Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Nilipata mtoto wangu wa kwanza nikiwa na miaka 17, kiukwrli nilikuwa na hisia mchanganyiko.
-Nilikua naogopa yet sijui naogopa nini
-Nilikuwa nina aibu as nilijiona dah, mi ndo naonekana muhuni mtaani
-Nilikuwa na majuto as niliona nimeaibisha walezi wangu as baba na mama walikwishafariki
-Nilikuwa nina hasira as nilijua sitasoma tena
-Nilikuwa ninahamu ya kumuona mwanangu as nilihisi atakuwa kama kamdoli
-Nilikuwa ninawivu as nilijua boyfrien wangu angeniacha
Yani tu kwa ujumla nilikuwa na sintofahamu kibao.
Binti yangu sasa ana miaka 26.
Leo hii ukiniuliza nitakwambia yafuatayo
KUTUNZA MIMBA NA KUKUBALI KUWA MAMA KWA UMRI ULE, ILIKUWA NI UAMUZI THE BEST NILIWAHI KUFANYA KWENYE MAISHA YAN
Vijna wawe makini, unaweza jikuta unamtongoza mama mkwe
 
Habari wakuu, najua wengine humu tayari mmesha oa au ni wazazi tayari.

Ningependa mtupe uzoefu wenu, kuwa uli jisikia vipi kwa Mara ya kwanza baada ya kugundua wewe ni mzazi mtarajiwa.

Kuna kipi Cha kuji funza zaidi , ili kuwa mzazi bora?
1. Changamoto mlizo kumbana nazo, kabla na baada ya kuwa mzazi. (Hii kwa wanaume na Wanawake, ita pendeza mki elezea kwa kina zaidi).

2. Una ushauri upi kwa vijana kuhusu suala hilo la kuwa mzazi.

3. Kwa mwanaume ni Mambo yapi ya kuzingatia zaidi, hasa Baada ya kupata taarifa hizo.

I mean no malice to nobody.
View attachment 2967184View attachment 2967185
Mmmh Intelligent businessman waenda kuwa baba nini jamani twambiee tuu šŸ˜…
 
View attachment 2967805
Nilichelewa kidogo ila nshatia guu šŸ™šŸæ.

āž”ļø My first and only daughter. Nilikuwa ndiyo nimeanza masomo ya juu nje ya nchi. Kitabu kinanipelekesha hatari mara vu bin vu eti SYB haki ya nani kumbe umeniacha na mimba. Kidogo masomo yanishinde!

Kwanza nilikuwa na wasiwasi sana kama kweli hiyo mimba ni yangu au nimebambikiwa. Nilikuwa bado kijana na bila experience yo yote na wanawake maana hata huyo baby mama hakuwa mpenzi wangu kivile. Anyway bahati nzuri nilikuwa na full scholarship na kuanzia siku hiyo nilianza kudunduliza vijidola vichache kutoka kwenye stipend yangu ili angalau mtoto wangu aje azaliwe kwenye private hospital na apate mahitaji yote ya msingi katika siku zake za mwanzo. Baada ya kuongea na washikaji wakasema kama una uhakika mimba ni ya kwako, mbona usipambane mtoto wako aje azaliwe huku ili apate na uraia kabisa. Hii itamsaidia wakati wa shule na fursa zinginezo...

Aisee nilihangaika sana, pamoja na kupiga box la ziada mpaka kweli malaika huyo akaja akazaliwa huko ugenini. Bahati mbaya/nzuri mama yake ilibidi arudi Bongo kwenye ajira yake nzuri. Na maisha yakasonga japo baadaye kila kitu kilikuja kuparaganyika; na baby mama akaolewa na majamaa yenye pesa zao huko. Na kuanzia siku hiyo nikawa proud single dad.

Kusema kweli I stopped my life ili kuhakikisha kuwa binti huyu anasoma na kupata kila kitu alichohitaji. I lived frugally (I still do) na kwa nidhamu sana ili angalau kila mwezi niweze kuweka vijidola kadhaa kwenye kiakaunti chake cha mambo ya shule na cha kuanzia maisha yake akifikisha miaka 18. Na niliweza! Mpaka ninapoandika hapa binti yupo anapambana kuwa pediatric cardiologist (daktari bingwa wa moyo kwa watoto) tena katika mojawapo ya chuo kikuu bora kabisa hapa duniani huku akiwa na full scholarship!šŸ™šŸæ

1. You haven't real loved anyone mpaka utakapobeba kitoto kichanga kisichojiweza na kinachokutegemea kwa kila kitu. That's the epitome of true love.

2. I was scared to death lakini kilichonisadia wakati ule ni kuwa karibu sana na Mungu. Hata nilipokichukua kibinti hiki kikiwa na miaka miwili tu na kwenda kukilea mwenyewe nilijua kuwa kila kitu kitakuwa sawa na kwamba I was going to be a great dad!

3. Kuwa responsible parent inataka kujitoa sana ikibidi kuahirisha baadhi ya mambo yako na kutanguliza maslahi ya wanao ili wao wasipitie magumu kama wewe uliyopitia. Ukishapata mtoto, it is no longer about you labda kama we ni mbinafsi usiyejali. Na definition yangu ya kufeli maisha ni pale unapojikuta wanao wanapitia magumu yale yale uliyopitia wewe baba yao!. Kama wazazi tunatakiwa angalau kuwaandalia wanetu maisha mema (elimu bora, viassets...) hata kama sisi wenyewe si matajiri wa kupigiwa mfano.

4. Ukijenga urafiki (wenye mipaka) na mwanao basi unakuwa umemaliza. Huyu binti ni rafiki yangu sana na tunaongea karibu kila kitu. Hata hekaheka zake na vibaharia vyake huko mi ndiye mshauri wake mkuu. Bichwa huwa linanivimba balaa akiniambia "I wish one day I will find a man like you. You are a good man dad. Thank you for everything!". Kwangu mimi haya ni mafanikio makubwa sana!

View attachment 2967799

5. Muache mtoto afuate ndoto zake. Huyu tangu utoto wake anapenda sana watoto. Miaka na miaka kanisani yupo kwenye infant ministry. Yeye alikuwa ndiye mwangalizi mkuu wa vitoto vidogo vinavyoachwa na wazazi wao wanapokwenda kwenye ibada kuu. Ndiyo maana hata career yake imeangukia huko huko kwenye kusaidia watoto. Mtoto akifanya kitu akipendacho anakuwa na passion sana na anafurahia anachokifanya...and this is priceless!

āž”ļøāž”ļøāž”ļø Vijana. Hakuna mimba ya bahati mbaya. Kama hauko tayari kuwa baba usiuze mechi hata iweje. Kuwa baba ni jukumu takatifu mno na ogopa sana kuleta kiumbe cha Mungu hapa duniani kama unajua hauko tayari kubeba jukumu hilo takatifu. Na hakuna mwanaume anayedharaulika hapa duniani kama yule anayezalisha tu na kisha kukimbia huku nyuma akiacha mateso ya usingo maza na watoto wasio na upendo wa baba wala male role models katika maisha yao (āž”ļø Girly men!). Kwangu mimi dhambi hiyo haisameheki; na mwanaume wa aina hii (deadbeat) hana thamani yo yote hapa duniani! šŸš®šŸš¶šŸæā€ā™‚ļøšŸš¶šŸæā€ā™‚ļøšŸš¶šŸæā€ā™‚ļø
Hongera sana Mkuu
 
Nilitambua sasa nimeleta kiumbe kipya duniani maisha yake ni wajibu wangu kuyatengeneza na kumwandalia kesho yake .
Ukipata taarifa umempa binti ujauzito , hakuna sababu ya kuuliza uliza ni yangu ama ni yake kama uliiloweka,wewe fungua account weka pesa ya mtoto na mama yake .
kumbe unaakili ila unajitoaga ufahamu tušŸ˜†šŸ˜†,ila hongera kwa kuwa baba bora
 
Back
Top Bottom