Ulioa au kuolewa ukiwa na umri gani?

Ulioa au kuolewa ukiwa na umri gani?

Team kataa ndoa mko wapi mje huku
Hao hawajawahi kuwa na point mbele yangu mkuu kwa sababu nimeshatangulia nalijua pori liko vipi,hata mimi nilikuwa na akili kama zao lakini zenye tafakuri kubwa na nilikuwa najua kwamba uanaume ni ku-face realty.

Mimi kwa kiasi kikubwa maisha yangu nimelelewa na binamu yangu (Mungu Mwenyezi amrehemu) ndoa yake ilivunjika nikiwa naiona mwaka 2001 wakiwa na miaka 12 ndani ya ndoa na nazijua shida alizopitia hadi anakufa but still nimekuja kuoa na nina maisha tulivu standard kwa umri nilio nao,sasa waulize hao wanaokataa ndoa wameshuhudia baya gani hadi wahofie wakati wengi ni under 30 ambao bado wanaishi na wazazi wao ambao hawajatengana?

Nasisitiza shida za ndoa zipo na raha za ndoa zipo mtu asiseme ndoa mbaya kisa amefumaniwa na mkewe nae huyo mkewe akalipiza kisha akajaza vijana sumu kwamba ndoa ni mbaya,hasha.
 
Back
Top Bottom