Ukweli usiowekwa wazi: Hayati Nyerere aliacha taifa letu likiwa masikini sana kiuchumi pamoja na kutoa msaada kwa nchi za jirani

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Alisaidia na kukomaa mataifa ya jirani yapate uhuru akasahau kabisa kuendeleza taifa letu.

Kauli mbiu ya kuwa sisi kuwa huru huku majirani zetu hawako huru sio vyema ilifanya akasau kuendeleza taifa letu.

Aliacha miundo mbinu iko hovyo, shule chache, hospitali chache na kila kitu kikiwa hovyo.
 
Ni kweli ana pia mazuri yake aliacha Dini yake ya RC imejipanga kutawala na kua sehemu kuu ya utawala wa nchi hi. Alijitahidi kuwapendelea kwa kuwapa vyeo serikalini jambo ambao paka leo watu wanataka kuliendeleza hilo jambo la kupokezana uraisi kati ya Dini mbili ni upuuzi sio democracy.
 
Tabia mbaya kuwalaumu marehemu..
Viongozi waliopo waache tu wizi na ufisadi, waache visingizio.
Tanzania ni nchi tajiri sana.
Hatupaswi kuwa hivi tulivyo.
Tunapaswa kuongoza Afrika kwa utajiri na nguvu za kisiasa.
Na hili linatakiwa liwe ndani ya miaka 10 tu ijayo.
 
Nashauri Nyerere day ifutwe...
 
Wewe endelea kunywa kangara.
Isingekuwa Nyerere ungekuwa unaendelea kula mapuya kijijini maisha yako yote.
 
Umasikini ni kafara la Uhuru na Sio yeye chanzo.
Ili wazungu waondoke ni lazima mtakuwa masikini wazee wapumbavu wakasaini,hizi ni Siri huwezi ambiwa popote.
Thus hatuwezi endelea itakuwa hivyo hivyo mara umeme,mara dollar sijui mafuta unadhani hivi vitu vinajitokeza tu
 
Kwa Kila Mwenye Ubongo Unaofanya Kazi Akiweka Mahaba Na Pembeni Hisia Pembeni, Huyo Mzee Lazima Achanwe Mwa Maamuzi Yake Ya Hovyo Yanayoligharimu Taifa Hili Mpaka Hii Leo,
Alikuwa na Nia nzuri matokeo yakawa tofaut.
Ni sawa na mtu anakopa pesa bank awekeze project then project isiendelee ikafa Sio kosa lake.
 
Kwenye hilo alikwaza taifa na waliompinga aliwaona sio watu Leo yuko wapi we gain nothing from it
 
Kosa la mwalimu ni kuchukia hata mazuri ya wakoloni
 
We ni ng'onda kabisa.
Hamkutaka kusoma elimu dunia mkaishia kukariri viarabu huko kwenye ajira mngeenda kufanya nini
 
Waliofuata Baada ya Nyerere wamefanya nini Taifa liwe Tajiri?
 
Kwa Kila Mwenye Ubongo Unaofanya Kazi Akiweka Mahaba Na Pembeni Hisia Pembeni, Huyo Mzee Lazima Achanwe Mwa Maamuzi Yake Ya Hovyo Yanayoligharimu Taifa Hili Mpaka Hii Leo,
Imagine nyerere angekuwa kama viongozi tulionao sasa kisha ujibu mwenyewe ... Mnaomtukana nyerere ni vijana mliozaliwa miaka 1990.
Nyerere aliacha shirika la ATCL linafanya safari ndani na nje ya nchi. Aliacha TRC na Tazara zikifanya kazi ya usafirisha wa abiria na mizigo kwa kiwango.
Nyerere aliacha nchi ikiwa na viwanda vya kutosha vilivyokuwa vinatoa ajira Textile industries, Tyres Industry, Automobile Industry, cement industries, electronic industries (kiwanda cha redio), viwanda vya kusindika na kuchakata mazao zikiwa katika mfumo wa Cotton Ginnery na National Milling karibu kila wilaya vilikuwepo. Viwanda vya viatu (Bora shoes).
Aliweka mkakati ya kujenga bwawa la kuzalisha umeme kwenye stiggler gorges miaka hiyo.
Aliacha mfumo wa elimu wenye focus ya kuzalisha wabunifu elimu ya leo ni knowledge based.
Aliacha Tsh ikiwa na nguvu.
Hakuwahi kuingia mikataba yenye harufu ya kuuza rasilimali za nchi.
Yako mengi sana.
Iwapo tungefanya jitihada ya kuyaandeleza nchi yetu ingekuwa ni miongoni mwa nchi tatu zenye uchumi imara Afrika.

Aliyoacha nyerere kama tungekuwa positive
 
Nchi hii ni tajiri sana toka kuumbwa kwake,na Nyerere kaicha ikiwa na utajiri mkubwa sana.

Tatizo tulilonalo sisi watanzania ni namna ya kupata watu makini wa kutuvusha katika angle ya uvunaji wa maliasili zetu,tumetawaliwa na ubanafsi,roho mbaya,uchawi,uroho,tamaa na kila aina ya ushetani,hili ndio tatizo la nchi hii
 
Nyerere alifanya kwa sehemu yake, sema baada ya yeye yalifuata majangili tupu ndiyo yametufikisha hapa
 

Na Tatizo Hilo Kalileta Nyerere Mwenyewe Kupitia katiba
 
Waliofuata Baada ya Nyerere wamefanya nini Taifa liwe Tajiri?
Wamekuta jengo lisilo na msingi imara, haliendelezeki.
Walipotaka kulivunja na kuanza upya alikua mkali kama mbigo as if hii nchi ilikua milki yake.
Baada kuondoka duniani imekua too late kuanza upya.
Wanalazimika kufanya yote kwa pamoja ambapo ufanisi unakuwa moja toa moja.
 
Upo nje ya mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…