Ukweli wa Kustaajabisha Kuhusu Nyota za Angani

Ukweli wa Kustaajabisha Kuhusu Nyota za Angani

Status
Not open for further replies.
Really? well you are a self-contradicting figure.

Well, kwani sisi tunaishi dunia tofauti? If you have kids you should let them aim high, do not let your fiascos become part of others, FYI Scientists around the world are coming from every places. In astronomy and science in general your little lines drawn by other people and made you believe you can’t do this just because you are from somewhere is only inferiority complex.

That is interesting, it will be a great contribution for others and yourself if you can "acces Google it" and then translate via google translator and share with us. We will be waiting even if you will take your chosen area such as "War in Gaza, Ebola and hunger in Ethiopia" or “katiba mpya and taifa stars” just don’t mix the forum.

There is nowhere that it has been claimed that this is new, even some details and theories are dating back to 1960, but still many would find them interesting and worth to read though it pain you so hard but of course I can understand, you provide a very good case of low self-esteem patient and I will use you in the topic that would help others to know about this kind of disaster starting to advance in our community. Genius? Oh no, I have said I am just another Tanzanian guy please take your time to read.

From another perspective, I could not see the coherence and main focus of your argument/s. What is the problem? Is it information posted that you don’t accept? Is it the way it is presented? Is it me as the presenter? Is it others who contributed and ask questions? Is it its morality, difficultness, or loo long for you to read? All this can be seen in your little paragraph then it only leave me to conclude that your arguments are too ambiguous and focus-less. They lack seriousness and collaboration to each other by mentioning incorrect things to support what you think.

We kiumbe unaakili nyingi mno..B-)
 
you have done a very good job on translating to us about stars, but one thing is missing, what is the source of this! Plagiarism of the highest order!!! Shame again unatuspoon feed to hapa tupe source ili watu tucritisize au kumodify hizi thiories acha blaa blaaa

Hahahaha 🙂 You should know what you are talking!

Kwanza unalalamika kwamba unakuwa spoon-fed alafu tena unataka uletewe sources? Sasa hapo how can spoon-fed end? You should get on your knees and get things that you claim are plagiarism and show how it was plagiarized. In-fact whatever you have been posted should have sources as well in order to play fair game.

I have read many books, meet many people, participated in many workshops, done number of studies, published several papers, written a book, participate in many conferences and webinars and read so many scientific journals and visited countless website that are dealing with science and space. Perhaps you have done the same but I kind of dont see that in your few lines spelling error posts.

Here is some sources for you go figure out and "critisize au kumodify hizi thiories" na kama una access kwenye Elsevier, Emerald changamka kwenye astronomical, astronomy and astrophysics, and astrophhsical journals dont wait to get spoon fed by me.

Pia nenda kamsome Brian Greene kwenye Elegant Universe, Fabric of the Universe, Hidden Reality na pia Richard Dawkins
Magic reality, alafu kuhusu kwanini jamii yetu isijifunze kuhusu science kitabu kinachokufaa ni Collapse cha Jared Diamond

Enjoy
 
Glory to God... Mambo makuu.. Magumu.. Tusiyo yajua!!! Probablly God is Living in one of those Gallaxy...!
 
At least you have meantioned some books, I can go through it, ila swali ni moja tuu kwa nini watanzania wakiwa critisized wanakuwa wakali sana??? Hili ni tatizo, huwezi ukaandika kitu watu wote tukapiga makofi, some people think differently, as I do. By the way, who cares about "I have read many books, meet many people, participated in many workshops, done number of studies, published several papers, written a book, participate in many conferences and webinars and read so many scientific journals and visited countless website" this is for you, what we need is what you got on bundle of books and how you have used those in improving our daily life.cheers!!
 
tunaomba uilete hapa hiyo "drake equation" kwa kiswahili chepesi na cha kawaida tunacho ongea huku manzese,tandele sinza na vitongoji vingine tz,siyo kile kiswahili cha google translator ambacho nacho ni mkorogano tu.ni kama anavyofanya mleta mada.tunamuelewa kwa lugha yetu ya mama.
ni ombi tu.hiyari yako kuchagua kutekeleza au kuacha.

That's your homework for this week.

Find what is "Drake's Equation".

Google unayo. Usipende kutafuniwa tu. Mie niliisoma mwenyewe kwenye vitabu, kabla.internet haijawa mainstream.

Leo wewe hata kitabu huhitaji.
 
Mkuu Kiranga, Thanks for your involvement. Yes my intention was to talk about basics and of course based on just "nature" and I did circumvented distinct notions which as I said would lead to confusion as a start thus obviously not about “number of communicating civilizations in our galaxy” or “a cat state of being alive and dead at same the mind of an observer” in order to explain quantum mechanics. Or would "mentioning" them at the start make stars facts more comprehensible?

Would it be sensible to start a topic about elementary facts about stars and jump right away to intelligent beings in our galaxy and behaviors of the smallest particles? No I don’t think so and as you may perhaps realize that some even took it as fortune-telling and inquire explanation of Gemini and Sagittarius. Knowing about science is cool but knowing your audience is a common sense. I think you can pick it from there and carry on to any direction not consider my outline as “limited” but rather a start.
🙂

Rest assured in.my eyes you are doing nit only well, but important work to popularize some of these concepts.

I was not at all considering your input limited, one has to pick a starting point somewhere after all.

I was reponding to someone on a tangent specifically targeted to that person, with exactitude.

Do not confuse the two.
 
Hivi nyota zinasaidia nini Tanzania kupata katiba mpya, au taifa stars kushiriki walau kombe la mtaa achilia mbali la dunia, To the hell na manyota yako, elimu ambayo haina application ni hadidhi tuu za kusimulia watoto ili walale kwa kiswahili zinaitwa Ngano

Unajimu.ndio.uliotupa calendar, iliyoweza kufanya watu walime kwa misimu, na kupata mafanikio ya kusaza chakula, sazio lililoweza kuwafanya wafikirie matatuzo mengine makubwa kama kujipanga katika serikali na kutoa huduma nyingine zote kama hizo za elimu, kuwa na katiba etc.

Sasa hivi kunaweza.kuwa na.kimondo kinakuja kugonga dunia na kuiunguza.

Je, ungependa kujua kama.kipo na kama.kipo kipo umbali gani na unawezaje kukipasua kabla hakijafika duniani?

Au ungependa kula majani tu kama ng'ombe.siku moja ushtukie tu daflao kama kiama?
 
At least you have meantioned some books, I can go through it, ila swali ni moja tuu kwa nini watanzania wakiwa critisized wanakuwa wakali sana??? Hili ni tatizo, huwezi ukaandika kitu watu wote tukapiga makofi, some people think differently, as I do. By the way, who cares about "I have read many books, meet many people, participated in many workshops, done number of studies, published several papers, written a book, participate in many conferences and webinars and read so many scientific journals and visited countless website" this is for you, what we need is what you got on bundle of books and how you have used those in improving our daily life.cheers!!

I think you do care and that response was for you specifically on origin of the information that I am writing. You know galloping a donkey along miles of sandy beach is one of the most exhilarating things you can do but it can also be one of the most dangerous. You got to somehow use donkey gestures to get things along.
 
Haaaa Jamaa anauza chai thus y chai nyingi town...

Also this can be put as: I responded to this knowledge with the kind of sophisticated language for which I am famous in my village. "thus y chai nyingi town" Poor guy.
 
Kijana it seems you know that field very well, but usikrem kila kitu kwa technologia yetu ya kibongo hiyo elimu sio muhimu sana kwamba inahitadi attention katika masomo yetu, hizo information ndeefu unazoleta hapa kila mtu anaweza kuziacces 'Google it' ulichofanya hapo ni kutafsiri tuu nayo pia kwa kutumia google translator, hakuna jipya hapo, watu ni wavivu tuu wa kutafuta mambo ulivyoandika hapa kuna watu wanakuona genius na wengine wanatamani upewe tuzo Nobel

Wengine tumepata elimu safi kabisa angalau kwa kiasi kidogo juu ya mambo ya anga...
Wewe pia kama una informations Zi-google uzianzishie thread tuelimike...

Hapo umeuliza swali? Umetoa ushauri au Umefanyeje?
 
Mkuu pachanya, shukrani kwa maelekezo bayana kabisa kwa watu wa aina hii.
 
Unajimu.ndio.uliotupa calendar, iliyoweza kufanya watu walime kwa misimu, na kupata mafanikio ya kusaza chakula, sazio lililoweza kuwafanya wafikirie matatuzo mengine makubwa kama kujipanga katika serikali na kutoa huduma nyingine zote kama hizo za elimu, kuwa na katiba etc.

Sasa hivi kunaweza.kuwa na.kimondo kinakuja kugonga dunia na kuiunguza.

Je, ungependa kujua kama.kipo na kama.kipo kipo umbali gani na unawezaje kukipasua kabla hakijafika duniani?

Au ungependa kula majani tu kama ng'ombe.siku moja ushtukie tu daflao kama kiama?

Hahahahaha! Eti kula majani kama ng'ombe. Usimlaumu jamaa unajua sie waafrika kwa asilimia kubwa tunachojali ni je leo nimekula vp kuhusu kesho ntakula pia na jingne ilmradi nimelala salama na nimeamka poa. Masuala ya teknolojia watajiju wazungu sie hayatuhusu yaani maisha yetu hayana tofauti na mifugo kama mbuzi.
 
Mtu anauliza umuhimu wa kujua elimu ya anga na unajimu.

Hata historia ya civilizations, na jinsi Egyptians walivyotupa habari za kalenda huyu hajui.

Sasa ni wa kuhurumiwa tu, kwa ujinga ambao hauwezi kujua elimu.ya anga ilivyojikita kila pahali.

Pia hajui kwamba, ugunduzi mwingi katika sayansi unaokuja kupata practical applications, huanza kama abstract curiosity.

Einstein alivyogundua relativity theory kuna watu wengi waliona thus is just a mathematical and abstract curiosity.

Leo hii tumepata GPS, unaenda sehemu huijui, GPS inakuongoza.

Tungesema tusichunguze vitu mpaka tuone practical application, tusingekuwa na umeme wala GPS.
 
Hujaongelea vimondo, vipi mahusiano yake na nyota?
Kwa vile kuna baadhi ya vimondo vilishawahi kudondoka duniani, inachukua muda kufika katika ardhi yetu?

Ni vizuri pia ukaelezea habari ya mwezi na mahusiano yake na ulimwengu wetu/jua

Mkuu platozoom, Labda kwaza tuongelee vimwondo na mwezi tuuache kando kwanza. Mwezi una mambo yake pia na ni mengi hivyo tutaujadili au kuuzungumzia baadae.

Asili ya vimwondo

Vimwondo ni miamba, mawe, mchanga au maumbo ya mkusanyiko wa madini yanalolizunguka jua ama yanayozunguka sayari nyinginezo, inategemeana tu na umbali lakini yote yako katika mizunguko (orbits) tofauti. Kuna wakati vinasogea karibu na hivyo kuingia kwenye mzunguko wa sayari yetu. Vinakuwa na majina tofauti kitaalam kutokana na size composition eneo vinapozungukia na hata vile vinavyoangukia duniani basi jina linabadilika kama tayari kimeshaanguka. Mfano meteor (ule mwanga wake kikiwa kinaanguka na kuwaka moto) alafu meteorite kile kipisi cha mwamba au jiwe au chuma kilichobaki baada ya kuanguka.

Vimwondo vipo siku zote katika solar system na pale vinapochomoka kwenye orbit zake mara nyingi vinakuwa either vimetokea katika Oort cloud au kwenye Kuiper belt ile inayozunguka sayari ya Neptune. Lakini kuna belts nyingine ambazo zimejaza haya mawe na mabonge ya barafu kuanzia kwenye mzunguko wa sayari ya Mars mpaka ile ya Jupiter. Asili ya vimwondo inasemekana ni wakati ule Big-Bang ilipotokea na ni mabaki ya sayari ndogo zilizopasuka na vipande vyake vimekuwa vikigongana na kuvunjana mpaka sasa hivyo sio matokeo ya nyota moja kwa moja.

Mara nyingi vimwondo vinaishia hewani.

Dunia imeshagongwa na vimwondo mara nyingi sana na hata ushahidi tunao pale mbozi Mbeya na sehemu nyingine maarufu lakini kwa silimia kubwa huishia na kuyeyuka hewani kabla ya kugonga dunia. Binafsi nimesha tembelea pale Mbozi na kwa kweli ni kitu cha kujivunia kuwa na kivutio kama kile lakini hakijajengewa au kutengewa eneo linaloendana nacho (hadhi). Kama ingekuwa sehemu nyingine pale pasingekuwa vile.

Kile kilichoanguka Urusi mwaka jana (February 15, 2013) katika mji mdogo wa Chelyabinsk ndio kilitoa somo zuri maana tayari kuna technology zenye kupima na kurekodi karibu kila kitu kinachotakiwa. Ukubwa wake ulikuwa mita 15 na uzito wake kama 7000 metric tons kabla ya kuingia katika anga la dunia. Mwendo wake ulikuwa 65,000km/h hiyo ni velocity kali sana na ndio pona pona yetu maana kwa mwendo huo kikiingia tu kwenye anga la dunia "Earth atmosphere" kinaanza kuungua kutokana na msuguano mkali sana. Kumbuka mwendo wa risasi ni kilomita elfu moja na mia mbili kwa saa (1,200km/h) hivyo ni wazi kimwondo kile kilikuwa na mwendo mkali mara nyingi sana zaidi ya risasi. Vipande vidogo tu viligusa ardhi baada ya kuungua na kulipuka ila shockwave na sauti yake watu wengi waliumia kwa kupanic, madidisha ya vioo yalipasuka na kuta za nyumba nyingi zilianguka. Na kama kingetua kama kilivyo bila kuungua na kulipuka basi ni impact yake ingekuwa zaidi ya bomu lilioangushwa hiroshima.

Wastani wa vimwondo kugonga Dunia.

Kila mwaka zaidi ya tani mia moja za vumbi na mchanga kutoka angani zinatua duniani na kwa wastani wa mara moja kwa mwaka kimwondo chenye size ya gari dogo huingia kwenye anga la dunia (Earth atmosphere) lakini huungua chote kabla ya kutua duniani. Kwa wastani wa kila miaka 2000 kimwondo cha ukubwa wa saizi ya uwanja wa mpira hugonga dunia na kusababisha madhara makubwa katika eneo husika.

Na katika wastani wa miaka milioni 10 hadi 100 kimwondo kikubwa zaidi kama saizi ya jiwe kubwa lenye upana wa kilomita 2 hadi 7 hugonga dunia na kutengeneza shimo kubwa sana, mlipuko zaidi ya bomu la nuclear, tetemeko, moto, vumbi, hewa chafu na moshi mzito ambao unaweza kukaa duniani kwa zaidi ya miaka elfu moja na hivyo kubadili majira ya dunia kwa kutoruhusu mwanga wa jua kupenya. Hiki ndicho kinachohofiwa sana maana ni wazi viumbe vingi vitafutika lakini sio maisha kwa ujumla.

Mfano mzuri wa hili unaelekezwa kwenye kimwondo kikubwa zaidi kilichoanguka zamani sana kabla binadamu hatujawa katika hali hii ambacho kinadhaniwa kuchangia kufuta wale reptiles wakubwa waliokuwa wametapakaa duniani (Dinosaurs) miaka millioni 65 iliyopita na pia kubadili majira na hali ya hewa ya dunia. Ingawa uwezekano wa kugongwa na kimwondo kikubwa ambacho kitaleta madhara mazito ni mdogo sana, lakini upon na inadhaniwa hutokea mara moja kwa kipindi kirefu labda miaka millioni mia moja. Kwa kuhofia hilo kuna baadhi ya programs zenye technologia ya juu sana zimejikita kuchunguza mwenendo wa vimwondo hasa vile vikubwa vinavyoweza kuleta madhara.

Labda pia labda ni bahati kwamba kimwondo kilibadili mazingira ya dunia na kutufanya binadamu taratibu tuongezeke kwa kuwa wale kina T-rex wasingetuacha. Si ajabu kujificha mapangoni kwa binadamu wa kale ndio ilikuwa suluhu. Labda kila kitu kinatokea kwa sababu maalum.

Airburst Explained: NASA Addresses the Russian Meteor Explosion
Comet/Asteroid Impacts and Human Society (2007). Authors: Bobrowsky, Peter T., and Hans Rickman
Fifty Years on the Space Frontier: Halo Orbits, Comets, Asteroids, and More.(2010). Authors: Farquhar and Robert Willard.
Asteroid Rendezvous: (2002). Authors: Bell, Jim, and Jacqueline Mitton
 
thank you so much iam geografy teacher i add sme thng in ma head now
 
Mgalanjuka Thanks kwa majibu post #125 .

Labda ungeogezea kidogo kama kuna any hypothesis juu ya sababu au chanzo kilichopelekea kuwepo kwa sayari, nyota nk, ni mchanganyiko upi uliosababisha mabonge makubwa yenye mawe, miamba n.k kuwepo kwenye galaxy. Unaweza kurudi nyuma pia kuangalia kabla ya kuwepo kwa sayari, nyota n.k kulikuwa na nini
 
Last edited by a moderator:

Theories zilizo na nguvu au ushawishi kisayansi za kuwepo sayari na nyota na kila kitu ni Big-bang theory ambayo ina-suggest mwanzo wa universe kama mlipuko mkubwa kabisa. Kutoka katika mlipuko huu kila kitu kinachoonekana sasa ni matokeo yake. Labda tukiichambua hii kwa kuegemea kwenye upande fulani bila ya kuchanganya tunaweza kupata mwanga fulani kwenye eneo hili. Ninamaanisha swali lako ingawa ni paragraph moja ila ni kubwa kuliko kawaida. Ukisema nyota na sayari ni kwamba hivi ni vitu viwili tofauti vyenye vyanzo tofauti na kimoja (sayari) kikiwa ni matokeo ya kulipuka kwa kingine(nyota). Pia miamba, mawe, mabonge ya barafu, mchanga na vumbi la kila aina pia ni vitu vilivyo angani maeneo tofauti na zenye vyanzo tofauti. Haya yote yanaweza kujibiwa katika Big-bang theory.

Katika kuelewa vizuri vitu vikubwa angani na mwanzo wake pia theories kuhusu vitu vidogo kabisa (Quantum theories, String theory, etc) zinatumika zikichanganywa na zile za vitu vikubwa (General relativity etc) Ukishajua behaviors za matter katika misingi yake ya chini au mwanzo kabisa (atomic level) basi unaweza kutengeneza theories ambazo zinaweza kusaidia kujibu maswali makubwa kama mwazo wa universe. Mfano experiments zilizofanyika Switzerland kwenye cern project ili kutafuta ushahidi wa kuwepo higgs particles pia unatoa mwanya wa majibu mengine ya kifizikia yalikuwa pending kuhusu mwanzo wa ulimwengu maana pale kilichotokea katika experiment ile (particles colliding) inafananishwa kwa njia moja ama nyingine na mlipuko ule wa big-bang katika large scale. Sayansi inaendelea na tutapata kujua mambo mengi zaidi.

Sasa katika kujibu swali lako tujikite kwenye kitu kimoja baada ya kingine tusiweke mambo mengi maana tutaishia kuchanganya ama kuwachanganya wengine.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom