Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

mkuu usemayo ni kweli kuwa mambo yote kuanzia ulimwengu wa roho..lakini wengi wetu ni watupu kabisa upande huo hatuna maarifa yoyote na darasa lako hili ndio utufungue macho sasa..tueleze code za ulimwengu wa roho ni zipi,je,unawezaje kuingia ulimwengu wa roho,ulinzi wa kiroho tunaupataje.? ni vipi mtu anakuwa imara kiroho au kuweza kupambana na wanaomchezea kiroho iwe wachawi au waganga.? je ni mambo gani yanaongeza au kukushusha kiroho.? je utaitambua vipi nguvu yako kiroho ni imara yenye nguvu au uko dhaifu kiroho.? je,mtu unaweza kuona linalokuhusu huko ulimwengu wa roho liwe lilifanywa zamani,sasa au hata lijalo unaweza kutumia njia gani kujua yanayokusibu kiroho hata kama umefanyiwa na watu wengine ili uweze kuyakwepa..na yapi yanatoa ulinzi mkubwa kiroho kiasi kwamba wanaokutafuta kiroho kwa ajili ubaya wakute kizingiti kwamba uko imara upande huo na huingiliki kizembe na mimi nitaweza kujua hila zao.? ni zipi code za kucheza na ulimwengu a roho.?
 
Maswali mazuri sana haya. Hata mie nina shauku ya kutaka kujua haya,
 
Umesema tuwe makini na maiti wetu dhidi ya wachawi, tutawezaje kuwa makini ilhali kuna vitu vingine vinaweza kutokea ila kwa macho ya kawaida mtu asijue wala asione kinachoendelea eneo la tukio, tunawezaje kuwa makini katika hali hiyo akhui...? Shukran.
 
Jambo muhimu kabisa maswali mengi yahusiane na kisa hiki au mambo ya ulimwengu wa siri usioonwa kirahisi nitajibu
Nini kazi ya maji yaliyooshewa maiti kwenye maisha ya kawaida...? Naskia pia hata vitu au sehemu iliyotokea kifo watu huchukua mfano kamba aliyojinyongea marehemu, au mchanga wa eneo lilipotokea ajali watu wakafa, hivi vitu vina kazi gani au husaidia nini katika ulimwengu wa kawaida sheikh...? Ahsante.
 
Jambo muhimu kabisa maswali mengi yahusiane na kisa hiki au mambo ya ulimwengu wa siri usioonwa kirahisi nitajibu
Kwa mfano kama kile chungu ulichokitoa chini ya uvungu, mi na mwengine tukitaka kujua humu ndani kuna vitu vinahitaji kutolewa tutajuaje au tutavionaje hivyo vitu kwa macho ya kawaida akhuy...?
 
Kwa nini kumuogopa jini anaetoa mali harakaharaka?
 
Maji ya maiti ni khatari, nasikia wachawi huogea ili wasionekane kwenye shughuli zao za kuwanga
 
Maji ya maiti ni khatari, nasikia wachawi huogea ili wasionekane kwenye shughuli zao za kuwanga
kumbe na wachawi nao huwa wana wanga??? Mana mim nilikuwa najua kuwa wachawi wana chawia tu na kuwanga hyo ni kazi ya wanga. Yani hapo kuna makund mawili yani wachawi pamoja na wanga.
 
Unaweza kunitumia ujumbe kwa kukueleza zaidi
 
Kwa mfano kama kile chungu ulichokitoa chini ya uvungu, mi na mwengine tukitaka kujua humu ndani kuna vitu vinahitaji kutolewa tutajuaje au tutavionaje hivyo vitu kwa macho ya kawaida akhuy...?
Asalam alaykum warahmatullah unafanya shughuli za tiba swahiba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…