Afrika ina dini ambazo ni nyingi sana kuliko bara lolote lile Duniani. Dini hizi nyingi zimepigwa ban na watu wa nje(whites) kwa sababu tu ya inferior ya mtu mweusi wa zamani. Kuishi kwa kumtegemea mzungu kwa kila kitu hadi ikapelekea hadi sasa watu wanategemea pia dini za kizungu.
Hakuna kabila hata moja Afrika ambalo limepoteza imani ya dini yao, ndio maana hata waendao makanisani hutembelea kwa mababu zao kupata kinga. Dini zote Afrika zilikuwa hazihusiani na uchawi ila mtu mweupe ndiye aliempa mtu mweusi uchawi kwa mafunzo maalumu akimdanganya ya kiimani.
Uchawi Afrika uliletwa na mzungu na ukweli huu haupingiki. ukiachana na hayo lakini pia upande wa maadili hapa nianze kwa salamu
U hai? ndugu hata kama haupo hai ila ukweli ukifikie huko huko ulipo. Nani aliyekuambia kuwa Afrika watu walikuwa wanavaa nguo full mwili mzima? Angalia wamasai japo na hao pia wamejaribu kubadilika. Ila hali ilikuwa mbaya sana zamani.
Watu walikuwa wanazuii tupu tu, Vikande vyote vya nyuma vilikuwa wazi na hakukuwa wa kushangaa katika hili kwa sababu ndiko tulikotoka. Ujio wa white man ukatibua hali ya hewa wakabadili,mtindo wa mavazi,dini, elimu, lugha, biashara na kila kitu.
Sasa katika mambo waliobadili pamoja na nidhamu na kusema nchi za Afrika hawajastarabika kwa sababu wanatembea uchi, wanaabudu madudu, wanaongea lugha chafu n.k. Watu wa Afrika walilazimishwa kukopi mila na mitindo yote ya Kizungu.
Unaposema vijana wetu hawana maadili ni kutukana wazee wetu wa zamani ambao walikuwa wanawinda,na kupiga ngoma uchi.
Hawa wapuuzi wa kizungu ndio walioita matabibu wetu kwa jina baya eti Matabibu wa kichawi(witch doctor) na wao kujiita Doctors, physician mara sijui wakemia n.k. Wakasema kupiga ngoma ni ushamba ila tupige miziki ya kisasa n.k.
Sioni jema la wazungu katika imani, wala tamaduni na wala technology kwa sababu naamini tungepigana na hali zetu. Wale wanaoenzi mababu zetu siku hizi wanajiita TIBA MBADALA sijui ndio nini. Wajiite wauguzi na wataalamu wa tiba na magonjwa mbalimbali.
Afrika without White's countries is possible, hatujachelewa sana tuanze ku uphold vya kwetu ili vitusaidie na sisi kwa masilai yetu. Hivi vya kuletewa havitufai kwani "NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI MA**KO" na ndio mana mambo hayaendi kama ilivyotakiwa.
Nawachukia wa Asia na dini zao i.e Christian and Muslims. Ww ndugu yangu mtoto na mjuu wa Likangamai hayo mambo utayaweza? Ndio maana kulikuwa na mabala na aina ya watu na mila tofautitofauti, sasa ya nje ya nn na kuona kama vile ulichelewa kuvipata?
Kwani wao walikuwa hawajui kama Afrika kuna watu? mbona wamefika baada ya manyanyaso mauaji na dhulma kwa ndg zetu? Nini za Asia ni dini za ukweli kwa Asia na dini za Afrika ni za kweli kwa Afrika tu?
Jambo gani jema limewahi semwa na hao watu juu ya mababu zetu? wamewatukana sana kupitia imani zao na leo wamefanikisha kutufanya ndg,jamani tunaenda wapi na ilihali tunakotoka tunakudharau?
NAIPENDA AFRIKA SANA NA HATA NIKIWA JIRANI NA MZUNGU WOTE WE FEEL DIFFERENCES ON EACH AND EVERYTHING.RELIGION, LANGUAGE, STYLES,CUSTOMS, COLOUR, AWARENESS, ASSERTIVENESS STATUS, RECOGNITION e.t.c.
Ukweli haupingiki hata mniue hadi nife
Frustration kama lote!!!
Mimi ninavyo jua chanzo cha binadamu ni kimoja yaani Mungu, chanzo cha uchawi wanasema ni Babel pale walipojenga mnara. Na kipindi hicho huu mgawanyo kuwa hapa ni Afrika ,kule ni ulaya havakuwepo. Uchawi kote upo ,hata kwa wazungu, hata kwa watu weusi. Kwa mtu aliyekulia kwenye hizi jamii hayo mambo yapo, ya uchawi na usifikiri uwepo wa uchawi unaondoa uwepo wa Mungu. Mungu hata kwenye jamii zetu wana lugha ambazo zinaonyesha walijua uwepo wake.
Mfano kwa wakurya Mungu anaitwa Enokwe, wajaluo wanaita Nyasae, wasukuma wanaita Sebha.....
Hata kwa waisrael uchawi ulikuweo na wapiga ramli walikuwepo.
Soma kisa hiki hapa utaona:
1Samwel28:1 Siku zile Wafilisti wakakusanya majeshi yao ili kupigana vita dhidi ya Israeli. Akishi akamwambia Daudi, “Lazima ujue kuwa wewe pamoja na watu wako mtafuatana nami kwenda vitani.”
2 Daudi akasema, “Ndipo wewe mwenyewe utakapojionea jambo ambalo mtumishi wako anaweza kufanya.”
Akishi akamjibu Daudi, “Vyema sana, mimi nitakufanya uwe mlinzi wangu daima.”
3 Wakati huo Samweli alikuwa amekufa, nao Israeli wote walikuwa wamemwombolezea na kumzika kwenye mji wake mwenyewe huko Rama. Sauli alikuwa amewafukuza waaguzi na wachawi.
4 Wafilisti wakakusanyika na kupiga kambi yao huko Shunemu, naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote na kupiga kambi yao huko Gilboa. 5Sauli alipoona jeshi la Wafilisti, akaogopa; moyo wake ukajawa na hofu kuu. 6Ndipo Sauli akauliza ushauri kwa Bwana, lakini Bwana hakumjibu kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa njia ya manabii. 7Basi Sauli akawaambia watumishi wake, “Nitafutieni mwanamke mwaguzi ili nimwendee, nipate kuuliza kwake.”
Watumishi wake wakamwambia, “Yuko mwanamke mmoja huko Endori.”
8 Hivyo Sauli akajigeuza kwa kuvaa mavazi mengine, naye usiku akiwa amefuatana na watu wawili wakaenda kwa huyo mwanamke. Akamwambia, “Nibashirie kwa uaguzi, unipandishie yule nitakayekutajia.”
9 Huyo mwanamke akamwambia, “Wewe unajua lile alilofanya Mfalme Sauli. Amewakatilia mbali waaguzi, wapiga ramli wote na wachawi katika nchi. Mbona umenitegea maisha yangu ili wapate kuniua?”
10Sauli akamwapia huyo mwanamke kwa Jina la Bwana, akasema, “Kwa hakika kama Bwana aishivyo, hutaadhibiwa kwa ajili ya jambo hili.”
11Ndipo yule mwanamke akauliza, “Je unataka nikupandishie nani?”
Sauli akasema, “Nipandishie Samweli.”
12 Yule mwanamke alipomwona Samweli, alipiga yowe kwa sauti kuu, naye akamuuliza Sauli, “Mbona umenidanganya? Wewe ndiwe Sauli.”
13 Mfalme akamwambia, “Usiogope. Unaona nini?”
Yule mwanamke akasema, “Naona mungu unapanda kutoka ardhini.”
14 Sauli akamuuliza, “Ni mfano wa nini?”
Yule mwanamke akasema, “Ni mwanaume mzee amevaa joho anayepanda.”
Ndipo Sauli akatambua kwamba ni Samweli. Sauli akasujudu kifudifudi, uso wake hadi ardhini.
15 Samweli akamuuliza Sauli, “Kwa nini unanitaabisha kwa kunipandisha juu?”
Sauli akasema, “Mimi ninasumbuka sana, kwa maana Wafilisti wanapigana vita dhidi yangu, naye Mungu ameniacha. Hanijibu tena wala kwa njia ya manabii wala kwa ndoto. Kwa hiyo nimekuita wewe ili unijulishe la kufanya.”
16Samweli akamuuliza, “Kwa nini uniulize mimi, maadamu Bwana amekuacha na kuwa adui yako? 17Bwana ametenda lile alilotangulia kusema kupitia kwangu. Bwana ameurarua ufalme kutoka mikononi mwako, naye amempa mmoja wa jirani zako, yaani Daudi. 18Kwa sababu wewe hukumtii Bwana, wala hukumtimizia ghadhabu yake kali juu ya Waamaleki, Bwanaamekutendea mambo haya leo. 19Zaidi ya hayo, Bwanaatawatia Israeli pamoja na wewe mikononi mwa Wafilisti, na kesho wewe na wanao mtakuwa pamoja nami. Bwana pia atalitia jeshi la Israeli mikononi mwa Wafilisti.”
20 Papo hapo Sauli akaanguka chini, akajinyoosha, akiwa amejawa na hofu kwa ajili ya maneno ya Samweli. Nguvu zake zikamwishia kwa maana alikuwa hajala chochote mchana ule wote na usiku.
21 Yule mwanamke alipomwendea Sauli na kumwona amepatwa na hofu, akamwambia, “Tazama, mimi mtumishi wako mwanamke nimekutii. Nimeweka maisha yangu hatarini kwa kufanya kile ulichoniagiza nifanye. 22Sasa tafadhali isikilize sauti ya mtumishi wako, uniruhusu nikupatie chakula kidogo ule ili uwe na nguvu za kurejea ulikotoka.”
23 Akakataa, akisema, “Mimi sitaki kula.”
Lakini watumishi wake wakaungana na yule mwanamke wakamsihi ale, naye akakubali. Basi akainuka hapo chini, akaketi juu ya kitanda.
24 Yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona hapo nyumbani, akamchinja mara moja. Akachukua unga, akaukanda, akatengeneza mkate usio chachu. 25Ndipo akamwandalia meza Sauli pamoja na watu wake, nao wakala. Usiku ule ule wakainuka na kwenda zao.
Katika hali kama hii ni Muhimu kuchagua Mungu wa kweli na kumtumikia