Siku kama ya leo marehemu Ben alitangaza, saa nne asubuhi kuwa Mwalimu ametangulia. Tulikuwa darasani, radio ya mchoma chipsi pembeni ya darasa letu ndo ilitupasha habari, kipindi kile ukisikia wimbo wa Taifa unapigwa redioni, mnakuwa shupavu kutaka kujua nini kimetokea, hivyo tulivyosikia tu huo wimbo, wote kimyaaa kusikiliza.
Ila wengi tulioishi maeneo ya karibu na kwa mwalimu tulishajua mambo yameharibika kule kabla ya tarehe tajwa, barabara ya kwenda kwa mwalimu ilikarabatiwa, walianza kukarabati nyumbani kwake, magazeti nayo yakiripoti; "Kawawa arudi na siri nzito" akitoka kumuona mwalimu St Thomas, mara Mwalimu apumulia mashine kwa 100%, magazeti ya Alasiri na Dar Leo yakiripoti hivyo, mara mortuary ya Muhimbili inakarabatiwa. Yote hayo yalikuwa kati ya tarehe 1 na 10 mwezi wa 10.
Nilikuwa darasani