Ulifanya kosa gani Shuleni Hadi kengele ya dharura ikagongwa watu wakaja mstarini kwa ajili yako?

Ulifanya kosa gani Shuleni Hadi kengele ya dharura ikagongwa watu wakaja mstarini kwa ajili yako?

Mi dingi yangu alikuwa boss wa waalimu wilaya fulani early 1990's na alikuwa kauzu sana,nilizingua nyumbani wakati nipo darasa la nne,akaja shuleni bila taarifa yoyote akagonga kengere mwenyewe, wanafunzi wote mstarini,mi sina hili wala lile nikajua mshua amekuja na mishe zake za Kazi, daah si nikaitwa mbele ya wanafunzi kama 400 hivi,dingi akaomba fimbo,nikala fimbo tano,baada ya hapo akasema makosa yangu na kutoa wosia pale,basi tukarudi darasani,nilichukia sana.

NB: Pamoja na hayo lakini Baba alikuwa mtu poa sana,ukipigana huko umepiga mtoto wa mtu,pale kwenye kesi atakuwa mkali sana ila mkitoka anakwambia safi,usikubali kuonewa kizembe,mengi aliyonihimiza yamekuwa msaada mkubwa sana kwenye maisha yangu.REST IN PEACE (25/11/1998)
Ushimen unatoa neno gani kwa baba yake Chukwu emeka ambaye kwa sasa ni mwenda zake.
 
Nilichora picha ya utupu ya madam wa English mwalimu wa Civics alinikamata nayo akaipeleka staff nikapewa adhabu ya kupalilia maua ya shule lakini baada ya kumaliza form four Kila mwalimu alikuwa ananisifia eti "...ila ulimpatia yule madam....".
Kuna mwalimu mmoja siku moja alikuwa ananipa story juu ya jinsi alivyokuwa anatumia picha ile ya madam kupigia punyeto😁😂🤣.

Nilijuvunia Sana.
 
Nilibambwa choo wa wasichana na mimi ni mvulana, O-Level hiyo, hiyo siku nilitoka shule matako yanawaka moto baada ya kula kipondo cha almost walimu wote.
Na suruali yangu ili Chanika matakoni hiyo siku, kufika nyumbani natoa maelezo yasiyo eleweka kwa mzazi, kesho yake akanirudisha shule kisago mara ya pili.
 
Jamani maisha ya shule ni safari ndefu sana nyie acheni tu.

Nakumbuka ndio nimeingia 4m.2 nikiwa shule # ya kisabato. Walikuja walimu wa field wakiume 2 na 4 wakike, baada ya kama wiki 3 kuna huyo madam wa field aliyepewa kutufundisha geography. Huyu madam alikuwa na mwili wa kati wala sio mnene english figure hivi😋na maji ya kunde.

Nilitokea kumwelewa sana na maranyingi alikuwa akija class kunipa Hi!! Kabla ya masomo kuanza, sikumoja nilitoka home na kibarua changu nimekichoronga usiku kucha misitari kama yote mixer kumsifia na kumwomba out siku ya weekend.

Hii barua nilidhamiria kuifikisha kwake kwa kuiweka kwenye daftari langu la geography maana aliagiza test alizotoa tukusanye asubuhi, nilifanya hivyo na muda ulipofika monitor akakusanya daftari zote na kuzipeleka staff. Amakweli siku ya nyani kufa miti huteleza.

Nilishangaa baada ya kama lisaa kupita dada mmoja wa 4m4 akija kwa mbwe mbwe na kuomba mwalimu aliyekuwa anafundisha darasani amruhusu kuingia ameagizwa na mwalimu wa nithamu.
Na nilivyokuwa napenda kukaa madawati ya mbele kabisa. Since that day niliacha kabisa kukaa mbele ya darasa nikajisajili back benchers.

Nilipo lisikia jina langu limetamkwa...nilihisi kama jiwe kubwa( fatuma ) limedumbukia ndani ya tumbo!!
Kwanza sikuamini kama nimesikia vizuri, nilijikuta natizama nyuma huko labda kuna mtu anasimama..." Mbona unashangaa au hujasikia unaitwa ofisini". Ni hii sauti ya mwalimu ndio ilinitoa kwenye hali niliyo kuwa nayo.

Nilikuta staff imechangamka sio poa maana walimu kama wa 3 ndio walikuwa wamepelea, kwanza niseme confidence ndio kitu nilijliwa nilipo tupa jicho kwenye meza ya huyo madam HAKUEPO ila madaftari yalikuepo na mwalimu wa somo aliye kuwa akitufundisha ndio alikuwa amekalia kiti. Kumbe madam alikuwa hajawasili na alikuwa mgonjwa hivyo majukumu aliyashika Mr. geography.........
 
Kunakipindi nilikua nasoma shule ya msingi kulikua kuna mama anapika mihogo nje ya shule, kwakua shule ilikua na uzio kwahyo kwenda kununua ni kipengele.

Mimi nlikua na fahamika vzur kwa kutoboa fensi, kwahyo nilikua napewa hela na darasa zima naenda kuwaletea mihogo wakati wa mapumziko..

Siku moja nikaingia tamaa ile hela ya wanafunzi nikanunulia saa kali ya mkononi..

Nkarudi darasani huku ninalia wanauliza mihogo iko wapi nkawaambia mwalimu Apolo amenishika nikiwa napita kwenye fensi akaniambia niile mihogo yote na fimbo za kutosha nimekula.

Sasa ubaya nikwamba kuna mtoto wa mwalimu akakazirika akaenda ofisini akamwambia mamake anaomba hela maana mwalimu apolo amemwambia Ayos ale mihogo yetu.

Kumbe mwalimu apolo akuwepo siku hiyo yaani nilikuja kuchukuliwa msobemsobe yani sita sahau milele lile tukio.. mpaka leo stakagi kabisa kuvaa saa naichukia yani nkama nina aleji na saa
 
Ulipata mpaka trauma..

Ilikuwa form six tunasoma kwa ajili ya mock examinations.

Sasa kwa bahati mbaya tulikuwa watatu darasani , ilivyogonga kengele ya assemble hatukuenda maana wiki inayofuata ilikua mtihani.

Sasa wakati tupo class tunajisomea, miongoni mwetu alikuwepo adui namba moja wa mkuu wa shule, huyu alikuwa akimkosoa sana yule mzee.

Kama zali vile , mkuu huyu hapa.

Akatuambia tuende ofisini kujieleza kwanini muda wa assemble sisi tunajisomea.

Baada ya kumpa maelezo, akagonga tena kengele akatuweka mbele ya shule nzima.

Akasema hawa wakati nyie mpo assemble wao wanasoma, huyu bwana kwakuwa yeye alikuwa ananikosoa sana siwezi muacha nampa adhabu sitamsamehe.

Tulifanya mock huku tunachimba visiki, yule jamaa alituponza kisa kumkosoa mkuu wa shule kila mara.

Ila baada ya hapo matokeo ya necta tukapasua.

Kwa sasa mmoja ana PHD yake.
 
Hapa ni katika level zote 3 za elimu shule ya Msingi, sekondari na Kidato cha 5 na cha 6.

Mimi nakumbuka niliwahi kamatwa na simu kengele ikagongwa nikaipasua kwa mawe hadharani..
Mi nilimwekea mwalim kioo . Si unajua gauni ukiwwka kioo pecha inaeleke chini hivyo kila kitu ndani unakiona ...
Na choo cha walim nilitoboaga tena tundu
Sema hili la tundu hadi mzazi aliitwa😭
 
Mimi sijawahi kugongewa kengele.... Ila sasa nikiwa fom six..... kama kawaida asubuhi ni assembly.......

Mkuu akaja siku hiyo kasalimia vizuri tuu,

Ghafla kataja jina langu, shule nzima ikaduwaa maake nilivyo innocent hawaamini kutajwa na mkuu Huku list nyingine ikiwa ni ya wanafunzi wale wababe,

Nafika pale ofisini waalimu wote vipi umefanya nini , mimi hata sijui

badae wanafunzi wenzangu vipi kulikoni, ukaitwa Kuna nn , wengine wakidai maybe mimi Nina ukaribu na mkuu labda snitch lakini sikujua sababu hasa mpk leo.....
 
Hapa ni katika level zote 3 za elimu shule ya Msingi, sekondari na Kidato cha 5 na cha 6.

Mimi nakumbuka niliwahi kamatwa na simu kengele ikagongwa nikaipasua kwa mawe hadharani..
Nilipenda sana vitabu, nikiingia library sitoki, sasa mmoja aliiba vitabu bahati mbaya mimi ndiye nilionekana ikapigwa kengele,, kilichofuata Siri yangu, ila kusoma raha jamani.
 
Back
Top Bottom