Ukiachana na historia ya kwenye vitabu, nimepata bahati ya kufika Zanzibar na kutembelea Soko la zamani la watumwa. . .niliyojifunza pale hakika nilisikitika, ndipo nilipoamini Waarabu (wa zama hizo) hawakuwa na utu kabisa, kuanzia kuwachukua watumwa bara na kisha kuwaleta Zanzibar,(enzi hizo bandari ipo Mangapwani) kuwafunga kwenye mti na kuwachapa mijeledi na mtumwa ambae halii ndio anaonekana mkakamavu...
kisha wanapelekwa mpaka sehemu ya kutunzia watumwa (ipo mpaka leo) ambako wanafungiwa kwa siku 3 bila chakula wala maji!!!,(kumbuka minyororo mizito bado mmefungiwa nayo mikononi, miguuni na shingoni) kisha ndio mnatolewa ambao atakutwa amekufa anatupwa na waliobaki wanaenda kuuzwa.
Ikitokea katika kundi la watumwa wa kike wanaouzwa tajiri akitaka “kuonja" alikuwa anachagua mmoja na kumfanyia hiko kitendo hapo hapo hadharani. (kama ambavyo mnafahamu wanaume tulivyo , mwenzako akifanya kitu nawe unataka kufanya, mfano katika kundi mmojà akisogea pembeni na kufungua zipu ili achimbe dawa utakuta wawili watatu wanaungana naye kufanya hivyo, hata walipokuwa wanatwaa mtumwa mmoja wa kike na kumfanyia ushenzi, basi wengine nao waliungana kufanya ufedhuli huo kwa wengine kwenye kundi hilo)
Watumwa waliteswa sana, sana , sana!!! na hao waarabu ambao leo hii watoto wao tunaishi nao kwa amani.
Cha kusikitisha zaidi ni kitendo cha kuwahasi watumwa kiume waliosafirishwa kwenda Arabuni( walienda maelfu lakini mpaka leo hii jiulize kwanini hakuna masalia ya weusi kama sio ukatili wa waarabu ambao waliwahasi bila taratibu za kitabibu, yaani wanakata hizo gololi kisha unapakwa chumvi nyingi, na kutokana na kuvuja damu nyingi wengi walikufa, wachache waliobahatika kupona waliuzwa arabuni kwa hela nyingi, walivyoona wakubwa wanakufa sana basi wakawa wanawahasi watoto).
Bado ambao walikataa utumwa na kuleta uasi njianwaligeuzwa na kuf**lwa mbele ya watoto na wanawake, ili kuwafanya wajisikie majuto, na hata waoivyokuwa wanasafiri na majahazi ilikuwa ni desturi ya waarabu kuwachukua watumwa wa kiume na kuwageuza ili kukidhi haja zao.
hivi vyote vilifanyika na historia ipo fika Zanzibar au hata Bagamoyo soko la watumwa uone historia picha na vithibitisho vingine kuhusu ufedhuli huo.waliofanyiwa mababu zetu (leo hii tunacheka nao hakika mababu zetu wakifufuka watasikitika sana).
Dini hizi hizi tulizoletewa tunafundishwa kusamehe waliotukosea, ilhali waliotuletea hizo dini walitufanyia ukatili huku tukishuhudia nasi tunachekelea kama mazombi. Tuishi kwa amani, tupendane na tusonge mbele tukitaka kuleta habari za historia na tuzibebe chuki za mababu zetu basi tutachukiana daima na tutauana.
Japo Muingereza alikomesha utumwa wa waarabu lakini naye alitesa manamba mashambani, Mbelgiji aliua watu wengi kongo,na mkaburu aliangamiza vizazi Afrika kusini, Huu ushenzi tuliofanyiwa waafrika ni mkubwa lakini tumesamehe na tuishi kwa amani bila kubaguana ili tusisahau na tuwaeleze vizazi vijavyo namna ambavyo mababu zao walipitia mateso ya wadhalimu waliokuja ili kutimiza haja za nafsi zao.