Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

Huna ulichodhibitisha zaidi ya kuja kuleta lugha chafu kwenye uzi wa mtu kumtuhumu kua ana "utajiri wa masharti ya kipumbavu" ...heshima kitu Cha Bure ...
Achana nae tuu yumo kwenye kundi la wasioifahamu dunia
 
TUNAENDELEA TULIPOISHIA.
Nb: Nafanya muendelezo huu sababu ya ahadi yangu kwenu ya kuwasimulia kisa hiki.
Basi baba na kaka walienda msibani mimi nilibaki nyumbani lakini nilipokuwa pale nafsi yangu iligoma kabisa kuhusu kubaki nyumbani, nilitaka niende siku ya pili yake ambapo ilikuwa ni siku ya kuzika yaani mazishi lakini nafsi ilifika muda ikanigomea nikawa nalia tuu pale chumbani.
Dada alisikia kwikwi zangu za kilio alikuja pale ndani na kuuliza mbona namzidishia huzuni?
Haujapita muda mrefu nakumbuka alikuja mtumishi wangu wa kijini mmoja na kukaa kwenye kona ya chumba karibu na boksi la vitabu dada alimuona mtumishi yule na alinambia nakupisha ufanye maongezi nahisi kuna ujumbe muhimu.
Baada ya dada kuondoka mle chumbani basi nikatoka nje kidogo nikashika udhu na kuvaa kanzu yangu na kusogea pale kwenye ile kona, alitoa salamu mwana wa jini yule nikamuitika nakunambia niache kulia na kusononeka kufanya hivi kunawaweka huzuni kubwa sana kama ni kutaka kwenda kwenye msiba basi yupo tayari twende mzee Ruhaby ameruhusu ila huko msibani kuna mengi ya ajabu ajabu hivyo nijiandae kukutana nayo .

Nilikuwa njia panda kukubali au kukataa lakini nafsi yangu bado ilikuwa inahitaji niende ila baada ya kusikia uwepo wa mambo ya ajabu ajabu akili yangu ilikuwa kwenye tafakuri kubwa nilishajua ni nini kinaweza kutokea huko .
Nakumbuka mtumishi wangu huyu alikuwa na kichupa kidogo mkononi kilikuwa na mafuta ya rangi nyekundu nilijuwa ni miski kumbe siyo, alinipuliza pumzi usoni na kisha akapaka yale mafuta, hayakuwa yakinukia sana kama nilivyohisi lakini nilihisi paji la uso wangu likivuta sana .
Mwili ulijaa joto sana na moyo ulianza kwenda mbio kiasi.
Nilionesha hali ya utofauti kidogo damu zilikuwa zikikimbia sana na nilipoangalia pale ukutani nilianza kuona picha za watu kule msibani.

Muda huo huo aliniamuru tutoke lakini nitakapokuwa natoka pale mlangoni nitangulize mguu wa kulia kwanza niseme Bismillah Rahman Rahiim kisha nimlaani shetani na kisha yeye nitamkuta barabarani karibu na muembe wa omary yule baba jirani yetu .
Nilimuita dada nikamwambia naenda msibani sasa hivi lakini naenda na yule mtumishi (Rauhiyah) . Nilifanya kama alivyonambia na kufika kwenye muembe nikamkuta kweli ila alinambia nitangulie mbele yeye atakuwa nyuma yake upande wa kulia . Nilifanya hivi na alikuwa akifata uelekeo wangu ila hakuwa karibu sana nami alikuwa umbali wa hatua kadhaa.

Tulivyofika pale msibani wasiwasi wangu mkubwa ilikuwa ni vipi itakuwa kama akitokea mtu mwenye jicho zuri lililofunguka akimuona mtumishi wangu Rauhiyah? lakini sikuwa na namna badala yake nilianza kusalimia watu kwa kuwapa mikono baadhi ya watu waliokuwa karibu.
Lakini nilipofika kumpa mkono mzee mmoja miaka kama 62 hivi Rauhiyah alishika mkono wangu na kukwepesha usigusane na wa yule mzee na Rauhiyah alikunja paji lake la uso sana ni kama alikuwa na hasira sana za ghafla.

Nikasogea kwa kijana mwingine wa miaka takribani 22 hivii lakini ghafla alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana na alianza kutokwa na jasho jingi na kabla ya kumpa salamu alisimama na kutoka nje ya jamvi, ghafla alivaa viatu vyake na kuondoka.
 
Basi

Basi nikaangaza macho kumtafuta baba na kaka walipokaa baada ya kuwaona niliwafata na kukaa nao pale , lakini nilipoangalia upande wa wanawake au wakina mama niliona wanawake kama Saba waliokuwa wamebeba ndoo za maji , walikuwa wakisombelea maji kwaajili ya matumizi ya kupikia pale msibani, sikuamini nilichokiona, nilirudia tena kuangalia ili kujiridhisha, nilimuona mmoja wa wale wakina mama amevaa kipochi mfano wa kile cha kuwekea simu lakini ndani hakukuwa na simu badala yake kulikuwa na uume wa mtoto mdogo, ulikuwa umeunguzwa ule uume na umekunjwa kwa mbele kama filimbi, na alikuwa na ushanga mwekundu na rangi nyeusi nao niliuona akili yangu ilivurugika kidogo lakini nilikuwa na utulivu mkubwa sana.
Niko palepale kwa wanawake walewale nikamuona mwingine amevaa pete ya silver ilikuwa na muundo wa ajabu kidogo lakini nikafahamu kuwa ni pete ya chuma ulete kiukweli nilijawa na hasira sana na nilimchukia ghafla sana yule mwanamke.

Watu walikuwa wakiendelea na maongezi lakini nami nilikuwa nikiendelea kujionea mambo ya ajabu ajabu kama ambavyo Rauhiyah alinambia kabla ya kufika msibani, muda wote huu Rauhiyah hakuwa mbali na mimi alikuwa upande wangu wa kulia na hakuna mtu aliyekuwa akimuona.

Ulifika muda wa chakula cha mchana wali na maharage nakumbuka, watu walituandalia chakula na tukawa tunakula lakini kuna bibi mmoja alikuwa akiniangalia kwa makini sana lakini sikuwa na wasiwasi hata hivyo, ila nilihisi kitu na kitu chenyewe ni kuwa tayari aligundua kuwa nawaona watu wabaya yaani wachawi au alikuwa akiona yale niliyokuwa nayo katika mambo mbalimbali ya ukaribu na viumbe.
Yule bibi alikuwa akipakulia watu chakula na kuwawekea mboga yaani maharage. Nakumbuka Rauhiyah alinambia najua wewe una haya sana lakini hebu jikaze sogea pale kwa yule mwanamke mtu mzima omba akuwekee chakula na mboga kisha kuna kitu utakiona kwake .

Basi nikamwambia baba ngoja nisogee niongeze chakula pale naona waandazi au waandaaji hawako karibu hivyo sina wa kumuagiza.
Nilisogea kwa yule bibi nikamwambia bibi naomba niwekee chakula na mboga ila mchuzi wa maharage uwe mwingi kidogo. Yule bibi aliniangalia usoni sana nami nikamkazia macho kwelikweli haswa eneo lake la mkono, hapo niliona kidonda kikubwa sana na kilikuwa kinawaka kama taa basi nikajua kabisa ni mtu wa vipi yule . Tulitazamana kwa makini sana na alikuwa na wasiwasi mkubwa sana yule bibi moja kwa moja nikajua ni yale mafuta aliyonipaka Rauhiyah

" Nakuwekea ila hii sahani yako nitatuma mtoto aje achukue muda sio mrefu, nataka niwekee chakula nami nile" yule bibi alinambia.
Muda huu Rauhiyah alinambia palepale sababu ya yule bibi kutaka sahani yangu , alinambia kuwa anahitaji rojo la maharage na mabaki ya chakula ili apate kusoma mambo kadhaa kupitia mkono wangu .
Nasema kweli nilipatwa na hasira na hapo busara ziliondoka nilijikuta nimempiga Kofi zito sana yule bibi hakuna mtu aliyejua sababu ni nini .
Nb: Itaendelea hii simulizi, na tuaangazia siku ya kuoshwa kwa mwili wa abushiri namna ambavyo watu walikuwa wakigombania maji ya maiti, sisimizi kujazana chumba cha maiti na wachawi kuadhirika baada ya mtumishi wa kiume kufika.
 
Ni
Muhimu kuelewa kisa kizima urefu bila kukielewa kisa haina faida , tuko pamoja na nimekuelewa
Nikajua umekimbia..nilisoma kisa chako chote tena usiku mzito..hatari sana ..kuna siku Moja ktk ndugu zangu alijisikia vibaya..basi kama huduma ya kwanza nikaagizwa nikatafute mizizi ya mkuyu nichemshe na nimpe mgonjwa ila chaajabu na yeye aliyeniagiza ambaye hakuwa mgonjwa akaitaka anywe..vipi hii imekaaje?
 
Nipo nitakaporudi safari nitakuwa na wakati mzuri.
Kuhusu huyu kutumia dawa hiyo naye ni wazi alifahamu umuhimu wa dawa hiyo mkuyu ni dawa muhimu sana ina kazi nyingi sana ni mti ambao nauweka katika kundi la miti muhimu sana
 
Fanya episode ziwe ndefu kiongozi maana unaishia patamu kichizi
 
Basi
Basi nikaangaza macho kumtafuta baba na kaka walipokaa baada ya kuwaona niliwafata na kukaa nao pale , lakini nilipoangalia upande wa wanawake au wakina mama niliona wanawake kama Saba waliokuwa wamebeba ndoo za maji , walikuwa wakisombelea maji kwaajili ya matumizi ya kupikia pale msibani, sikuamini nilichokiona, nilirudia tena kuangalia ili kujiridhisha, nilimuona mmoja wa wale wakina mama amevaa kipochi mfano wa kile cha kuwekea simu lakini ndani hakukuwa na simu badala yake kulikuwa na uume wa mtoto mdogo, ulikuwa umeunguzwa ule uume na umekunjwa kwa mbele kama filimbi, na alikuwa na ushanga mwekundu na rangi nyeusi nao niliuona akili yangu ilivurugika kidogo lakini nilikuwa na utulivu mkubwa sana.
Niko palepale kwa wanawake walewale nikamuona mwingine amevaa pete ya silver ilikuwa na muundo wa ajabu kidogo lakini nikafahamu kuwa ni pete ya chuma ulete kiukweli nilijawa na hasira sana na nilimchukia ghafla sana yule mwanamke.

Watu walikuwa wakiendelea na maongezi lakini nami nilikuwa nikiendelea kujionea mambo ya ajabu ajabu kama ambavyo Rauhiyah alinambia kabla ya kufika msibani, muda wote huu Rauhiyah hakuwa mbali na mimi alikuwa upande wangu wa kulia na hakuna mtu aliyekuwa akimuona.

Ulifika muda wa chakula cha mchana wali na maharage nakumbuka, watu walituandalia chakula na tukawa tunakula lakini kuna bibi mmoja alikuwa akiniangalia kwa makini sana lakini sikuwa na wasiwasi hata hivyo, ila nilihisi kitu na kitu chenyewe ni kuwa tayari aligundua kuwa nawaona watu wabaya yaani wachawi au alikuwa akiona yale niliyokuwa nayo katika mambo mbalimbali ya ukaribu na viumbe.
Yule bibi alikuwa akipakulia watu chakula na kuwawekea mboga yaani maharage. Nakumbuka Rauhiyah alinambia najua wewe una haya sana lakini hebu jikaze sogea pale kwa yule mwanamke mtu mzima omba akuwekee chakula na mboga kisha kuna kitu utakiona kwake .

Basi nikamwambia baba ngoja nisogee niongeze chakula pale naona waandazi au waandaaji hawako karibu hivyo sina wa kumuagiza.
Nilisogea kwa yule bibi nikamwambia bibi naomba niwekee chakula na mboga ila mchuzi wa maharage uwe mwingi kidogo. Yule bibi aliniangalia usoni sana nami nikamkazia macho kwelikweli haswa eneo lake la mkono, hapo niliona kidonda kikubwa sana na kilikuwa kinawaka kama taa basi nikajua kabisa ni mtu wa vipi yule . Tulitazamana kwa makini sana na alikuwa na wasiwasi mkubwa sana yule bibi moja kwa moja nikajua ni yale mafuta aliyonipaka Rauhiyah

" Nakuwekea ila hii sahani yako nitatuma mtoto aje achukue muda sio mrefu, nataka niwekee chakula nami nile" yule bibi alinambia.
Muda huu Rauhiyah alinambia palepale sababu ya yule bibi kutaka sahani yangu , alinambia kuwa anahitaji rojo la maharage na mabaki ya chakula ili apate kusoma mambo kadhaa kupitia mkono wangu .
Nasema kweli nilipatwa na hasira na hapo busara ziliondoka nilijikuta nimempiga Kofi zito sana yule bibi hakuna mtu aliyejua sababu ni nini .
Nb: Itaendelea hii simulizi, na tuaangazia siku ya kuoshwa kwa mwili wa abushiri namna ambavyo watu walikuwa wakigombania maji ya maiti, sisimizi kujazana chumba cha maiti na wachawi kuadhirika baada ya mtumishi wa kiume kufika.
Interesting..... Asee hii ni noma, dunia ina mambo mengi ya ajabu
 
Nipo nitakaporudi safari nitakuwa na wakati mzuri.
Kuhusu huyu kutumia dawa hiyo naye ni wazi alifahamu umuhimu wa dawa hiyo mkuyu ni dawa muhimu sana ina kazi nyingi sana ni mti ambao nauweka katika kundi la miti muhimu sana
Kama hutojali ..hii safari ndo ya Iran?
 
Back
Top Bottom