Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Wakuu,

Disclaimer🫢 Hapa hatuongelei pesa madafu

Kuna mtu alisema ameenda kwa rafiki yake akakuta wana pump ya mafuta kwao🤣🤣🤣🤣

Yaani mambo za kwenda sheli si habari zao. Wanamaliza tuu hapo nyumbani

Hata mimi ningeshtuka kwa kweli 😀

Wewe ni nini uliona kwa Watu ukajua pesa ipo?
Wachagga kwao Christmas migombani.....
Kuna familia kadhaa wanapaki private jet zao KIA....halafu haoo kimya kimya migombani.
Sasa humo migombani humo...ngumu kuelezea ukaeleweka kwa lugha ya kawaida.....
 
Wakuu,

Disclaimer🫢 Hapa hatuongelei pesa madafu

Kuna mtu alisema ameenda kwa rafiki yake akakuta wana pump ya mafuta kwao🤣🤣🤣🤣

Yaani mambo za kwenda sheli si habari zao. Wanamaliza tuu hapo nyumbani

Hata mimi ningeshtuka kwa kweli 😀

Wewe ni nini uliona kwa Watu ukajua pesa ipo?
Nishaendaga na mwanangu mmoja kwao siku zile za free shule za boarding. Ukiachana na mjengo mkali ndani nilikuta kaunta kama ya bar aisee ina ma vinywaji ya ulaya utasema yale masebule ya kwenye muvi za kinaijeria. Iyo ilikua 2011 na ilikua mara yangu ya kwanza kuona kaunta ya bar ndani , mafanicha meupe peee!! Aisee kuna watu wanaishi.
 
Balaa Sana mlangoni mnaweka ndoo za maji masufuria na sahani vikombe in case mwizi akijaribu kufungua mlango vipige kelele kuwa amsha.

Ndio ivyo HITACHI, PHILIPIS nao waka take over
Hakika mchina kafanya mapinduzi makubwa Sana kwenye Electronics appellant.
☺️☺️
Philips alikuwa muingereza anachuana na wajapan. Baada ya kuja Hitachi na Sony Bravia kusumbua mwishoni mwishoni kuanzia 2007 ndo mkorea akaingilia soko kwa Samsung na LG electronics. Baada ya mkorea ndio kaja mchina sasa kwa bei rahisi kupitia Singsung na Rising
 
Wakuu,

Disclaimer🫢 Hapa hatuongelei pesa madafu

Kuna mtu alisema ameenda kwa rafiki yake akakuta wana pump ya mafuta kwao🤣🤣🤣🤣

Yaani mambo za kwenda sheli si habari zao. Wanamaliza tuu hapo nyumbani

Hata mimi ningeshtuka kwa kweli 😀

Wewe ni nini uliona kwa Watu ukajua pesa ipo?
Yaani jamaa wanakaa Petrol Stesheni-Sheli?
 
Nilikua naendesha gari ya mizigo nikapata kazi kupeleka mavyuma fulani hivi mbweni, sikwenda na mtu ila nilipewa namba ya simu nikaambiwa ukifika maeneo fulani piga simu kuna mtu atakufuata.

Mie huyoooo nilipofika eneo la tukio nikapiga simu full kufoka nimeshafika muda mrefu hapa, dk 0 ikaja V8 nyeusi tiiii. Ikaja kuni block kwa pembeni, jamaa akashusha kioo akasema nifuate.

Asee kila kona tunayokunja ni mijengo ya maana, mitaa mizuriii halafu pako kimyaaa, tukafika mpaka nje ya mjengo mmoja geti kuubwa, lile lango likafunguliwa kwa rimoti tukazama ndani.

Asee ile kuingia ndani nikawa nashangaa shangaa tu hata sielewi, lilikua bonge la jumba, swimming za maana halafu juu ya paa kuna parking ya helicopter, mataa ya barabarani yapo ndani.

Kuna jamaa nahisi aliona shauku yangu, akaniambia "zunguka zunguka uone nyumba ya rais wako ili uende ukasimulie na wenzio" nilizunguka kidogo tu ila maeneo mengi yalikua na makatazo kupita.(nyumba ilikua haijaisha ila ilikua inatisha aseee)

Nb; ninaposema rais, anaweza akawa wa tff, wa yanga au hata wa chuo.
Baaaasi tushapajua si kule unapita njia bara bara ipo juu juu kidogo🤣🤣
 
Enzi hizo nipo form six tumetoka shule jumamosi kufanya test tukaenda nyumbani kwa rafiki yetu huyo..

Dah..tumefika tu tunakuta maagizo kwa house girl wao eti mama yake ameacha laki 100,000... jamaa akachukue chakula cha paka da nilishtuka sana.. nikamwambia jamaa yaani paka wenu hawa wanabudget nzuri hivyo kuliko watanzania wengi sana kweli maisha hatufanani.... akacheka tu.

Paka wenyewe wawili 2 nikiwaangalia kama wa mitaani tu..wamejilaza kwenye makochi
Hiyo ni mwaka 2014..

Kifupi jamaa hata chuo akwenda hakusubili matokea akasepa zake state hadi leo yupo huko alisoma chuo hukohuko ameoa hukohuko kifupi maisha kwenu yakiwa kwenye hali nzuri kuna uwezekana mkubwa sana watoto pia wakaishi maisha mazuri tu hata wakikuwa.

Yule jamaa napiga nae story hadi leo namkumbusha wale paka anasema walikufa.yeye anawaita na majina kabisa.
😂😂Hiyo bajeti kwanza nimekasirika ghafla. Sema unaweza ukahisi ni kufuru lakini ni vile hatuna maisha wallah, umaskini mbaya sana
 
Back
Top Bottom