Namuona mzee hapo anatazama kwa huzuniMimi nilikuwepo live siku hiyo hapo hapo uwanja wa Taifa .nilishuhudia zoezi likianza kwa kupitisha vifaeu na mizinga iliyotekwa toka Uganda na hiyo ilikuwa baada ya Gwaride la majeshi na chipukizi kumalizika.
Ndipo zikafuatia Ndege na hatimae hiyo ajali kutokea.Mwalimu alipewa taarifa rasmi ya ajali na Brigedia General Mayunga pale jukwaani.
Kwa ishara hii unamaanisha nilichoandika ni uongo. Wakati huo, mwaka 1980, nilikuwa mwaka wa tatu UDSM na nilihudhuria kwenye hayo maonesho ya kijeshi pale uwanjani. Kwa umri nilio nao siwezi kuandika mambo ya upuuzi katika JF. Naomba unitake radhi kama kweli wewe ni muungwana.
Kwa maelezo tuliyopewa, baada ya rubani kuona ndege inaelekea kuanguka maeneo ya ndani ya Uwanja, aliikwepesha kidogo ili kuepusha madhara ambayo yangeweza kutokea. Binafsi nilimpongeza Sana kwa kitendo chake cha ushujaa na kweli alikufa kishujaa.Ilikuaje Rubani wa ndege akaiangushia nje ya uwanja wakati ilikua inaangukia ndani ya uwanja.. Hii story ipo pale SKUA . Nataka nijue ni ile ile au kila sehemu Kuna Script yake
Mimi huyu huyuWe mkuu
Nilikuwa viduduIlikuwa tarehe Mosi September 1980 wakati ndege ya Jeshi la wananchi wa Tanzania ilipoanguka kwenye eneo la uwanja wa Taifa katika sherehe za kuwapokea wanajeshi wetu wakirejea kutoka Uganda kumng'oa nduli Idi Amin Dada.
View attachment 3276670
Je ulikuwa wapi wakati huo?
Angekuwa Bi Tozo angesema Gen Z ndio wamesababishaNyerere alilengwa sana na mchozi lakini akasimama imara kama kiongozi wa nchi na kusema maneno mchache tu tu kuwa mashujaa wetu waliorudi walikumbana sana na matukio kama hayo wakayashinda. Nadhani mahali ilipoangukia ndege hiyo palijengwa mnara ikiwa ni pembeni kidogo ya kambi ya Mgulani na chuo cha elemu cha Chang'ombe. Ndiyo gharama tuliyopata sana kwa kuamini ndege za mchina. ndege hiyo ilikuwa ni Shenyang J6.
Nilikuwa Upanga.Ilikuwa tarehe Mosi September 1980 wakati ndege ya Jeshi la wananchi wa Tanzania ilipoanguka kwenye eneo la uwanja wa Taifa katika sherehe za kuwapokea wanajeshi wetu wakirejea kutoka Uganda kumng'oa nduli Idi Amin Dada.
View attachment 3276670
Je ulikuwa wapi wakati huo?