Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Kisa changu ni cha tofauti kidogo miaka ya 90 kama sikosei tulienda likizo kwa baba yetu mkubwa huko Daslamu tukitokea kijijini ,baba mkubwa yeye alikua njema sana na alikua anakaa mitaa ya Oysterbay kule karibu na uwanja wa farasi pale,

Basi siku hiyo isiyo na jina tukapikiwa sausage( soseji) kwa mara ya kwanza nilizifurahia sanaaa ,nikaona nimuulize broh ,Broh akanipanga hizi ni karoti zinachemshwa na hamira ndio zinakua hivi,

Broh hakujua kuwa mwenzake nimeliweka ,likizo ilipoisha kurudi bush huyoo hadi jikoni nikakusanya mikaroti yangu nianze kutoa soseji🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 khah nyie acheni
 
Hakunaga tajiria anafanya ujinga wa aina hio 😂!

Ungeniambia festive season anawapa budget ya $200k waende wakainjoy maulaya huko ningekubaliana na hilo. Ila sio kila mwezi!
Bakheresa mwenyewe tu utajiri wake tunaambiwa haufiki hata $2b.... Halafu leo hii eti awe anatenga $200k Kila mwezi anawapa watoto wake waende wakaitupe?, huo uwendowazimu hata watoto wake wenyewe tu hawawezi kuukubalia.

Hapo kwenye bold ndio familia nyingi za kitajiri zinafanya hivyo huwa wanaandaa budget ya maana kwa ajili ya kula Bata mahala popote duniani inapofika holiday season.

Afterall Hawa wanaoongelewa hapa ni upper middle class tu, yaani ni watu wenye hela za kuwakidhi mahitaji yao na familia zao tu basi labda na kufanya anasa za hapa na pale.

Mfano Sasa hivi nikiuliza kati ya hao matajiri(kwa mujibu wa hizi story hapa) walioongelewa hapa kwenye huu Uzi ni wangapi ambao angalau wamejenga hata barabara za mitaa yao kwa kiwango Cha Rami na wakaweka street lights, utakuta hakuna hata mmoja..

Au ni wangapi ambao angalau wamejenga hata vyuo vya ufundi kwenye mikoa yao waliotoka hili kuleta impact kwenye sector ya elimu kama alivyofanya bwana Patrice Motsepe huko kwao south Africa? obvious jibu ni hakuna.

Dar Kuna shida kubwa sana ya maji, najua watu wengi sana wanachimba visima...je, Kuna tajiri hata mmoja ambaye kwa gharama zake mwenyewe amevuta maji Moja kwa Moja kutoka mto ruvu ambapo maji hayo yananufaisha mamia ya watu..? Jibu ni hakuna

Hivi ndivyo vitu ambavyo matajiri wa kweli wanafanya na sio Hawa upper middle class citizens wanaoongelewa hapa.
 
Mzee wangu alitokea familia ya kimaskini Sana.
Babu alikuaga na ngo'mbe wengi Sanaa
Kimiujiza miujiza miaka ya 60's watoto wa Babu kwa miaka tofauti tofauti walikua wanafaulu darasa la saba na kuchaguliwa shule za SERIKALI

Walisomaga zamani na wakabahatika kupata kazi nzurii serikalini na wote wamekua watumishi mpaka Kustaafu kwao utumishi serikalini.

Kwenye tumbo la mama tupo wa 5 hakuna hata mtoto mmoja ambae Hana degree wa mwisho ndio kamaliza hapo Udsm mwaka huu

NB.
Kuna familia ukizaliwa unakua mwenye bahati na chance kubwa ya kuwa na option mbali mbali za kutimiza ndoto/goals E.t.c
Hilo suala la familia nzima kuwa na degree kitu cha kawaida sana mzee au ulilenga kusema nini?
 
Kinachoamua sio unachokikuta nyumbani ni assets, net worth na vibunda vilivyo akaunti

Vitu vya nyumbani haviamui sana ikiwa mtu au familia iko vizuri kiuchumi

Kwa mfano ukimpima Mo kwa vitu alivyo navyo nyumbani unaweza kusema yuko sawa na lower second fulani tu pale Mbweni au Mbezi Beach
 
Dah kuna huyo mwanetu enzi tunasoma sekondari 2006 mwamba alikuwa mtu wa mbeya somebody Mwangoka nadhani, alifiwa na mzee wake ilikuwa ajali ya gari au alianguka na pikipiki akakanyagwa pande za Mwenge mataa.

Kituko ni ule msiba picha linaanza tunafika msibani wameweka mziki full buster zinapigwa zile kwaya za Mbeya.

Msiba haukusafirishwa kama wiki hivi anangojewa kaka wa marehemu kutoka Russia.

Wafiwa wote full matisheti ya picha za marehemu.

Mie na masela wangu tulikuwa tunatoka shule tunaenda kumfariji mwanetu msibani, msosi ni mwendo wa kujipakulia minyama kwenye bufee.

Yaani nyuso za wafiwa hakuna hata mwenye huzuni.

Upande wa kina baba ni watu smatsmat tu wamekaa kwa mafungu wanakunywa na kula taratibu taratibu.

Pale kulikuwa na hela sio mchezo..
 
Nilishtuka tu kuona GETINI kuna Mlinzi wa K.K SECURITY nikahisi labda tu ni viwalinzi vimejivalia kujikosha.

Jioni Shift ikibadilika KK SECURITY gari inamleta Mlinzi wa kupokea shift akiwa na MTUTU begani.

Nikajua Humu ndani Sio Pa kawaida kuna La ziada nisilolijua.
 
Tumekula usiku Vyakula mboga sio 7 ile ni Mboga 20 bufeee la kwenye maharusi nikalikuta pale. NIKAHISI kwasababu sisi wageni tunakaribishwa.

Day 2 same applies

Day 3 same applies

Day 4 asubuhi nikawa na hamu sana na Kunywa chai na kiporo, Nikamuomba dada kiporo..

Akaninyima akaniambia ntaumwa TUMBO kimeenda kumwagwa...

Nikaona enheee hapa Nimefika, Likizo irefushwe.
 
Tuko ndani ya uwanja unaenda kule na kule, unakula upepo tuu..

Nikataka kwenda kuzurura zangu, nafika getini MLINZI kanikazia.

Kaniambia siruhusiwi kutoka kwa miguu, Akapgiwa simu DREVA nikaambiwa niende nae kapewa funguo kuingia kwa gari DEREVA ananiuliza nataka kwenda wapi?

Nmamwambia mi sijui nilitaka kwenda kutembea tu, Basi jamaa akaichukua hiyo ndo fursa akaenda mishe zake namimi ndani ya gari, akipgiwa simu kuulizwa tulipo anasema ananitembeza.

Wajomba IST zilikua hazijaingia enzi hiyo tuko na PRADO SAFARI lile limebenjuka flani ndo hiloo tunazurura nalo. LINAMKONGA kwa mbeleee.

Oyaaa wajombaa hiyo ndo life ya watu.
 
Hilo suala la familia nzima kuwa na degree kitu cha kawaida sana mzee au ulilenga kusema nini?
Sio kitu Cha kawaida maana Kuna familia nyingi hazijaweza ku support watoto wao kwa kiwango icho Tena kwa pesa yao wenyewe.

Kwako inaweza kua sawa na rahisi Ila kwenye familia nyingi sio rahisi watoto watano wote wasome na kufikia viwango vya juu kielimu.

Au ulitaka kusema Nini mkuu?!
 
Back
Top Bottom