Ulifikiria nini kujibatiza username unayoitumia JamiiForums

Ulifikiria nini kujibatiza username unayoitumia JamiiForums

Scorfield ndio jembe and that makes tBug a kijembe and, mahone a kijembee,and me a kijembeee
 
kijembeee said:
......Kijembe kidogo kama cha kupalilia maharagwe? Au ni kijembe (msuto) kwa kumaanisha kumsema mtu? Au jembe (mtu Shupavu) ?
 
Wakuu,kwanza nikiri wazi
kwamba JF siyo tu mtandao wa kupashana habari na kuongeza uwezo wa
kujenga hoja kinzani lakini pia,ni moja kati ya sehemu inayonipa raha
hata ninapokuwa na stress kutokana na shughuli za kila siku.
Leo napenda tuchangie mada hii iliyonifanya nicheke baada ya
kutathmini baadhi ya majina ambayo watu wanayatumia hapa JF mfano
Mbogo,Popobawa,Gandagumu,Mtimkavu,Mcameroon,kitimoto n.k
Binafsi nilipojibatiza jina la Gandagumu ilikuwa ni kuendeleza
kumbukumbu ya itikadi ya U-hardcore niliyokuwa nayo sekondari miaka
mingi iliyopita.Niliamini katika kujikaza na kupambana kuyafanya yale
ambayo wengi wanashindwa kuanzia lifestyles,mtazamo,maamuzi,mahusiano na
weledi...! |Je,wewe ulifikiria nini ulipojibatiza jina unalolitumia
hapa JF?

Kuchasoni Kuchawangu ni msemo wa kisukuma na kinyamwezi.Maana yake ni Kuona aibu ni kufa mapema.jamaa na mke wake waliishi maisha ya taabu sana mjini.Wakaona michango mingi inayotolewa pindi mtu akifiwa.Wakaona hii ni dili,wakaamua kujifanya kufa kwa zamu ili wapate fedha ya kujikimu.Wakakubaliana itakapofikia kipindi cha kuupeleka mwili wa marehemu kaburini mwenza aliyehai atasema fufuka kisha maiti kukohoa na watu kuahirisha mpango wa kuzika.Waombolezaji wakiondoka maisha yanaendelea.Wakaanza na mume jamaa kajifanya amekufa mke katandika mkeka nje kaangusha kilio watu wakaja daftali la michango likatembea,kaburi likachimbwa na maiti ikatolewa kwenda malaloni.Mke kaanza FUFUKA MUME WANGU,FUFUKA MUME WANGU jamaa kakohoa zoezi la kuzika likashindikana.wakatawanyika jamaa wakala pesa zikaisha.Zamu ikabidi mke naye afe,taratibu zikawa ni zilezile watu wakaja michango ikakusanywa kaburi likachimbwa maiti ikatatolewa.Mume kaanza FUFUKA MKE WANGU,FUFUKA MKE WANGU mke akajibu NAONA AIBU! kwa sauti ya chini kabisa ambayo haikuweza kusikika.Maiti ikafika kaburini mke anaona aibu.Mume alipozidi sana wazee wakaamua kumshikilia wakimwambia ajikaze kazi ya Mungu haina makosa.Mke akazikwa angali hai kwa kuona aibu.Ndiyo maana ya KUCHASONI KUCHAWANGU kuona aibu ni kufa mapema.
 
Mimi ni kaka mkubwa kwenye familia, means first born, so am BIGBRO.
 
sky, kwa rang yangu niipendayo blue, haf for three first letters of my name..i love sky_haf
 
Last edited by a moderator:
Hiyo yako ni kali kaka mm Dine halitofautiani sana na jina langu halisi
 
The last don ni mshabiki mkubwa wa novel za Mario Puzo the author of The Godfather,nilijiunga jamiiforums wakati nasoma novel ya huyu Mzee iitwayo The last don.....
 
Kuchasoni Kuchawangu said:
...Mkuu nakushukuru sana kwa simulizi kali,fupi na inayobeba maudhui ya kweli haswa kwa upande wa kina dada na mama zetu wanaodhani aibu ni heshima.Natamani ungefanyika mchakato wa kuzikusanya na kuhariri hadithi nzuri toka asili ya makabila yetu kwani zinaburudisha kuliko hata bia.
 
Mi napenda sana LOLIPOP nddo maana nikajibatiza LOLI
 
The name "Mkiliman" comes from here:

Mkili- ni kijijini kwetu. I just love to be MKILIMAN.
 
Napenda sana music pande zangu za Mbeya lazima nijichanganye sana mitaa flan hasa weekend.
{THK DJAYZZ}
 
kule kwetu kinshasasa mukuruu maana mutu mukubwa enye mapesa mingi ka wawonaga papa shelii vile
 
mukuruu said:
Comment ca va papaa Mukuruu! Mutu yenye kupenda watu wadogo na kuwaona wanyonge kama ******! (Mkuu Mkuruu una cheti cha uraia lakini)
 
Kuchasoni Kuchawangu said:
...Mkuu nakushukuru sana kwa simulizi kali,fupi na inayobeba
maudhui ya kweli haswa kwa upande wa kina dada na mama zetu wanaodhani
aibu ni heshima.Natamani ungefanyika mchakato wa kuzikusanya na kuhariri
hadithi nzuri toka asili ya makabila yetu kwani zinaburudisha kuliko
hata bia.
Ni kweli mkuu,zipo hadithi nzuri za asili zetu zenye mafundisho.
 
Back
Top Bottom