pekee aliyefanya makubwa kwa muda mfupi kuliko marais wote waliotutawala

Ukweli usiopingika: Katika marais waliotumikia taifa letu ni hayati JPM pekee aliyefanya makubwa kwa muda mfupi kuliko marais wote waliotutawala

Wasukuma kubalini kuwa mungu wenu ameshatangulia mbele ya haki ya Mungu Mkuu.... Mbele ya Mungu mkuu, wengine wanamwita Elshadai, wengine Allah, wengine Maulana,

Yule alikuwa binadamu kama sisi wengine.... alikuwa na mapungufu yake mengi na mazuri yake mengi pia.

Mwacheni mungu wenu apumzike kwa amani basi... Dah!

Siku ya hukumu Mungu mkuu ndio ataamua....
mimi sio msukuma ila jamaa ksongea ukweli
 
Hata ungekuwa wewe ungeruhusu watu wakukashifu mbele ya raia wako unaowaongoza?

Nenda katazame video za tundulisu namna alaivyokuwa anatoa kauli za madharau na kebehi kwa mkuu wa nchi.
Tatizo la kuishi nchi za kimaskini na zisizo na demokrasi, mkuu wa nchi sio mungu na kumkosoa au kumtukana sio kosa, acha watu waongee sio kuwaua kwa sababu hupendezwi na walichosema
 
Pamoja na hayati Julius kutawala kwa miaka 23 huwezi kulinganisha makubwa aliyofanya na yeye na hayati Magufuli. Hayati Julius aliacha nchi imechakaa kwa kila namna, miundo mbinu hovyo, ajira hovyo na hata taifa halikuwa na pesa kabisa.

Huyu Mwinyi ndio alizingua maana hakuna alichofanya cha maana zaidi ya kusaidia watu wasivae masempele.

Mzee Mkapa(RIP) alijitahidi lakini naye hakutufanyia makubwa sana.

Jakaya ndio alituharibia nchi kabisa. Ufisadi ukawa ni heshima kwa watumishi wa umma.

Hayati Magufuli kwa miaka mitano tu alijenga miundo mbinu, shule mahospitali na zahanati kuliko marais waliomtangulia.

Hospital ya rufaa mkoa Mara ilianza kujengwa wakati hayati Nyerere mwaka 1972 lakini ni hayati JPM alihakikisha inakamilika akiwa madarakani.
Uko sawa kweli wewe?
 
Wasukuma kubalini kuwa mungu wenu ameshatangulia mbele ya haki ya Mungu Mkuu.... Mbele ya Mungu mkuu, wengine wanamwita Elshadai, wengine Allah, wengine Maulana,

Yule alikuwa binadamu kama sisi wengine.... alikuwa na mapungufu yake mengi na mazuri yake mengi pia.

Mwacheni mungu wenu apumzike kwa amani basi... Dah!

Siku ya hukumu Mungu mkuu ndio ataamua....
Wasukuma hawataki kabisa kuamini kama mungu wao kafa
 
Wasukuma kubalini kuwa mungu wenu ameshatangulia mbele ya haki ya Mungu Mkuu.... Mbele ya Mungu mkuu, wengine wanamwita Elshadai, wengine Allah, wengine Maulana, ...
Hilo suala la kabila linaingiaje hapo wewe kibwengo?
 
Ila kiukweli Mimi Nilikua simkubali Kwa SABABU ya chama chake tu ila Magufuli ni alikua Rais Bora sana Afrika nzima.

Alijenga miundo mbinu mingi Kwa muda mfupi na kudhibiti Rushwa na Matumizi mabaya ya Serikali.

Kosa Kubwa la JPM lilikua kutuletea Wabunge na madiwani wasiofaa kabisa. Na Tauzi za wakuu Wa Wilaya na Wakurugenzi wasiofaa.

Lakini nafikiri ilikua ni mbinu yake ya kuwapata watu anaoweza kuwakimbiza mchakamchaka kuleta Maendeleo.

Trabu na trati.
Nadhani Ndani ya CCM ndiye Kada Pekee anayeweza kuja kuwa kama Lowasa na Maamuzi kama JPM.
Tusubiri. Ukoo Wa panya KAZI yake ni kula Nafaka stoo.
 
Back
Top Bottom