Watu duni hupenda kujadili watu wengine, watu welevu hujadili mawazo
Rais kuongea Kiswahili kwenye ziara yake Kenya haitofanya lugha yetu ikue ghafla, ili Kiswahili kikue tunahitaji kuja na mikakati ya kukikuza, lazima tutengeneze uhitaji wa lugha ya Kiswahili duniani, lazima tuandike vitabu, lazima tuongeze bidhaa zitakazofanya Kiswahili kitafutwe duniani.
Sasa badala ya kujadili namna gani tutafanya hayo tunalazimisha Rais aongee akiwa ugenini. Unadhani kuna mtu ataenda kujifunza Kiswahili sababu Rais ameongea kwenye ziara Kenya?