Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Hii lugha ya kiswahili haina soko. Kwasabb ilipaswa kubeba teknolojia/maarifa ambayo ndiyo yangevutia watu kujifunza kiswahili
Lugha ya kiswahili naona waoitetea wanajikita katika kuipondea lugha ya kingereza lakini ukweli ni kwamba ukitaka lugha ikue lazima uwape sababu watu Kwanin watumie lugha yako na sio lugha nyingine
 


Kama unajua lugha zote kinakuuma nini? Ni lugha tu ndugu yangu haina maana kiswahili kimeshuka ukiongea Kingereza !
 
Anamsomea nani hizo vizungu za kwenye makaratasi?

Wewe mama yako anajua Kiingereza kweli?
 
Kama hujui Kiingereza Acha Wivu
 
unaweza kuwa na wazo zuri lkn unakosa busara ya kuliwasilisha ....toa maoni yako vizuri na ktk kuwasilisha kwako usijaribu kuonesha ww ndio upo sahihi sana na wengine ni hovyo #BUSARATAFADHALI
 
..anatakiwa aandikiwe HOTUBA nzuri ya kuwasilisha mbele ya wenyeji wake
Heheheee....

Kuwa kiongozi sio swala la kuvaa tu ushungi na kurembua. Uongozi ni kipawa.

Kwa tunaofuatilia siasa za kimataifa, tunaelewa nini maana ya Kiongozi mwenye kipawa cha uongozi.

Nikupe kijikazi kidogo — fuatilia hotuba ya Obama ndani ya bunge la uingereza.

Nina uhakika kwamba, itamchukua Bibi sasha zaidi ya miaka mia kuweza kumudu ile mastery ya oratory skills.

Ndio maana, sisi wenye utambuzi wa mambo, tunashangaa anapotusomea vizungu vya kwenye makaratasi.

Lakini kwa ninyi magoigoi msiojua dunia inaenda wapi, kwa hakika anawakoga sana kwa kile kizungu chake butu.
 
unaweza kuwa na wazo zuri lkn unakosa busara ya kuliwasilisha ....toa maoni yako vizuri na ktk kuwasilisha kwako usijaribu kuonesha ww ndio upo sahihi sana na wengine ni hovyo #BUSARATAFADHALI
Busara gani unayoitaka?

Unataka nikulambe miguu?
 
Tatizo lako la 'Language Barrier' lisiwe 'Chukizo' kwa wale 'Wordsmiths' wa hiyo ( hii ) Lugha ya Kiingereza. Vituo vya Kufundisha vyema hii Lugha muhimu duniani ( ya Kiingereza ) vipo vingi nenda 'Ukanolewe' zaidi uijue ili usiwaonee tena 'Kijicho' wale wanaoijua vyema sawa?

Kwani mfano Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiongea kwa Lugha ya Kiingereza ambayo Wakenya wengi wanaimudu na Wewe usiyeijua ukatafsiriwa kila Kitu kwa Kiswahili chako 'Kilichokudumaza Fikra' tokea Uhuru mpaka leo utakuwa Umepungukiwa na nini?
 
Kati ya mambo ya kipumbavu yaliyo asisiwa na kuachwa na awamu ya tano ni chuki dhidi ya Kiiingereza na ukitaka kufa kwa cheko Bashite apige ngeli, Ndalichako akiongea kimalkia utazikwa na mzee baba R.I.P akipiga ile "pipo uzed to die in ze ze rake" tunakula matanga.

Lugha huenea kutokana na product zinazozalishwa kutoka kwa wenyeji, sasa mtu amekomaa na Kiswahili na akati product ni udaga, togwa pambaav
 
Analeta mikogo mwishowe anachemka... Alileta mbwembwe kwenye maneno
"reiterate... expeditiously..." akakwama nayo..
Hahahahaaaaa....

Werevu mwingi mbele giza.

Mtu mswahili unajilazimisha vizungu!

Yaani.....
 
Nina uhakika wewe na nduguzo wote mkiunganishwa hamuwezi kunipiku umahiri nilionao wa kutema mayai.
Mkuu jibu comments kwa ung'eng'e jamaa asante akujue wewe ni nani linapokuja suala la kimombo, washangiliaji tupo.
 
chuki dhidi ya Kiiingereza
Wala hakuna chuki yoyote hapo wewe zumbukuku!

Matter of fact, ninazungumza lugha nne za Kimataifa kwa ufasaha ikiwemo hicho kizungu chako.

Ninyi wajinga wajinga mliosoma shule za makuti ndio mnababaika na vizungu vya kusoma kwenye makaratasi.

Mimi nilishavuka hivyo viwango vya kubabaikia vizungu toka kitambo.

Niko viwango vya juu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…