Ukweli wazidi kujulikana. Dada aliyejitambulisha kama Mkatoliki ni Katibu wa UVCCM Tawi la Dovya

Kama huyu ni katibu yupo hivo pata picha hao anaowaongoza wapo vipi

Kweli huko sisiemu hakuna mwenye akili kuanzia mwenyekiti mpaka katibu wa tawi
 
Hivi huko UVCCM na CCM kwa ujumla? inakuaje kanisa lao linadhalilishwa kiasi hiki na wao kubaki kimya kama si kuhusika kulifedhehesha kanisa lao? misheni mbovu zinapangwa na wao wamo humohumo hawa react, ni umasikini wao au ni kulinda vibarua vyao?
 
Wakatoliki hawawezi kumnyanyasa huyo binti
Wakatoliki wanajali sana haki, sio amani pekee
 
Kanisa langu haliwezi kufedheheshwa namna hiyo na mimi nimo ndani ni lazima nitibue huo mpango haraka sana. Hao wakatoliki wa ccm akili zao zikoje?
 
Acha uongo- Hivi wakatoliki wangapi wanalifahamu jina la Papa. Hipa nilipo kazini wapo wakatoliki watano, nimewauliza jina la Papa ni wawili tu ndio wamelifahamu. Wengine wakajibu, la muhimu ni kufahamu tu kiongozi mkuu wa ukatoliki duniani ni Papa.
Huna akili unajibunia tu ujingaz!
 
Amani ya nchi hii imo mikononi mwa wakatoliki aisee, ingekuwa kobazi wanafanyiwa michezo hii wangetembeza bakora na majambia wale wehu, wasingevumilia dini yao kuchezewa kishenzi namna hii
 
Kila taasis na taratibu zake
 
Hivi huko UVCCM na CCM kwa ujumla? inakuaje kanisa lao linadhalilishwa kiasi hiki na wao kubaki kimya kama si kuhusika kulifedhehesha kanisa lao? misheni mbovu zinapangwa na wao wamo humohumo hawa react, ni umasikini wao au ni kulinda vibarua vyao?
Mkuu haya yote yanatokana na ulichoandika hapo chini mwisho kwenye post yako.

Hakuna kingine.
 
Wakatoliki hawawezi kumnyanyasa huyo binti
Wakatoliki wanajali sana haki, sio amani pekee
Akinyanyaswa tutamsikia, pengine kama akitolewa roho yake. Sina mawasiliano naye ila nitafuatilia kwa karibu na kujaribu kupata mawasiliano naye. Nimelichukulia hili swala kwa umakini mkubwa. Imeniudhi sana hoja za mtoa Uzi, tena nimesikitishwa sana.
 
Chama mbona kinafanya mambo ya kitoto hivi?
 
Acha uongo- Hivi wakatoliki wangapi wanalifahamu jina la Papa. Hipa nilipo kazini wapo wakatoliki watano, nimewauliza jina la Papa ni wawili tu ndio wamelifahamu. Wengine wakajibu, la muhimu ni kufahamu tu kiongozi mkuu wa ukatoliki duniani ni Papa.
Ndio maana mnaonekana wapumbavu tu Kwenye Misa za kikatoriki Kila Jumapili lazima jina la papa na Jina la askofu mkuu wa Jimbo kuu yatajwe, Sasa hao waumini hawasaligi mpaka kushindwa kujua majina ya hao watu muhimu katika ukatoriki?.
 
Rip Ruge.....'Ogopa Mungu na teknolojia.'
 
Alishindwa pia kutamka jina la Askofu anayemshtaki na Papa anayempelekea mashtaka. Sasa sijui kama hata anajua anachokilalamikia. Hakuna mkatoliki asiyejua kutamka jina la askofu wa jimbo lake, hata watoto wadogo wa Utoto mtakatifu, labda kama ni mkatoliki jina tu na awe alienda kanisani mara ya mwisho alipopata kipaimara miaka kadhaa iliyopita na hajakanyaga tena. Askofu huwa anaombewa kwenye kila misa, anatajwa kwa jina lake, na kama askofu ana msaidizi ama wasaidizi pia wanatajwa kwa majina yao. Papa pia anatajwa kwa jina lake kwenye kila misa. Kutokana na hii majina huwa yanabaki kwenye kumbukumbu na unajua namna ya kuyatamka. Tukiacha code nyingine za kikatoliki ssiyejua majina ya Paroko, Askofu wa jimbo lake na Baba Mtakatifu....huyo ni mkatoliki wa mchongo. Hakuna mkatoliki anayeweza kufanya press kumlalamikia hata katekista. Acheni kulitesa kanisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…