Ulichukua hatua gani baada ya kugundua umebambikwa mimba/ mtoto?

Ulichukua hatua gani baada ya kugundua umebambikwa mimba/ mtoto?

Pole kwa kulea mimba hewa. Mimi mwenzako nilikuwa matawi ya juu zaidi. Nilimhamishia yule mwanaharamu kwenye makazi yangu, nikalea mimba na mtoto akazaliwa, nikalea. Alas, kufikia kama miezi mitatu, nikagusia mambo ya kwenye kupima DNA. Nikajibiwa ''unataka kumpima mwanangu amekuwa nyama ya kununua dukani?''. Huyooo akatimka mwenyewe bila kutimuliwa na mpaka sasa sijui aliko.
Hahahaa jamaa umenifurahisha
 
Huwa sisahau aibu niliyoipata Mimi Kwa ndugu zangu na marafiki zangu .
Nilibambikiziwa mimba nikalea mimba hadi kujifungua,miezi miwili baada ya kujifungua nikashangaa mbona siombwi hela kama mwanzo ilihali Sasa hivi mtoto na mama wanahitaji pesa nyingi!!?!siku kuja kumuuliza anasema mwenye mimba alikataa mwanzo Sasa kakubali kwahiyo Sina changu.
Irene popote ulipo sijakusahau mshenzi wewe ulinisababishia aibu na fedheha,nilikonda,nikakosa ufanisi kazini, nilipewa warning letter baadae wakakataa kurenew mkataba wangu,nilikosa kazi.
Niliskia uko marangu mtoni unateseka mbwa weweee.[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
😅😅😅😅😅😅pole sana.
 
Huyu dem amesoma udom??
 
Mimi nilitulia...nikatuma elfu 15,mpaka niliposkia ameenda hospitali..nikajipeleka kisirisiri..nikamkuta mwanaume mwenzangu amenitangulia..nukajua ndiye Muhusika..maana mtoto alitoka wa kipemba wakati Mimi mwenyewe gunia la mkaa..
Mkuu tuseme kwa mfano angekuwa na yeye wa gunia la mkaa mpaka hapo ungekuwa ushapigwa
 
Nilihudumia Ujauzito hadi akajifungua , baada ya kunilazimisha kwake nimuoe yeye kama mke wa pili (mke mdogo) kugonga mwamba, akaniambia mtoto si wa kwangu, nikamjibu poa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe ujuba nao unasaidia sana. Ungekubali tu ingekula kwako.

Aisee hawa wanawake kumbe wametubebesha sana.

Unajua Mungu akusaidie uzae mtoto mnayefanana. Nje ya hapo unabaki na mashaka kweli kweli
 
Yaan yule mshenzi alisababisha mivurugano kwenye kichwa changu ilifikia hatua hadi kila nikisalimiwa na mtu natamani nimsimulie yanayonisibu.
Mapensiiiii mabayaaaaaaaa[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
😅😅😅inaonekana ilikuwa unampenda sana. Ila yeye hakuwa anakupenda.
 
Binafsi sijawahi kubambikwa mimba wala mtoto, ila nimewahi kuhudumia mimba hewa! Nilikuwa nampenda sana naye alikuwa anajua nampenda, siku ya siku akaniambia hazioni siku zake, tulipoenda kupima ikaonekana kweli ana mimba.

Siku hiyo nilikuwa na furaha isiyo kifani, kuanzia hapo nikaanza kumhudumia kama mke wangu. Mara kinatakiwa hiki, mara kile, nikaja kushtuka baada ya miezi mitatu na nusu ukawa ndiyo mwisho wa mahusiano yetu baada ya kumpa kipondo kitakatifu.

Kinachoniuma mpaka kesho ni zile gharama za hospital/clinic, maana alikuwa akiniambia mimba inatishia kutoka kwahiyo anatakiwa kuhudhuria clinic kila wiki.

Wewe je, ulibambikwa nini na ulichukua hatua gani baada ya kugundua umefanywa bwege?
Wakati niko chuo miaka hiyo nilikuwa na Mpenzi wa Uswazi.
Kiukweli alikuwa mzuri na alikuwa ananipa mapenzi motomoto.

Ilifika mahali akawa ananiletea pesa chuoni au chakula cha nyumbani kizuri.

Basi siku zikasonga na nilipanga nitamuoa nilimuona ana tabia njema na mchapa kazi.

Kwa kuwa nilikuwa bize na masomo ilipita kama miezi mitatu hatuonani ila tukiwasiliana mara kwa mara kwenye simu. Nilijua yuko na mishe za pesa kwani tulishaongea na kupanga mikakati ya kazi fulani mimi na yeye.

Basi ikawa anaanza kuja kunitembelea aisee alikuwa anang'aa pamba kali mtoto kiuno kinazidi kuchanika ndembe ndembe.

Nilimuuliza mwenzangu vipi michongo imekubali mbona maisha yako umebadilika akasena mambo si Haba Mr Rasterman na leo nimekuja nikuletee zawadi. Basi nikamkula siku hiyo.

Ikapita kama miezi miwili akaja nikanuona ana mimba Kubwa usawa wa miezi minne hivi.

Siku hiyo kavaa nguo za kubana ili nisione. Akaja room wakati nataka kupiga machangamsho nikaona tumbo la mimba kubwa. Ub....o ukanywea pale pale tukalala.

Nilimuuliza mbona una mimba akaniambia eti ni yangu nikamwambia sio kweli hiyo mimba ni kubwa na mimi tumeonana 2months ago.

Aliondoka hatukuonana tena hadi after 7yrs.

Yule aliyempa mimba hakumuoa ila hadi leo analipa ni mzuri tu yaani.

Ila ndio sitaki makombo mie.
 
Yaan yule mshenzi alisababisha mivurugano kwenye kichwa changu ilifikia hatua hadi kila nikisalimiwa na mtu natamani nimsimulie yanayonisibu.
Mapensiiiii mabayaaaaaaaa[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
😂😂😂Mapenz mabaya sana
 
Mkuu watu wanaenda na mkojo wa mja mzito akifika anapewa kikopo anaenda kumimina. Mpimaji yeye anajua mkojo ni wa aliyeweka
Sasa mkuu matokeo yakija lazima kutakuwa na utofauti wa miezi au wiki mfano umeenda kupima na mpenzi na huyo mpenzi wako kapeleka mkojo siyo wake kachukua wa mjamzito sasa majibu ya kutoka lazima utashtuka siku mliyokutana na jibu mtakalo pewa.
 
Sasa mkuu umelea mimba mpaka mwanamke kakifungua ukaishi nae, sasa hukuwajua ndugu zake na wazazi wake maana ni ngumu kuzaa na mwanamke halafu husijue ndugu zake
Nawajua. Waliwahi kuja mpaka nyumbani. Infacy tunaishi karibu tu. Ila baada ya hapo mwanamke alitimkia mjini. Nilisikia fununu kuwa alienda kwa huyo mwenye mimba, na huko hakukaa sana akamwachia mtoto, na kuondoka. Sasa hivi sijui aliko na ndugu zake wanaficha.
 
Kumbe ujuba nao unasaidia sana. Ungekubali tu ingekula kwako.

Aisee hawa wanawake kumbe wametubebesha sana.

Unajua Mungu akusaidie uzae mtoto mnayefanana. Nje ya hapo unabaki na mashaka kweli kweli
Ndioooooo
 
Pole kwa kulea mimba hewa. Mimi mwenzako nilikuwa matawi ya juu zaidi. Nilimhamishia yule mwanaharamu kwenye makazi yangu, nikalea mimba na mtoto akazaliwa, nikalea. Alas, kufikia kama miezi mitatu, nikagusia mambo ya kwenye kupima DNA. Nikajibiwa ''unataka kumpima mwanangu amekuwa nyama ya kununua dukani?''. Huyooo akatimka mwenyewe bila kutimuliwa na mpaka sasa sijui aliko.
Hahahahahah mie lazma nipime DNA siwezi kulea kibwege...Hawa wanawake wahuni sana sikuhizi.
 
Back
Top Bottom