T
TUNAENDELEA.
Basi nikafanya ibada zangu nilipomaliza nikapumzika kwa usiku ule sikuwa na ugeni wa kiumbe chochote hivyo nililala mpaka ilipofikia alfajir niliamka kwaajili ya swala ya alfajir, nakumbuka baba alitangulia masjid hivyo nikawa natoka na kaka kwenda masjid lakini tukiwa njiani tukaskia matangazo mawili kwenye spika za masjid.
Tangazo moja lilikuwa ni kuhusu mazishi ya abushiri na jingine ni tangazo la msiba mpya wa mama fulani na hapo nikakumbuka kuhusu vurumai la dada Aisha na wale wachawi usiku .
Baada ya swala watu waliendelea na usomaji wa nyiradi mbalimbali lakini mimi nilirudi nyumbani.
Njia nzima nilipishana wamama na watu wengine wakiongelea yaliyojiri msibani kwa abushiri huku wakisema kuwa shangazi yake abushiri anahusika na kifo cha abushiri, sikufanikiwa kuwajua vizuri watu wale sababu ya kiza lakini nilihisi kuwa sio wakazi wa mtaa wetu ni wapita njia tuu .
Nilipokaribia nyumbani kabisa niliona kikundi cha watu waliokuwa wamesimama karibu na njia ya kwenda kwa yule mama ambae tangazo la kifo chake limetolewa.
" Yule kaingia pabaya kagusa pabaya pigo zito muda mrefu ni mtu mbaya mchawi yule wana kikundi chao ..... si unaona njia nzima ya kuingilia kwake kuna miburuzo na damu ukweli utajulikana tuu ..." Walizidi kuongea.
Ni kama walikuwa hawajaniona vizuri nilipowakaribia kabisa walinyamaza niliishia kutoa salamu na kuingia nyumbani, hapo nilimkuta dada Aisha na mama wakimalizia kuswali Alfajir na wao , moja kwa moja niliingia chumbani nikachukua chetezo na kuchoma ubani mashtaka kushtakia yale yaliyoendelea mchana kwa kina abushiri na kuhitaji msaada zaidi kwa mola .
Lakini nilikuwa na mawazo mengi sana nikataka kumuita mama niongee nae, mara nikataka kumuita dada Aisha ila nikawaza bora baba na kaka warudi kisha niongee nao wote .
Baba huwa anachelewa kurudi sababu usomaji nyiradi mbalimbali hivyo nikavuta subra ndefu kuwasubiri. Baada ya kurudi kwao tulijumuika pamoja kwenye dua ya asubuhi nyumbani na baada ya dua tuu nikamwambia dada awasimulie kilichojiri usiku .
Dada alieleza na mwisho nikawaambia kuhusu tangazo jipya la kifo cha yule mama na maneno yanayosemwa na watu mtaani.
Lakini bado nilikuwa nawaza nini kitatokea msibani kwa abushiri kama jana yake yalijiri mengi vile jee siku ya mazishi itakuwaje?
Hatimae muda wa kwenda msibani uliwadia na sheikh Yusuf alikuja pale nyumbani kumpitia swahiba yake ambae ni baba na safari ya kwenda msibani ilianza. Tulifika pale msibani macho yangu moja kwa moja yalilenga kwa kina mama yaani wanawake nikakumbuka hekaheka za jana yake .
Tukaenda kwenye jamvi la waombolezaji na kukaa pamoja na watu wengine tuliowakuta. Ratiba ikatangazwa na muda si mrefu wakachaguliwa watu kadhaa kwenda kuosha marehemu huku maandalizi ya sanda yakiendelea .
Baba yake abushiri alikuwa akilia sana ni mtoto wake wakiume pekee kwa wakati ule kuwa nae .
Muda wote huu Rihani na Rauhiyah sikuongozana nao lakini uwepo wao niliuhisi hawakuwa mbali nami. Mazungumzo ya watu yalikuwa habari za siku ya jana mchana kilichotokea pale msibani huku habari za msiba mpya zikitokota nazo , watu walikuwa wakiniangalia kwelikweli.
Pale tulipokuwa tumekaa kulikuwa na pipa la maji basi kukaja mtu kuchota maji ya kwenda kuoshea marehemu nikakumbuka kuhusu wadudu wa jana chumba cha marehemu.
Tukiwa pale hali ya hewa ilibadilika ghafla wingu zito jeusi lilitanda kukaanza mvua kubwa sana lakini cha ajabu ilikuwa ikinyesha ule mtaa wenye msiba tuu siwatanii akili yangu ilichoka ghafla tuu nilijuwa tayari mambo ya ajabu ajabu yameanza.
Watu walishangaa sana ni mvua ya vipi ile hivyo ikabidi zoezi la kuidhibiti lishike hatamu watu waweze kufanya mazishi.
Tukiwa pale pale watu waliokuwa kwenye kuosha maiti mmoja wao alitoka nje lakini alionekana kuwa na sintofahamu na kumuita baba mdogo na marehemu abushiri waliongea kwa siri lakini mambo yaliposhindikana wakasogea kwenye jamvi la masheikh na kumuita sheikh Yusuf hapo nikajua tayari kuna kilichoharibika.
Kilichokuwa kimejiri ni kwamba maiti alikuwa anatokwa na damu puani na mdimoni na mwili ni wamoto sana kwahiyo inakuwa vigumu kwao kumaliza zoezi la kuosha mwili papatikane sheikh wakwenda ndani .
Sheikh Yusuf alitakiwa kuongozana na wale watu , muda si mrefu nikasikia kila ishara kuwa Rihaan anakuja lakini alisema nami kwa sauti nakunambia kuwa mule ndani wale waoshaji kuna mmoja sio nzuri mzuri na anahitaji kuchukua maji ya maiti na vitu muhimu kwahiyo juu chini yule adhibitiwe.
Nikaingia kwenye hekaheka mpya kabisa nikawaza naanzia wapi na hapo nikamuita baba na kumwambia lakini kabla ya baba kufanya chochote sheikh yusuf alipokuwa anatoka nje aliongozana na mzee mmoja na mzee huyo alionekana kama aliyepandisha mashetani huku anasema "mimi sio mchawi ni vile hizo dua zenu sipatani nazo shangazi yake mwenyewe yule mtoto ndio ametuagiza..."
Ndani mambo yalibainika wakati sheikh Yusuf akifanya dua amani ipatikane alisoma kisomo cha kushurutisha majini ya wachawi kuwa dhalili na hapo yule mzee alianza kuropoka mengi sana hivyo ikabidi atolewe nje .
Ilikuwa ni aibu kubwa sana watu walimsikia mzee yule maneno yake .
Baada ya shughuli za uchimbaji kaburi na ushonaji sanda muda wa mazishi ulikaribia, hali ya taharuki na hekaheka za wachawi kutaka kuchukua vitu muhimu kwenye mwili wa marehemu zilionekana kudhibitiwa vikali sana na zoezi lao kushindikana hatimae abushiri alizikwa mazishi halali.
Nb: hiki ni kipengele muhimu katika simulizi hii yakweli kabisa na nafikiri mpaka hapa mmeona umuhimu wa kusomea dua maiti zenu , umuhimu wa kuwa makini mnapopata misiba ya ndugu na jamaa zenu kwani wachawi hujipenyeza humo kupata vitu vya kujiimarishia nguvu .
Kitambaa cha sanda iliyobaki, nywele za maiti, maji, unyevu unyevu kwenye mwili wake na vinginevyo jitahidi kuhakikisha vinabaki salama.
Nitawapatia kipengele chengine cha maisha yangu na kuamiliana na hawa viumbe mtajifunza kitu naamini.