Ukweni hawanitaki, wanasema nimempa dawa kijana wao. Nifanye nini?

Habari wana jf,

Mimi ni binti wa miaka 26 na nipo kwenye mahusiano na Tunatarajia ndoa ila Ukweni wanaweka pingamizi sana na sijawahi fanya chochote kibaya na wala sina mazoe na wakwe zangu ila chakushangaza mama mkwe Anamuuliza Kijana wake "Hivi Bado upo na yule mwanamke tu kwani amekupa nini? Si umwache mbona wanawake wapo wengi umekaa nae muda mrefu hivyo itakua amekupa Dawa huyo"
Na ukweli nikwamba mimi sijui mambo ya Dawa wala ushirikina

Namwamini sana MUNGU Na hata kumpata huyu mwanaume nilifunga kwa maombi nikaongea na MUNGU anijalie mwenza wa maisha na sio kupoteza muda
Ila nashangaa kwao kumekuwa na pingamizi sana
(ila kwao wana imani za kishirikina)

Mara wanasema najipendekeza kwao mara nimemloga mwanao, sasa nashindwa kuelewa ana tatizo gani hasa hawa wakwe zangu, ila nikikutana ma mama mkwe anafurahi nampa zawadi na yeye ananipa zawadi na tena mara nginyi ni yeye ananipigia simu niende tukapange siku za weekend's ila akiwa na mwanae ndo anamwambia hayo maneno na mwanae anakuja nieleza.
Legeza dawa wenzie wakipewa wanauliza najinsi ya kulegeza

Punguza kidogo
 
Kama kwao ni wachawi achana na hiyo familia, ukizidi kung'ang'ania watakumaliza ww kwanza au uzao wako. Hao wazazi kuna kitu walitarajia kwa kijana wao labda kuoa binti kabila moja na wao au binti walisha muandaa, kwani ww ni kabila moja na mchumba wako?
hivi siku izi kuna kuchaguliana mchumba?
 
Huyo jamaa yako ndio mwenye matatizo. Yeye kama mwanaume anatakiwa awe na msimamo na anachokitaka. Hayo mambo ya mwanao ana mwanamke gani sio juu yao, hawakutakiwa hata kuongea namna hiyo juu yako, hiyo familia ni ya kihuni. Maamuzi ni yako.
 
Kama kwao ni wachawi achana na hiyo familia, ukizidi kung'ang'ania watakumaliza ww kwanza au uzao wako. Hao wazazi kuna kitu walitarajia kwa kijana wao labda kuoa binti kabila moja na wao au binti walisha muandaa, kwani ww ni kabila moja na mchumba wako?
Imagine unachaguliwa binti wa kumgeuza kitandani? Huo ni uboya high quality. Huyo jamaa hafai kuwa baba wala kiongozi wa familia.
 
Habari wana jf,

Mimi ni binti wa miaka 26 na nipo kwenye mahusiano na Tunatarajia ndoa ila Ukweni wanaweka pingamizi sana na sijawahi fanya chochote kibaya na wala sina mazoe na wakwe zangu ila chakushangaza mama mkwe Anamuuliza Kijana wake "Hivi Bado upo na yule mwanamke tu kwani amekupa nini? Si umwache mbona wanawake wapo wengi umekaa nae muda mrefu hivyo itakua amekupa Dawa huyo"
Na ukweli nikwamba mimi sijui mambo ya Dawa wala ushirikina

Namwamini sana MUNGU Na hata kumpata huyu mwanaume nilifunga kwa maombi nikaongea na MUNGU anijalie mwenza wa maisha na sio kupoteza muda
Ila nashangaa kwao kumekuwa na pingamizi sana
(ila kwao wana imani za kishirikina)

Mara wanasema najipendekeza kwao mara nimemloga mwanao, sasa nashindwa kuelewa ana tatizo gani hasa hawa wakwe zangu, ila nikikutana ma mama mkwe anafurahi nampa zawadi na yeye ananipa zawadi na tena mara nginyi ni yeye ananipigia simu niende tukapange siku za weekend's ila akiwa na mwanae ndo anamwambia hayo maneno na mwanae anakuja nieleza.
jikabidhi kwa Mungu, omba juu ya tatizo Hilo Utapata majibu.
 
Back
Top Bottom