shichandao
JF-Expert Member
- Sep 11, 2024
- 274
- 418
Yote hayo lakini marehemu hakufufuka. Mimi ni Christian ila napenda waislam hawana tabia ya kuchosha marehemu.Dah kuna huyo mwanetu enzi tunasoma sekondari 2006 mwamba alikuwa mtu wa mbeya somebody Mwangoka nadhani, alifiwa na mzee wake ilikuwa ajali ya gari au alianguka na pikipiki akakanyagwa pande za Mwenge mataa.
Kituko ni ule msiba picha linaanza tunafika msibani wameweka mziki full buster zinapigwa zile kwaya za Mbeya.
Msiba haukusafirishwa kama wiki hivi anangojewa kaka wa marehemu kutoka Russia.
Wafiwa wote full matisheti ya picha za marehemu.
Mie na masela wangu tulikuwa tunatoka shule tunaenda kumfariji mwanetu msibani, msosi ni mwendo wa kujipakulia minyama kwenye bufee.
Yaani nyuso za wafiwa hakuna hata mwenye huzuni.
Upande wa kina baba ni watu smatsmat tu wamekaa kwa mafungu wanakunywa na kula taratibu taratibu.
Pale kulikuwa na hela sio mchezo..