Ulikuwa wapi wakati kifo cha Mwalimu Nyerere kimetangazwa?

Nilikuwa nimemaliza la saba na nikawa najishughulisha na biashara ya ndizi.....kuna brother mmoja mpangaji wetu alikuwa anazitoa kijijini huko na kuzileta hapo mjini; akawa ananipatia kidogo niuze ili nami nisikae hivihivi. siku ya habari ya msiba kulikuwa kuna mahafali yetu ya kumaliza la saba.............yakaghairishwa na hatukufanya tena!
 
Nilikuwa Dallas, Texas

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa na kingereza kibovu kama cha Meko ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Azaboy pale,siku hiyo wanafunzi tulitembea mpaka Uwanjani...Halafu pale getini tulikuwa na kipaumbele. Yaani ndio ilikuwa siku yangu ya kwanza kumuona Nyerere live na ya mwisho.R.I.P
 
Yule si alikua na hadhi ya kipekee hapa kwetu, walivyosimamisha masomo ilikua sawa...

Ila maisha yako kasi, Mkapa kaondoka kumekua tofauti, maisha yamebadilika.
Anyway, ni suala la mjadala zaidi, maana wao walimu walikuwa wanakuja shule kama kawa, sasa kwanini walikuwa hawafundishi? Angali hata hawakuwa kwenye msiba wa Nyerere?
 
Dubai
 
Duuh,hii huwa inanikumbusha mbali sana. Tukio hili la kifo cha Baba wa Taifa huendana na kumbukumbu ya Mimi kuachwa na demu wangu kipenzi.

Nakumbuka nilikua Mwaka wa kwanza SUA demu alikua Mwaka wa kwanza UDSM. Dalili za kuachwa zilikuwepo, Weekend ya tarehe 8 nilikua nimeenda ili kujua hatma ya penzi letu. Nilifikia kwa mshkaji wangu Hall 9 na demu alikua akiishi hall 3.

Usiku huo niliofika hakuwepo chumbani, kesho yake tarehe 9 jmosi nilienda nikakutana na room mate wake akaniambia "shem, huyu mwenzako Alisha hama chumba anaishi oyster Bay huwa anakuja asubuhi na gari baadae ya vipindi anaondoka. Kwa hiyo kumpata hadi darasani wakati wa vipindi "
Nilipiga moyo konde nikaondoka kurudi kwa mshkaji wangu, siku yangu iliharibika kabisa.

Sikurudi Morogoro niliamua kubaki ili nijaribu kuonana nae jtatu. Nilianza kuhudhuria vipindi vyake vyote kuanzia jtatu hadi Nyerere alivyofariki ndo nikarudi.
Kwa hiyo RIP Nyerere Rip mapenzi
 
Oh!
Baba umekula chumvi, Heshima yako Mkuu.

Kwa umri wako saivi, hata mzee wangu bado sana!
 
Dah!
Zile picha za graduation zingekua ukumbusho wako leo
 
S
Story yako inasisimua!!

Alivyohama kwenye hall hizo na kuhamia ostabei hlf anakuja na gari asubh tayar alishapata mwingine..

Ila tumeumbwa kusahau.
 

Vp Ney siku hizi yukowapi mana ukimkumbusha lazima akumbuke..

Mkuu uzalendo utaanza kurudi kuanzia October 28,watu watarudsha mapenzi na nchi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…