Ulipokea vipi Msiba wa Hayati Magufuli?

Japo sikufurahishwa na uongozi wake lakini nilihuzunika ile kibinaadam, ajabu nikasikia mziki mkubwa na sauti za watu kama wanasheherekea hivi kuna Bar kubwa ipo ng'ambo ya Barabara ikabidi nitoke nikajionee wanashangilia ama Wanalia? Lahaulaaa walikua wanashangilia wanamwaga bia, wanacheza mziki, nikasema ama kweli kwenye hii Dunia ishi vizuri na Watu.
 
Akili ili-jam ikashindwa kulitafsiri tukio la msiba huo. Macho yangu yalikuwa yanaona watu wanaomboleza lakini akili bado ilikuwa haiwezi kukubaliana na ukweli huo. Kwa upande mwingine tena macho hayo hayo yaliyokuwa yanawaona waombolezaji, yalikuwa yanapeleka signal kwenye ubongo kwamba hayupo huku akili ikiwa imegoma kuupokea ukweli huo

Imeenda hivyo hadi ukapita muda mrefu na hatimaye kujikuta niko tu kwenye hali ya kujua kuwa hayupo, ila akili yangu haikuwahi kulipokea tukio hilo.

Kwa hiyo kwa maana nyingine, kwa upande wangu mimi ni kwamba sikuwahi kuupokea msiba wa Rais wangu mpendwa JPM; akili iliukataa kwamba haukuwa halisi; I LOVED JPM (RIP)
 
Ama kweli ulikuwa msiba mzito
 
Mbona na hilo jibwa halikufia kijijini kwake Chato?
Ukiishi kiudhalimu utanangwa tu so frustrations zako za kufiwa jiliwaze na chawa wenzako, kuwa chawa wa maiti that's total ridiculous.
All in all kila mja anavuna alichopanda, Jiwe anavuna udhalimu aliofanyia watu.
 
Ilinikuta hivi kwa furaha
 

Attachments

  • VID-20230102-WA0028.mp4
    5.1 MB
Nilichinja kondooaliyenona na kufanya sherehe. Nyama choma na vimiminishi kwa wingi> Kwa hakika ilikuwa siku nzuri sana kwangu na washikaji wangu!
Ni upuuzi wako tu na hao washikaji zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…