Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Hangaya leo karudi toka huko Ulaya alikokuwa.
‘Wenyewe’ wamefurahi sana. Wanadai anaupiga mwingi.
Sasa hebu tuliangalie tena suala la ulinzi wake, kwa kiasi na kiwango ambacho tunaweza kukijadili kutokana na kile tunachokiona.
Akiwa huko nje ya nchi, ulinzi wake huwa ni wa kawaida sana. Hawa askari wanaovaa nguo za kijeshi huku wamebeba yale mabunduki yao makubwa, huwa hawapo kabisa.
Huko huwa anakuwa na walinzi wachache tu.
Lakini pindi anaporudi, hao askari wenye mabunduki makubwa, ambao kipindi cha Magufuli walisemwa kuwa ni Warundi, na wenyewe wanampokea hapo uwanja wa ndege.
Inachekesha kuona sasa hivi hayo maneno ya hao jamaa kuwa ni Warundi hayapo tena, licha ya kwamba sura za hao jamaa bado ni zile zile.
Huo ulinzi mkubwa wa hao wanajeshi hapa nchini ni wa nini?
Ina maana nchi yetu haiko salama kama tunavyoamini kiasi cha kuufanya ulinzi wa Rais nje ya nchi uwe ni mdogo kulinganisha na ule wa hapa nchini?
Rais wetu anakuwa salama zaidi akiwa nje ya nchi kuliko akiwa ndani ya nchi?