Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

story yoyote Ukiandika then ukawa Una ilia Timing inaonekana unaangalia Upepo Jinsi kuiongezea ..okay Any way iran alikuwa kwenye vita vp anaingiaje kwenye story ..
story ya uwongo ukweli waujua mwenyewe ni ya kweli ukweli unaujua mwenye I don't judge you
 
Sina jawabu lolote lakini ukweli ni kuwa haya mambo sio ya kubuni na sihitaji kumlazimisha mtu kuamini ila naamini watu watajifunza kitu kwenye kisa hiki.
Shukrani
 
MUENDELEZO.
Basi njia nzima wakati tunarudi nyumbani nikawa namuuliza baba iwapo yule mzee anamfahamu, kwa kauli yake alisema kuwa hamfahamu na ndio mara ya kwanza anamuona mzee yule, nilimuangalia baba yangu kwa upole sana nikamuuliza kweli baba humfahamu yule mzee? aliposema ndio nikamwambia yule ni mzee Ruhaby, baba alishtuka kidogo na kuuliza nimemjuaje na mbona nilisimama nae muda mrefu kidogo pale masjid.
Nilitamani kumwambia ukweli wote baba lakini niliona bado sio muda sahahi kuyaweka wazi mambo ninayoyaona na kuendelea.
Kwa siku ile pale kwenye mti wa mkuyu na muembe sikuwaona tena wakija mpaka alfajir ya siku ya jumamos baada ya kuchelewa kuamka kwenda kuswali swala ya alfajir ndio nikamuona mzee akiniita niamke nikaswali lakini chaajabu alikuwa ananiita huku taswira yake nikiiona kwenye ukuta wa chumba.
 
Sehemu ijayo ni ya nne nitaendelea nayo nipo kazini Bado.
 
Mkuu pole na majibu ya hovyo ya Hawa mambulula..humu watu wanasumbuliwa na umaskin, uchawi, jobless, maradhi, ujinga na nyege ..wewe ukimaliza tusaidie sisi ikiwemo Mimi tusaidike na msaada wa majini katika sekta mbalimbali za kimaisha ikiwemo uchumi n.k...
 
Mwisho wa kisa hiki nitawapatia njia ya kushirikiana na hawa viumbe katika njia mbalimbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…