Sikupingi ila tambua hicho ni kiwanja chenye mgogoro
1,rafiki yangu aliolewa akiwa na mimba mwanaume akahaidi kumhudumia mtoto, mtoto kazaliwa mme kabadilika na vile mtoto ni wa kiume mapenzi yamepungua kwa huyo shoga yangu. Mme hataki kutoa matumizi ya mtoto sasa mm ndo natumika kumbembeleza bava mtoto halisi atume matumizi
2.Ndani ya familiya yetu kabisa kuna binti aliolewa na mtoto mwanzo wa ndoa full mahaba tukafurahi ndogo wetu kapata mme na kampenda mtoto ambae sio wake.tukasema asante yesu. Aiiiiiii nachokwambia sasa hivi huyo mtoto kawa kikwazo mwanaume hampendi kama mwanzo.
Mbaya zaidi waliamua kuwaficha wazazi wa mme, ila tambua pembe la ng'ombe halifichiki, wazazi wamejua, ni vurugu pande zote. Mke/ yaan mdogo wetu hapumui akienda sehemu basi ni kumsingizia kaenda kukutanda na mzazi mwenzi wakati hawana hata mawasiliano.
Mleta mada natamani umuoe huyo dada ila kwa afya ya familiya yako aiseee sikushauri, labda na wewe kama una mtoto hapo sawa.utaweza kuwaconvice wazazi. Lakini pia usije kujipendekeza mtoto utamlea yakikushinda ukashindwa kumuhudumia mkeo akalazimika kuomba matumizi kwa mzazi mwenzie usije kutuchosha haoa kutaka ushauri, wakati unajua incase wakikutana lazima angegede.
Hicho ni kiwanja cha urithi mgogoro kama wote pambana.