Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Mimi sikubishii mkuu, najua biashara zina mambo mengi ndio maana nataka tushauriane hapa ili angalau hata kama hatutatoboa, basi tusaidie wengine wasiendelee kuchoma mitaji bure..

Bro naona wengi wameshauri mambo mazuri tu kama location, juhudi, kufanya utafiti wa biashara unayotaka kufanya, na pia nidhamu ya pesa, inabidi uwe mbahili, narudia tena mbahili kama unaanza.

Kubusu ulimwengu wa roho the choice is yours ila upande wa Mungu, inahitaji usali sana na utoe asilimia kumi za mtaji alafu ukisali kwa Imani then ukipata faida utoe tena 10% ya ile kwa Mungu, 90% ya kwako alafu utakuja kuniambia.

Sali Baba yetu wa Mbinguni kwa Mkristo then omba kwa nia njema, ila sasa usifanye uovu, hata demu usimtamani.
 
Nilichojifunza,
Ili utoke kwa haraka lazima uwe na mentor au mtu mzoefu ambaye atakuwa tayari kukuonyesha njia na kukupa siri za game. Asiye na wivu.

Ila kama unataka ukomae mwenye uwe mvumilivu sana.
Mimi niliwahi kupuuza ushauri wa mentor. Nikajikuta natumia 700K nikaambulia 120K. Kosa ni dogo tu la kuleta ujuaji kwa kupuuzia ushauri wa Mentor. Nilikuwa nalima. Ila hilo zao formula yake nilipuuzia kakitu kadogo sana. Ula yeye alifanya akatumia 400K akapata 2M.
 
Yani unakuta mtu anafanya biashara nne ndani ya mwaka mmoja 😆🤣🤣 Sasa utapataje experience,unatakiwa kukaza tako axiee ukiona huoni njia hapo ndipo ilipo njia Sasa kwenye biashara unatakiwa kujikana Sasa wkt mwingine unakuta mfanyakazi kaajiriwa kaanzisha biashara,kachukua mkopo na alikuwa mtu wa Bata Sasa biashara hata haijaanza kumpa matunda,anaanza kuinywea pombe Tena 🤣😆,ukiamua kuingia kwenye biashara inakubidi uachana na anasa zote,unakuwa umezaliwa upya pambana mpaka isimame
 
Mkuu hatukimbii kwa kupenda, unalazimika kutoka nduki! We imagine mimi kuna wakati nilikua na mgahawa, asubuhi mnanunua kila kitu kwa 200,000 ikifika jioni kufunga mahesabu unakuta kila kitu kimeisha na mmepata 150,000. Hapo una vijana kama wanne wanasubiria ujira na kesho kunatakiwa hela ya sokoni kufuata mahitaji! Kwanini usivizie watu wakiondoka unakunja majiko yako unatia mfukoni na kutoka nduki kali...???😄😄
Walikuwa hawakupigi shoti kweli?
 
Naelewa hiyo situation. Mimi mwenyewe mkimbiaji mzuri wa biashara ila ili usikimbie biashara inabidi ujue sana mchezo wake ulivyo kabla hujaingia, usubiri kupata real experience uko.
Usiende na assumption kwamba kuna hela wakati hujui utaipataje. Usiende na assumption kwamba mzigo utatoka, mauzo yatakuwepo. Nenda na kutafuta profit sio kuonekana uko busy.

Mfano kwenye mgahawa umetumia kwa hesabu za haraka umetumia:
1kg mchele 2300
¼ nyama 2250
Viungo 1000
Mafuta 700
Misc. 250
Gas 1000
Jumla 7500.
Hapo ukiuza kama mtoa msaada unauza sahani tano @ 2000 unapata 10,000.

Gross profit ni 2500 yani hapa umeuza kama mpuuzi bado hujalipa vibarua. Sasa how comes unatumia 200,000 unapata 150,000?

Biashara ya wazi kabisa hii, ulijiuliza ukajua kwanini au uliamua ukimbie kama kawaida yako? Mimi biashara niliyokimbia naweza nikaiandikia kitabu kwanini niliacha, maelezo kibao. Na najua kwanini wanaoifanya hawawezi toboa, na sikukutana na yeyote aliyetoboa.
 
Waambie hao wanafikiri biashara inataka ubishoo [emoji23][emoji23][emoji23]
Wanavyoishi kipindi cha mvua ndio wakinga siku zote tunaishi hivyo
Aisee tulijifunza in a hard way. Yaani umepata faida eti unataka ule party, uende club au bar, ukahonge alafu biashara changa, yaani hapo hata Mungu aliyekusaidia anakuweka pembeni unless kama mtu yuko upande wa pili.
 
Sema baadae nilikuja kutulia nikagundua kuna makosa ya kiufundi nilifanya. Tatizo unakuja kugundua hayo wakati umeshachoma mtaji na huna hela tena so inakua haisaidii sana..
Andika business plan , alafu kopa.
Sema hakikisha unasimamia Hesabu wewe, ukiwaachia wafanyakazi utaliwa shoti, wale wasiguse pesa ndo maana wafanyakazi wengi wa serikalini biashara zinawashinda.
 
Aisee tulijifunza in a hard way. Yaani umepata faida eti unataka ule party, uende club au bar, ukahonge alafu biashara changa, yaani hapo hata Mungu aliyekusaidia anakuweka pembeni unless kama mtu yuko upande wa pili.

Akijaza mzigo akaanza kupata wateja mauzo kwenye droo yanasoma tayari anajibadilisha jina Papaa, Tajiri, Mutu ya watu, Don na mengine ya ujiko mengi.
Anaacha kuongeza mzigo na kutafuta mrija wa pesa zaidi anarukia skirt [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Na sisi wanawake wa kukuonyesha pesa zinavyotumiwa tunawasubiri na mawig yetu km Joti full kuwindana
 
Bro naona wengi wameshauri mambo mazuri tu kama location, juhudi, kufanya utafiti wa biashara unayotaka kufanya, na pia nidhamu ya pesa, inabidi uwe mbahili, narudia tena mbahili kama unaanza.

Kubusu ulimwengu wa roho the choice is yours ila upande wa Mungu, inahitaji usali sana na utoe asilimia kumi za mtaji alafu ukisali kwa Imani then ukipata faida utoe tena 10% ya ile kwa Mungu, 90% ya kwako alafu utakuja kuniambia.

Sali Baba yetu wa Mbinguni kwa Mkristo then omba kwa nia njema, ila sasa usifanye uovu, hata demu usimtamani.
Umeanza vizuri hapo mwisho ndio umeharibu 😀
 
Back
Top Bottom