Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Sema vingine uko sahihi.
Kariakoo paache tu, ukiwauliza wanakwambia nidhamu & kujituma

Sema njia za Mungu zinahitaji uvumilivu sana na pia uishi maisha matakatifu sana, usikwepe kodi na utoe zaka.

Hapo kwenye kutokwepa kodi ndo watu inawashinda .
Ewaah lazima uwe mwanamaombi kweli kweli, Imani ya 4G ila angalau kuliko upande wa pili.

Ninapochoka upande wa pili ni Ile Kila siku urenew dawa, so hapo unapata dawa mpya plus masharti mapya.
Usipoangalia unafikia level za kutoa sadaka za damu.. hahahah patamu hapo
 
Watu wamezungumzia issue ya jambo la kiroho..hii kitu inawork 100% sema wengi wetu tunakuwa wavivu au tunapuuzia kusali....hii sio uwongo au utani kama ni mtu wa maombi kabla hujaanza kuuza bidhaa zishike na ombea na liombee eneo hilo utaona matokeo yake. Nasisitiza its work kabisa
 
Bro kuna siri sana kwenye biashara pale, wanakwepa Kodi wale balaa plus na wengine wanatumia ulimwengu wa roho.

Hayo maneno wanayaongea tu, although kwenye kujituma, huwa wanatafuta supply nje ya nchi kama China kwa bei ndogo , alafu huku wanapiga bei ndefu kutokana na carry trade.
Mfano Kuna mtandao upo pale yaan mwekezaji kutoka nje ana back up kubwa ya viongozi wa serikali tena wale wakubwa kwenye issue za Kodi yy ni mwendo wa 'sahau', kama haitoshi ana viwanda kadhaaa sasa kwenye vile anazalisha mizigo mikubwa sana mwenyewe anauza, pia ana wafanyabiashara wa Kati wengi anawazalishia mizigo ya kutosha wanauza anawapa gawio na venye Kodi ni 'sahau' ila hao watu wakikushauri sasa

Mm nlijaribu tena sio direct kiasi hicho 🤔🤔🤔walichonifanya task force mpaka Leo naitwa Mpaji Mungu
 
Ewaah lazma uwe mwanamaombi kweli kweli, Imani ya 4G ila angalau kuliko upande wa pili

Ninapochoka upande wa pili ni Ile Kila siku urenew dawa, so hapo unapata dawa mpya plus masharti mapya.
Usipoangalia unafikia level za kutoa sadaka za damu.. hahahah patamu hapo

Upande wa pili jau sana. Yeah maokoto yanaweza flow ila sasa ndo sacrifice kama hizo. Yaani kwa Mungu inabidi uwe na juhudi ya kuomba kuliko hata unavyofanya biashara na imani ya kuamini kuwa imefanyika, sio Imani ya mpaka uone.
 
Mfano Kuna mtandao upo pale yaan mwekezaji kutoka nje ana back up kubwa ya viongozi wa serikali tena wale wakubwa kwenye issue za Kodi yy ni mwendo wa 'sahau', kama haitoshi ana viwanda kadhaaa sasa kwenye vile anazalisha mizigo mikubwa sana mwenyewe anauza, pia ana wafanyabiashara wa Kati wengi anawazalishia mizigo ya kutosha wanauza anawapa gawio na venye Kodi ni 'sahau' ila hao watu wakikushauri sasa

Mm nlijaribu tena sio direct kiasi hicho 🤔🤔🤔walichonifanya task force mpaka Leo naitwa Mpaji Mungu

Hata mimi nimesikia hizo ishu, angalau umeyathibitisha.
Watu wanadhani mambo ni simple, Ili kuwa tajiri mkubwa inahitaji uwe mafia.
 
Acha kabisa mkuu. Nimechoma milioni 80 kwenye dhahabu. Imeniacha mbendembende. Daah...! Bahati mbaya napoteza hela na umri ndio umeenda 40+.

Nimegundua ndio maana wakinga wakishika biashara moja ya duka ni hiyo hiyo hawabadiriki.

Hivi najitafuta kwa upya. Duka nililipukutisha kuingiza kwenye dhahabu. Hivi ndio napambania kulirudishia. Bidhaa sina japo biashara ipo. Hapa ili nirudi sawa natakiwa angalau milioni 40 kwa uchache 20 mpya niitupie humo.

Ila unajua nini? Lazima niyarudie madini yanipe hela.
 
Ulimwengu wa roho kuna sehemu mbili, kwa Shetani au kwa Mungu.
Wote wana kanuni zao kwenye biashara unayotaka kufanya, ili watoe urahisi wa kufanikiwa. Usione pale mfano wale wa Dar Kkoo watu wanapiga business, asilimia kubwa wamejiungamanisha kwenye ulimwengu wa roho, nimewahi sikia kwa Mhindi mmoja ana mgahawa maarufu sana, huwa anatamka maneno fulani kabla ya kufanya chochote asubuhi. Na anauza balaa, Wala hakukaa sijui miaka miwili.

Watu wana mbinu mkuu, na hawatazisema labda uwe na ukaribu nao sana.
Mtu hawezi kupa mbinu zake kudadadeq hilo alipo we utasikia omba Mungu tu
 
Mkuu watu humu wananibishia sana.
Alafu unakuta hawajawahi jaribu kufanya .
Mafanikio siyo masihara kuna mambo mazito sana, kuna watu wapo tu furaha yao ni kuona umeshindwa yeye hata akikushindwa anaenda kuomba msaada kwa mchawi mwenzake yaani watu wanakukalia kikao kabisa cha kukaanga, Hapo ndiyo huna Mungu kisawasa ndiyo kwisha habari yako.
 
".....kuanzia bar, stationary, usafirishaji, kilimo, ufugaji nk na zote hakuna hata moja iliyofanikiwa walau hata kurudisha mtaji!..."

Hizo biashara hazilipi kivile hasa kama uliweka watu. I bet stationary ulienda kwa mkumbo baada ya kuangalizia. Inahitaji location sahihi sana, wateja wawepo sio wakupitie au wakufuate. Hiyo sio online business kwamba mtu akiona nguo nzuri ataifuata from Mbezi to Tabata.

Usafirishaji ukute ulinunua bodaboda nyingi kama kichaa wakati wewe sio mkorofi na strict, au ulinunua gari la abiria. Ulisafirisha nini hasa.

Kilimo. Hapa ukute ulilima kilimo cha uti wa mgongo ukapinda mgongo. Kilimo ni biashara, ni hesabu, ni utaalamu. Na hakitaki mtaji mdogo kama ni kibiashara, labda kama unafanya kilimo cha kubeti.

Ufugaji haurudishi hela haraka kama unavyotaka, na hauna hela kubwa kivile kama una mtaji kidogo.

Bar sijui wanaendeshaje naona wanaleta matako makubwa na wanayabadili baada ya muda kidogo.

Hapa nahisi una matatizo makuu mawili. Kuwekeza kwenye biashara common kwa Mtanzania ila hazina return nzuri kwa mtaji mdogo, zile biashara za kupatia hela ya kula. Na kukimbia biashara kabla hujaizoea.
 
Back
Top Bottom