Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Rais needs to address Kenyans in a Language that Will be understood by many.
Have u noticed that Kenyans are celebrating the demise of the late and the rise of mama?? Have u noticed that her visit is largely anticipated by Kenyans??
Can u figure out why??
 
Moja Kati ya mambo yanayonisikitisha sana ni hii tabia ya baadhi ya WaTanzania kushobokea lugha za kigeni hasa hasa English na kuona kiswahili si mali kitu.

Laiti kama wangejua kuwa kwenye nchi nyingi tu ambazo zinatumia lugha zao wenyewe,ukiongea hiyo English yako watu wanakuona mshamba tu bila kujali kama ni "broken " au "fluent"

Lakini cha ajabu hapa Bongo baadhi ya watu wanawaona viongozi wao washamba kwa kuhutubia kwa kutumia kiswahili,inasikitisha sana.

Sisi kama TAIFA,TUMEKOSA MISINGI,tunafuata tu mkumbo!!
Mkuu, ukiwajulia watu wa Jamiiforums huwezi kupata tabu!

Humu kuna wajuaji wengi lakini bahati nzuri ni wajuaji wasiojua kitu.

Na kwa vile mitandao inazoa every tom and dick, basi kila mtu anataka kujitia mchambuzi nyuma ya keyboard ilimradi tu ajitutumue.

Huwezi ukaacha kutumia lugha yako ukarukia lugha za wengine. Ni ukichaa.

Ati diplomasia! Yaani kwa mujibu wa hawa vinyangarika; diplomasia ni kuongea kizungu!

Bila kizungu huwezi kuchagiza diplomacy!

Anayezungumza na kushupalia hayo, yeye mwenyewe hawezi kutamka japo "tree".
 
Muhimu kuongea lugha ya Kiingereza kuifikia dunia hata kama ni ziara ya Kenya ili kurudisha mguso wa kidiplomasia uliokuwa umepotea kwa Tanzania kimataifa

Kwahiyo huwezi kufanya diplomasia bila kizungu? Ona jinga hili!

Wachina na warusi mbona wamekupiku kwenye kila jambo pamoja na hicho kiingereza chako cha kuokoteza?

Ati diplomacy sijui nini nini!

Umejipiiindaa mwenyewe unaandika uharo mtupu!
 
Uko sahihi kabisa Ambokile Amanzi

Hadi sasa SADC wameanza kkujifunza Kiswahili. So Rais anatakiwa aendelee kukikuza.
Huyo Bibi sasha sijui kama anaelewa hili.

Mradi tu kavaa ushungi basi yeye ni kujimwaga tu na kizungu cha makaratasi.

Ni maajabu sana, tuna lugha yetu kubwa tu ambayo imeenea karibu nusu ya Afrika, lakini watu bado watajilazimisha kuongea vizungu!

Sijui ni ugonjwa wa akili?
 
Sijaelewa, una maanisha: Shule = Maarifa?

And then Maarifa iwe = Kiingereza?
Nimeuliza. Mi huwa nadhani ile dhana ya usomi ni kujua kuzungumza kiingereza kwa ufasha ni makosa. Tena imefika mbali kwamba uwezo wa ubongo wa mtu unaangaliwa kwa hiyo lugha.

Tulipo sasa, MAARIFA=PESA
 
Nimeuliza. Mi huwa nadhani ile dhana ya usomi ni kujua kuzungumza kiingereza kwa ufasha ni makosa. Tena imefika mbali kwamba uwezo wa ubongo wa mtu unaangaliwa kwa hiyo lugha.

Tulipo sasa, MAARIFA=PESA

Inategemea na ulivyoangalia context.

Usomi siyo kujua kuongea kiingereza kwa ufasaha, unless unataka kutwist topic.

Asilimia zaidi ya 80 tunajifunzia kiingereza shuleni, kwa sababu siyo lugha inayotumika mtaani kwa Bongo. Kuna nchi za wenzetu kama Kenya, hii ni lugha ya taifa, hivyo mtaani mnaongea tu, uwe umeenda shule au hujaenda utaijua.

Hapo ndipo linapokuja swala la kwamba ukimsikia mtu anaongea kiingereza (Kwetu Tanzania), moja kwa moja unajua huyu kapita shule (ingawa kuna hiyo 20% inayoweza kuwa imejifunzia nje ya shule, labda kaishi na watu ambao hiyo ni lugha yao ya mawasiliano na akajifunzia hapo).

Swala la maarifa na usomi ni topic tofauti.
 
Ndio maana unaitwa Denlson.

Mnyaturu wa singida ndani huko mavumbini unaitwa DENLSON...... Aisee!!!

Kwa kukusaidia tu "Bwana Denlson", Lugha ya Taifa ya Kenya ni Kizungu pamoja na Kiswahili. Na zote ni lugha rasmi zinazotambuliwa na Katiba yao mpya.

Kwako DENLSON.
Watu duni hupenda kujadili watu wengine, watu welevu hujadili mawazo

Rais kuongea Kiswahili kwenye ziara yake Kenya haitofanya lugha yetu ikue ghafla, ili Kiswahili kikue tunahitaji kuja na mikakati ya kukikuza, lazima tutengeneze uhitaji wa lugha ya Kiswahili duniani, lazima tuandike vitabu, lazima tuongeze bidhaa zitakazofanya Kiswahili kitafutwe duniani.

Sasa badala ya kujadili namna gani tutafanya hayo tunalazimisha Rais aongee akiwa ugenini. Unadhani kuna mtu ataenda kujifunza Kiswahili sababu Rais ameongea kwenye ziara Kenya?
 
Watu duni hupenda kujadili watu wengine, watu welevu hujadili mawazo

Rais kuongea Kiswahili kwenye ziara yake Kenya haitofanya lugha yetu ikue ghafla, ili Kiswahili kikue tunahitaji kuja na mikakati ya kukikuza, lazima tutengeneze uhitaji wa lugha ya Kiswahili duniani, lazima tuandike vitabu, lazima tuongeze bidhaa zitakazofanya Kiswahili kitafutwe duniani.

Sasa badala ya kujadili namna gani tutafanya hayo tunalazimisha Rais aongee akiwa ugenini. Unadhani kuna mtu ataenda kujifunza Kiswahili sababu Rais ameongea kwenye ziara Kenya?
Wacha manadharia yako bwana weye!

Kiswahili kilishakua na kuenea siku nyingi.

Na hapa wala sijasema lolote kuhusu kukuza Kiswahili.
 
Tumesikia Bi. Samia anaenda Kenya kwa ziara ya kikazi mnamo hapo kesho.

Ni matumaini yangu na fahari yangu kwamba, atatumia Kiswahili katika shughuli zote atakazoalikwa kuzifanya.

Hivi majuzi tu alipoenda Uganda, tuliona anatumia kizungu kuhutubia.

Wengi wa wananchi wetu nina uhakika hawakuelewa hata anachozungumza.

Ifahamike kwamba, Kiswahili si lugha ngeni Afrika Mashariki. Tuachane na Viingereza pasipo na ulazima.

Sijui ni nani aliyewalaghai kwamba kuongea kizungu ni ufahari na usomi?

Hata katika mazingira yasiyohitaji kizungu, bado watu watajing'ang'aniza kuongea kizungu hata kama hawakiwezi na tunajua kwa hakika kwamba hawakiwezi.

Hebu tuachane na hizi "You Know You know ofcozi zea zea" mingi mingi. Tunajiaibisha na kujidunisha.

Tunayo lugha adhimu ya Kiswahili. Tuitumie hiyo.

Nasubiri kuona hiyo kesho vile Bibi SASHA atakavyojitutumua na viingereza vyake uchwara.

Ashauriwe vyema. Maana shughuli za aina ile sio mahali pa kuonesha mbwembwe za kuzungumza kwa lafudhi bandia za kimalkia.

Tunahitaji kusikia "maswala" yakijadiliwa na kuzungumzwa. Hatuhitaji mikogo ya lafudhi bandia za Kizungu.
Waganda wengi hawajui kiswahili na ila wa Kenya nadhani ataongea kiswahili tu ndio watu wengi watamuelewa na kinapendeza hasa akitia vile vijineno kama kudemka.
 
Wacha manadharia yako bwana weye!

Kiswahili kilishakua na kuenea siku nyingi.

Na hapa wala sijasema lolote kuhusu kukuza Kiswahili.
Kiswahili kinakua bado hakijajitosheleza ndio maana imeashindikana kuwa lugha rasmi ya kufundishia sekondari na vyuo.
 
Back
Top Bottom