Pamoja na hayati Julius kutawala kwa miaka 23 huwezi kulinganisha makubwa aliyofanya na yeye na hayati Magufuli. Hayati Julius aliacha nchi imechakaa kwa kila namna, miundo mbinu hovyo, ajira hovyo na hata taifa halikuwa na pesa kabisa.
Huyu Mwinyi ndio alizingua maana hakuna alichofanya cha maana zaidi ya kusaidia watu wasivae masempele.
Mzee Mkapa(RIP) alijitahidi lakini naye hakutufanyia makubwa sana.
Jakaya ndio alituharibia nchi kabisa. Ufisadi ukawa ni heshima kwa watumishi wa umma.
Hayati Magufuli kwa miaka mitano tu alijenga miundo mbinu, shule mahospitali na zahanati kuliko marais waliomtangulia.
Hospital ya rufaa mkoa Mara ilianza kujengwa wakati hayati Nyerere mwaka 1972 lakini ni hayati JPM alihakikisha inakamilika akiwa madarakani.