Oyaa! Salimia na hapa! [emoji41][emoji41]Shikamoo bro. Mi nilikua la 3. Njia nzima nilikua naangalia angani nikijua kwakua Baba wa Taifa amefariki wakoroni wanakuja any time. Yaani mawazo yangu Nyerere ni kama Anold Shwaziniga yaani yeye ndio kamanda mwenyewe.
Mamndenyi Nakupenda!Nilikuwa mbeya, nimeajiriwa serikalini.
Nilimlilia sana Mwalimu Nyerere.
Nilikumbuka elimu ya bure niliyopata, nililia sana.
Nilkmlilia Mwalimu Nyerere mpaka akanijia kwenye ndoto, ananionesha alivyozidiwa na madaktari walivhojitahidi kuushtua moyo lakini ikashindikana.
Aliniaga na akasema nimeondoka sitarudi tena acha kulia.
Mbali ya Mwalimu watu wengine wawili niliwahi agana nao mmojawao ni Marehemu Papa Yohana yule aliyewahi tembelea Tanzania,
Namshukuru Mungu kwa yale maono hayo makubwa hivyo.
Endelea kuPumzika vizuri huko Mbinguni Mwalimu Nyerere.
Amkia wakubwa zakosisi wengine baba yetu wa taifa ni mkapa maana tulizaliwa zama zake[emoji849][emoji849]
Mkuu ID zinaficha mambo mengi humu ndani.Walikuwa watoto, sahizi ndo wanauelewa huu uzi.
Jf vimejaa vitoto hadi kero. Siku zote nilijua kuna watu wazima humu kumbe ninabishana na watoto tu. Kila siku ni CDM kumbe wamezaliwa wakati inazaliwa.
Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Dah Aisee!Mimi nilikuwa mwanza nyumbani,baadae nilitoka kwenda kupata moja moto moja baridi huku nikiangalia taarifa ya habari,baadae taarifa maalumu iliingia,lkn alikuwepo jamaa mmoja mlevi alikuja akazima tv na kusema nyerere ni nini?!, mzoga huo wa nini sisi,siku hiyo nilishudia kile ambacho sipendi nikikumbuke lkn pia siwez kukisahau,yule mtu alipigwa mpk aliuwawa hivihivi kizembe kizembe,
Kwahiyo hii 14 tunapigwa kamba ?Siku kama ya leo marehemu Ben alitangaza, saa nne asubuhi kuwa Mwalimu ametangulia. Tulikuwa darasani, radio ya mchoma chipsi pembeni ya darasa letu ndo ilitupasha habari, kipindi kile ukisikia wimbo wa Taifa unapigwa redioni, mnakuwa shupavu kutaka kujua nini kimetokea, hivyo tulivyosikia tu huo wimbo, wote kimyaaa kusikiliza.
Ila wengi tulioishi maeneo ya karibu na kwa mwalimu tulishajua mambo yameharibika kule kabla ya tarehe tajwa, barabara ya kwenda kwa mwalimu ilikarabatiwa, walianza kukarabati nyumbani kwake, magazeti nayo yakiripoti; "Kawawa arudi na siri nzito" akitoka kumuona mwalimu St Thomas, mara Mwalimu apumulia mashine kwa 100%, magazeti ya Alasiri na Dar Leo yakiripoti hivyo, mara mortuary ya Muhimbili inakarabatiwa. Yote hayo yalikuwa kati ya tarehe 1 na 10 mwezi wa 10.
Nilikuwa darasani
Nikisema watu wataanza kusema niwape salamuWakuu Salaam:
Leo Oktoba 14 inatimia miaka 21 tangu muasisi wa Taifa hili atutoke duniani.
Wakati kifo chake kimetangazwa, binafsi mimi sikua na uwelewa kuhusu hilo hivyo sijukujua chochote kinachoendelea. Mwaka wa 2000+ ndiyo naelewa sasa.
Kuuliza uliza, kipindi kile tulikua Moshi wakati hiyo taarifa imetoka na ilitangazwa usiku.
Ulikuwa wapi ulipopata habari hizi?
1999 = Darasa la 4 = 10 to 12 yrs of ageNIlikuwa shule tena tuko darasan ndio tunapewa hizo habari mida ya saa 4 iv
Nilikuwa darasa la 4 wakati huwo
Msamvu Primary school