Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Hii kweli

Kuna nyumba hapo makonde mbezi beach walikuwa na budget ya mbwa kama 700,000 kila mwezi na anakula nyama kwa asilimia kubwa
Kuna siku brother angu mmoja yupo hapo Dodoma.
Akijaga dar zamani iyo tunapata shushu ya kuzunguka na lishangingi la ofsn kwake.

Jamaa tunaenda nae kununua mbwa akalipia mbwa mmoja laki 9 iliniuma Sana jamaa kununua mbwa wawili kwa 1,800,000 cash

Mbwa kwa ajili ya kumsaidia kulinda mbuzi na mifugo yake hapo Dodoma aisee nilishangaa

Kuna species mbali mbali za mbwa wanauzwa kuanzia laki 7,8,9 na kuendelea..
 
Kuna wezi waliendaga kuvamia nyumba ya kibibi na jiwe fatuma.

Wakati wanaliset set bibi akaamka akawasikia mipango yoote,

Bibi alichofanya alienda akasimama nyuma ya mlango, wale jamaa wakaanza moja, mbili...... ile kufika tatu, bibi akaufungua ule mlango ghafra, jiwe likapita mazima bila kugusa mlango mpaka ndani kisha kwa haraka akaufunga.

Jamaa wakakosa means ya kuvunja mlango wakaanza kumuomba bibi awafungulie walau wachukue jiwe lao
Kweli hii ilitokeaga maeneo mbali mbali ni hatare sanaaa Sanaa 😊 mkuu.
 
Kwa wakati ule mlikuwa matajiri wakubwa sana
Yalikua Maisha ya kawaida Tena tukiishi low profile.
Ukipata wazazi walio bahatika kupata. Exposure ni kawaida.
Hata baadhi ya taasisi za serikali Mbona zilikuja na facilities Kama izo...


Lilikua ni life la kawaida Sana Mbona vitu Kama bomba la mvua, washing machine, Brenda za kutengeneza juice, mashine za kutengeneza ice cream, Tv,PASI za umeme,fridge, mashine ya kukamulia ufuta, e.tc
 
Miaka ya 60's mpaka early 2000 kilikuaga na wizi /uvamizi kuvunja mlango na ndio kisa Cha watu kuanza kuweka milango ya ma grill

Iko ivi wezi watakuja na jiwe kubwaa ambalo liliitwa FATUMA....Wezi watakua na mbeleko na wanaweza kuhesabu mpaka tatu na kulirusha jiwe uelekeo ulipo mlango then mlango utavunjika ndipo watapata nafasi ya kuingia ndani na kuwaibia Mali mbali mbali..

Wengine watakuja kuongezea zaidi..
Uko sahihi kabisa na mara nyingi wale jamaa huwezi kuamini ule mjiwe walikua wanausomea visomo kwa waganga wao wakibeba ni jepesi na wanakuja nalo ila likirushwa ni kama Myahudi karusha kitu kwa mzee Sinawali pale Gaza na nyie kubeba hamuwezi ila wao wenyewe safi safi
 
Uko sahihi kabisa na mara nyingi wale jamaa huwezi kuamini ule mjiwe walikua wanausomea visomo kwa waganga wao wakibeba ni jepesi na wanakuja nalo ila likirushwa ni kama Myahudi karusha kitu kwa mzee Sinawali pale Gaza na nyie kubeba hamuwezi ila wao wenyewe safi safi
😂😂🤣🤣
 
Baada ya kumaliza form IV nikapangiwa kwenda Minaki high school, mzee wangu akaona huyu kijana hajawahi kufika mji mkubwa kama Dar ikabidi ampigie mjomba wangu anipokee. Kiukweli Kwa zile harakati za mjomba akijaga vijijini anaonekana ana ukwasi lakini nilipofika kwake maeneo ya kimara kilichonionyesha hii family inapesa licha ya kuwa na bonge la jengo, ni garden aliyonayo. Unajua kimara enzi za nyuma ilikuwa inashida Sana ya maji lakini yeye alikuwa na garden ambayo Kila siku zinakuja boza tatu Kwa ajili ya kumwagilia na kipindi hicho boza moja ilikuwa 100,000 + 20,000 ya dereva kusubiri tumwagilie. Yaan Kwa siku 350,000 Ilikuwa inaimwagwa kwenye garden. Ila kilichonishangaza Kwa ukwasi alikuwa nao sijui kwann aliishia kimara
 
sio kweli. sisi wenyewe mzee alikua anaenda zambia hio 80s ilikua colgate na ndara zile subutu ukutwe nazo na serikal .gari alinunua Niva kwa rafiki yake mzungu alikua kigoma UN ndio yule mzungu alikua anaruf kwao akamuuzia friji.heater pressure cooker.even us we had those things
Sijaelewa.
Au ndo vitu vyenye majina ya kitajiri ambavyo mimi siyajui
🥲
 
LAzima uone chai watu wanaishi mzee baba..

Nishashuhudia MBWA wananunuliwa Nyama STEKI tena za mbavu kikahesabiwa kibunda nyama ikabebwa.

Yote kisa mmbwa ni mzazi katoka kuzaaa,na ile ni siku zote.

Hamna chai mzeee ni pesa watu hawana pakupeleka
HA!HA!HA

Sahihi mkuu , Tumeziwekea limitation akili zetu kufikiria hayo sababu Tumejiwekea ukomo wa kipato ..

Lakini ukifanya hayo make sure watu wa msingi wote umewasaidia...
 
Wakuu,

Disclaimer🫢 Hapa hatuongelei pesa madafu

Kuna mtu alisema ameenda kwa rafiki yake akakuta wana pump ya mafuta kwao🤣🤣🤣🤣

Yaani mambo za kwenda sheli si habari zao. Wanamaliza tuu hapo nyumbani

Hata mimi ningeshtuka kwa kweli 😀

Wewe ni nini uliona kwa Watu ukajua pesa ipo?

Wakuu,

Disclaimer🫢 Hapa hatuongelei pesa madafu

Kuna mtu alisema ameenda kwa rafiki yake akakuta wana pump ya mafuta kwao🤣🤣🤣🤣

Yaani mambo za kwenda sheli si habari zao. Wanamaliza tuu hapo nyumbani

Hata mimi ningeshtuka kwa kweli 😀

Wewe ni nini uliona kwa Watu ukajua pesa ipo?
Shamba boy ana gari yake aina ya double cabin
 
Mimi nilikwenda Kwa Mtu mmoja mkubwa sana Jeshini wakati huo,akiwa ni swahiba wa Mzee wangu.
Wakati wa kula nilijionea Vituko.
Kulikuwa na Samaki wa Mchuzi na mkavu,Nyama ya Ng'ombe Kavu na ya mchuzi,kuku pia hivyo hivyo.
Mboga za Majani zaidi ya tatu.
Mezani Kuna wali,ugali na pilau!
Juisi ndio majagi!
Uvumilivu ukanishinda nikauliza mnakula hivi hivi Kila siku!?
Wakaniambia ndio tunavyokula,sisi Kila kitu tunaletewa na Jeshi!
Nikajisemea moyoni,kweli aliyenacho ataongezewa.
 
Back
Top Bottom