Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya


..sio sahihi kuzungumzia "kurembua macho," na "kuvaa ushungi," halafu ukamtaja Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

..kuhusu Barack Obama, yule anajulikana kama mmoja wa wazungumza mahiri kabisa popote duniani.

..pia lazima uelewe kwamba hotuba ya Rais Obama ambayo umetutaka tuiangalie ni hotuba ambayo imeandikwa na alikuwa akisoma kutumia kifaa kinaitwa teleprompter.

..mimi nadhani sio sahihi kumtaka Rais wetu atoe hotuba kwa viwango vya Barack Obama, na haijalishi hotuba hiyo ni ya Kiingereza, au Kiswahili. nadhani tutakuwa hatumtendei haki hata kidogo kunatokana na kipaji cha kipekee alichokuwanacho Barack Obama.

..Rais Samia Suluhu awe na utaratibu wa kuandikiwa hotuba, na ahakikishe anafanya mazoezi ya kusoma hotuba hizo kabla ya kwenda mbele ya hadhira. Na haijalishi hotuba hizo ni za Kiswahili au Kiingereza. Viongozi wote wa mataifa makubwa hu-practice hotuba zao kabla ya kupanda majukwaani.

..Hotuba ya Obama nimeiweka hapo chini.

 
Very Good.

Wakati mwingine mjifunze kuchagua viongozi wenye VIPAWA badala ya kufuga fuga watu waliojichokea!
 
Uganda akiongea Kiingereza, sawa tu manake wale jamaa wana bifu na Kiswahili!!

Kenya, kwa kuwakomoa tu, anapaswa atumie Kiswahili manake Kiswahili wanakijua vizuri lakini kutokana na ulimbukeni wao wa kumsujudia Mzungu, wanajifanya hawakijui!!
Wakenya wote hufikiri kwa Lugha ya kigeni huona ni ufahari kuongea kingereza kuliko hata Lugha zao za Asili
 
Uganda siku ile, pamoja na waganda kukijua kiswahili lakini hadhira ile ilihusisha pia na wawekezaji wa bomba la mafuta ambao hawajui kiswahili bali kiingereza, kuna sababu gani kulazimisha kiswahili kama Magufuli aliyekuwa hajui hiyo lugha nyingine?
Kutojua kingereza siyo dhambi kwani hata wachina kwa idadi kubwa hawajui kingereza lakini wana tekinologia kubwa
 
Wakenya licha ya kuwa watumwa wa Lugha za Mkoloni bado ni washamba mbele ya watanzania kwani hata kuvaa vizuri hawajui idadi kubwa ni washamba kupindukia
 
Wachina German Spain ureno france korea hawajui kingereza wengi lakini wana maendeleo makubwa
 
Moja Kati ya mambo yanayonisikitisha sana ni hii tabia ya baadhi ya WaTanzania kushobokea lugha za kigeni hasa hasa English na kuona kiswahili si mali kitu.

Laiti kama wangejua kuwa kwenye nchi nyingi tu ambazo zinatumia lugha zao wenyewe,ukiongea hiyo English yako watu wanakuona mshamba tu bila kujali kama ni "broken " au "fluent"

Lakini cha ajabu hapa Bongo baadhi ya watu wanawaona viongozi wao washamba kwa kuhutubia kwa kutumia kiswahili,inasikitisha sana.

Sisi kama TAIFA,TUMEKOSA MISINGI,tunafuata tu mkumbo!!
 
Zumbukuku kingeli inaitwaje? Wewe ndugu ni lofa mwenzangu tu acha hizoo!
 

Muhimu kuongea lugha ya Kiingereza kuifikia dunia hata kama ni ziara ya Kenya ili kurudisha mguso wa kidiplomasia uliokuwa umepotea kwa Tanzania kimataifa

 
Sasa hivi dunia ni kijiji, macho yote kwa kiongozi huyu mpya wa Tanzania, hivyo fursa yoyote na jukwaa lolote ni vizuri kutumia lugha hii rasmi ya pili ya Kiingereza kupata 'matokea makubwa' ktk Geopolitics na diplomasia maana muda ni mchache mambo mengi fursa kama hizi hazitakiwi kuchukuliwa ni za "kikanda" bali ni jukwaa la kuiambia dunia Tanzania kuna fursa gani kibao ktk lugha inayotumika zaidi ulimwenguni
 
Tusijifungie kwa visingizio vya uzalendo na lugha ya kiSwahili.

Tuna bahati sasa viongozi wa juu hawaoni haya kutumia lugha ya Kiingereza kuifikia dunia iwe ni ktk jukwaa la hapa nyumbani au kikanda au kimataifa. Makamu wa Rais Dr. Mpango anatumia lugha ya kiingereza kama Rais Samia S. Hassan ili kuiweka Tanzania mahala pake kimataifa:
Dr. Phillip Mpango, discusses Africa's engagement with both new and traditional donors at a roundtable discussion organised by UONGOZI Institute (Institute of African Leadership for Sustainable Development) on 29 May, 2012.
 
Tumecheleweshwa sana na kiSwahili cha awamu ya tano, sasa tunarudi kimataifa

9 Aug 2019

Panel Discussion | Redefining Success​

Panel Discussion on “ Redefining Success" joined by * H.E Amb Pamella O’Donnell, High Commissionar of Canada in Tanzania, Zambia and Seychelles * Hon. Chansa Kapaya, UNHCR Representative in Tanzania * Dr. Blandina Kimala, Senior Researcher REPOA * Hon Sophia Mjema, Ilala D.C, United Republic of Tanzania. Moderated by Jocelyne Msigwa.
Source: SheFound
 
Hii ni hotuba ya Muheshimiwa Rais akiwa nje ya nchi inafatiliwa na dunia kiswahili tanzania tu kuna watu hawakielewi nadhani umeelewa tofauti ni jukumu ya habari maelezo kutafsiri kwa kiswahili kama kuna umuhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…