Ulikutana vipi na mwenza wako? Je, mazingira yanafungamana na tabia ya mtu?

Ulikutana vipi na mwenza wako? Je, mazingira yanafungamana na tabia ya mtu?

Tupeane uzoefu , ulikutana wapi na mwenza wako kwa mara ya kwanza, inasemekana mazingira unayokutana na mtu huwa yanatoa mustakabali wa penzi lenu na yanaeleza tabia ya mtu , kama ni mtaani , uswazi au ushuwani , Bar au kwenye nyumba ya ibada n.k je ni kweli mazingira huwa yanafungamana na tabia ya mtu
Mi nlimuona tu nikasema moyoni huyu ndo mke wangu lazima nimwoe and tukapotezana hata salam hatukusalimiana nikaja kutafuta namba yake, nlikuwa domo zege nikamwambia direct nakupenda akanitoa balu, nikakomaaa baadae akatiki sms niloandikiwa sitaisahau hadi nakufa, nanukuu " unashtskiwa kwa kuuteka moyo wangu hadi nakuwa nakuwaza wewe tu kila mda" siku hiyo hata chakula hakikulika, tuliongea hadi asubuhi maana ilikuwa ile tigo unaongea dakika 1 ya kwanza zingine zote bure,date ya na mimba juu, tukaachana alivojifungua nikaanza kuishi naye
 
Back
Top Bottom