Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Tutakuwa na vitabu vingi vingi mfano kusini karibia makabila yote wanafanana mf, ngoni kwa ruvuma kitabu kimoja kaskazini ni wasukuma na pacha wao kitabu kimoja, hivi kidogokidogo hadi tunatengeneza kitabu chetu kimoja mithili ya bible na qur'an
 
Naomba unipe uongo wa kwenye Qur'aan hata mmoja tu.
Mkuu Zurri naomba usitoke kwenye mada husika, mada ipo wazi kabisa yaani tuangazie ukweli usiosemwa kuhusu dini za Afrika! Hapa hatushindanishi vitabu vya kidini ila tunataka tuthibitishe ukweli uliopewa kisogo juu ya dini za Afrika. Pia hatupo kumlazimisha mtu akubaliane na sisi juu ya uzuri wa dini za Afrika ila tunashawishi kwa hoja ili Waafrika waamue wenyewe na pia tunaheshimu mawazo ya wakuu wote.
 

Hii pia iko ndani ya mada sababu huwezi kusema Qur'aan bila kuzungumzia dini. Kadhalika hatuwezi kufumbia macho uovu.
 
Africa tumewahi kuwa na Sayansi gani yenye tija?
 
Hii pia iko ndani ya mada sababu huwezi kusema Qur'aan bila kuzungumzia dini. Kadhalika hatuwezi kufumbia macho uovu.
Sawa mkuu
Ninachomaanisha hapa ni kuruhusu watu wawe na mawazo huru, sipo kudharau dini ya mtu naheshimu dini zao kwani ni sahihi kwa mazingira yao. Ninachotetea ni dhana ya kuwa na utambulisho rasmi wa dini za kiafrika. Ili ikifika siku na waafrika tuape kwa namna yetu si kwa kutumia vitabu vya kigeni na miungu ya kigeni.
 
Bado hatujachelewa tunaweza kuanzisha dini yetu , Kwanza hawa wanaojiita manabii wanapotosha sana watu kwa kutumia dini za kizungu.Wanatuchanganya sana, majina yenyewe wametupa ya kizungu .Kizazi cha baadae kitatushangaa sana!!! Nafikiria tu kipindi mvua zilipogoma watu huwa wanaenda kuomba mvua kwenye sehemu ya miti mikubwa au milima na mvua zinanyesha . Tuwe na dini yetu, ukombozi wa kweli wa fikra kwa Waafrika.
 
Tukisema Elimu tunaweza rudi kwenye njia ile ile ya KIMFUMO ambao uasisi wake ni kutoka kwa hao hao Wazungu, LABDA TUSEME TATIZO LIPO KWENYE UFAHAMU UNAOPELEKEA KUJUA (na hasa kuujua UKWELI WENYEWE KUTUHUSU KWA KUHADITHIWA NA MKWELI HALISI NA HATA KIMAANDIKO).
 
Mkuu umechanganya vitu vingi sana kwanza sayansi sio ya wazungu ni ya watu wote, pili tamaduni zimeenda zikibadiri hatuna haja ya kurudi nyuma tena kwa ajiri ya kuonyesha ubora wetu hata wazungu walikuwa na imani zao kabla ya ukristo hata wao walitupilia mbali. Tatu ligha zina kawaida ya kuzaliwa na kufa kuna lugha ya kiyunani haiongelewi popote kuna lugha nyingi kongwe za kale zilikufa usizionee huruma lugha kuwa inferior.
 
Mkuu Frustration hata mzungu alikuwa na dini yake ya asili lakini alipopelekewa ukristo aliupokea na akazipiga chini dini zake za asili za kipuuzi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…