Ulikuwa wapi kipindi ndege ya JWTZ inaanguka wakati wa kupokea wanajeshi waliotoka Uganda?

Ulikuwa wapi kipindi ndege ya JWTZ inaanguka wakati wa kupokea wanajeshi waliotoka Uganda?

Mimi nilikuwepo live siku hiyo hapo hapo uwanja wa Taifa .nilishuhudia zoezi likianza kwa kupitisha vifaeu na mizinga iliyotekwa toka Uganda na hiyo ilikuwa baada ya Gwaride la majeshi na chipukizi kumalizika.
Ndipo zikafuatia Ndege na hatimae hiyo ajali kutokea.Mwalimu alipewa taarifa rasmi ya ajali na Brigedia General Mayunga pale jukwaani.
Namuona mzee hapo anatazama kwa huzuni
 
Kwa ishara hii unamaanisha nilichoandika ni uongo. Wakati huo, mwaka 1980, nilikuwa mwaka wa tatu UDSM na nilihudhuria kwenye hayo maonesho ya kijeshi pale uwanjani. Kwa umri nilio nao siwezi kuandika mambo ya upuuzi katika JF. Naomba unitake radhi kama kweli wewe ni muungwana.
 
Ilikuaje Rubani wa ndege akaiangushia nje ya uwanja wakati ilikua inaangukia ndani ya uwanja.. Hii story ipo pale SKUA . Nataka nijue ni ile ile au kila sehemu Kuna Script yake
Kwa maelezo tuliyopewa, baada ya rubani kuona ndege inaelekea kuanguka maeneo ya ndani ya Uwanja, aliikwepesha kidogo ili kuepusha madhara ambayo yangeweza kutokea. Binafsi nilimpongeza Sana kwa kitendo chake cha ushujaa na kweli alikufa kishujaa.
 
Jeshi letu tukufu kumbe tushawahi angusha chopa🤨,sio kila siku Gaza tu,vipi Kuna manusura wowote walotoka hapo🤔🤔!!!
 
Nyerere alilengwa sana na machozi lakini akasimama imara kama kiongozi wa nchi na kusema maneno mchache tu kuwa mashujaa wetu waliorudi walikumbana sana na matukio kama hayo wakayashinda. Nadhani mahali ilipoangukia ndege hiyo palijengwa mnara ikiwa ni pembeni kidogo ya kambi ya Mgulani na chuo cha elemu cha Chang'ombe. Ndiyo gharama tuliyopata sana kwa kuamini ndege za mchina. ndege hiyo ilikuwa ni Shenyang J6.
 
Nilikuwa kizimkazi na girlfriend wangu ambaye leo ndio nanii wenu
 
Nyerere alilengwa sana na mchozi lakini akasimama imara kama kiongozi wa nchi na kusema maneno mchache tu tu kuwa mashujaa wetu waliorudi walikumbana sana na matukio kama hayo wakayashinda. Nadhani mahali ilipoangukia ndege hiyo palijengwa mnara ikiwa ni pembeni kidogo ya kambi ya Mgulani na chuo cha elemu cha Chang'ombe. Ndiyo gharama tuliyopata sana kwa kuamini ndege za mchina. ndege hiyo ilikuwa ni Shenyang J6.
Angekuwa Bi Tozo angesema Gen Z ndio wamesababisha
 
..Rubani wa ndege alipaswa kutambuliwa.

..Wananchi walitakiwa wajue wasifu wa rubani huyo.

..Mashujaa wa kweli hawapewi heshima na nchi yetu.
 
Enzi za kula asali na maziwa hizo,
mshua kwenye politiki hakuwemo kabsaa
 
Back
Top Bottom