Kuna biashara moja hivi tulijaribu miezi ya mwanzoni hivi, tulitengeneza Faida ya 1mil+ ndani ya wiki tatu hivi, ila nisikufiche tulitumia ujuzi wa Ulimwengu wa roho, baadaye tukaona tutumie tu akili zetu na uzoefu maana wateja si tayari wapo, alooo.......walipungua na kuzidi kupungua, hapa tumeamua kutulia tu, tunalisoma soko halafu turudi tena kwenye ulimwengu wa roho.Ukipata nafasi hebu tupe hayo madini mkuu manake sasa hali imeshakua mbaya. Watu kila tukijaribu tunafumuliwa mi mbata unatoka unaona nyotanyota
N:B - Ulimwengu wa roho sio kupitia Shetani tu, hata kupitia njia za Mungu inawezekana.